Friday, June 24, 2016

Makamu Wa Rais Mhe. Samia Suluhu Akutana Na Waziri Kutoka Malaysia Na Makamu Wa Rais Wa Tigo Afrika


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN ameiomba serikali ya MALAYSIA kujenga ofisi za ubalozi wake hapa nchini ili kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili. 
 
Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo leo Juni 24, 2016 alipokutana na kufanya mazungumzo Waziri asiye na Wizara Maalum Dkt SRI IDRIS JALA ambaye aliongozana na Balozi wa MALAYSIA aliye na makazi yake jijini Nairobi Kenya, ISMAIL SALAM walipomtembelea ofisini kwake Ikulu jijini Dar Salaam.
 
Makamu wa Rais amesema ujenzi wa ofisi za ubalozi huo hapa nchini utarahisisha kwa kiasi kikubwa Watanzania wanaotaka kusafiri kwenda nchini MALAYASIA kwa ajili ya shughuli mbalimbali zikiwemo za masomo na biashara kuliko hali ilivyo sasa ambapo ofisi za balozi hizo zipo Nairobi – Nchini KENYA.
 
Kwa upande wake Waziri asiye na Wizara Maalum Dkt SRI IDRIS JALA amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa nchi yake itaendelea kuimarisha,kukuza na kuendeleza mahusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Malaysia hasa uanzishaji wa ubalozi wake hapa nchini.
 
Hata hivyo, Waziri huyo amesisitiza umuhimu wa kuanzishwa kwa Makubaliano ya pamoja ya ushirikiano kati ya Tanzania na Malaysia ambayo yatajikita  katika sekta mbalimbali zikiwemo za elimu, uchukuzi na biashara.
 
Wakati huo huo, Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN pia amekutana Makamu wa Rais wa TIGO – Afrika RACHEL SAMREN ambapo wamezungumzia masuala mbalimbali ikiwemo namna kampuni hiyo itakavyosadia katika kuwawezesha wanawake kuondokana na umaskini hapa nchini.
 
Katika kuhakikisha taifa linaongeza ukusanyaji wa mapato,
Makamu wa Rais ameuhimiza uongozi wa kampuni ya Simu ya Tigo hapa nchini kuhakikisha unalipa kodi kwa uwazi ili fedha hizo ziweze kusaidia serikali katika kuimarisha utoaji wa huduma za kijamii hapa nchini.

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )