Saturday, June 25, 2016

RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ) - Sehemu ya Nne


Mtunzi: Enea Faidy
Ilipoishia sehemu ya tatu ( kama hukuisoma bofya hapa)
 Dorice akamsogelea Doreen kwa hatua chache.
"Jana ulikuwa na nani pale kwenye mti usiku?" aliuliza Doreen huku akiuchezesha mguu wake wa kulia chini na mkono mmoja akiwa kaushika kiunoni.
"hukuniona au?" aliuliza Dorice kwa mshangao.
"jibu swali!"
"OK! nilikuwa na Eddy"
"nani yako Eddy?"
"Doreen unanitisha ujue?"
"kha! nakutisha nina mapembe hapa? nijibu swali langu"
"Eddy mpenzi wangu!"
"nimekupata sasa... tangu lini Eddy mpenzi wako hujui kama ni mume wangu mtarajiwa?"
"Ati nini....... Eddy ni. .."

 
 Sehemu ya nne
.... DORICE alishtuka sana kusikia Eddy ni mume mtarajiwa wa Doreen hakutaka kuyaamini maneno ya Doreen hata kidogo.
"hivi we Doreen umechanganyikiwa au upo timamu?" Dorice aliropoka kwa hasira.
 
" nikuulize wewe, hivi upo timamu au mwendawazimu unavomng'ang'ania mpenzi wangu Eddy? mpaka watu wanakushangaa! inaniuma sana Dorice usione nimekukaushia!" Alisema Doreen kwa msisitizo wa hali ya juu. Maneno ambayo yalizidi kumuumiza Dorice mpaka machozi yakaanza kumlengalenga machoni mwake. Alimtazama Doreen kwa hasira huku akiumanisha meno yake kwa ghadhabu, moyoni alitamani kumuadhibu vikali Doreen kwa kutaka kulitia DOA penzi lake na Eddy lakini hakuwa na uwezo huo.
 
"Ama kweli kikulacho ki nguoni mwako! sitaki kuamini kama rafiki yangu kipenzi Leo unageuka adui yangu!"alisema Dorice huku akipiga hatua na kutaka kuondoka mbele ya mbaya wake. Lakini ghafla Doreen akamvuta shati na kumrudisha pale alipokuwa amesimama.
 
"we vipi? hebu niache niondoke?"
"nitakuachaje sasa wakati unaniharibia penzi langu na Eddy?" alisema Doreen kwa kujiamini sana huku akibetua midomo yake kwa dharau utadhani Eddy ni mpenzi wake kweli kumbe hakuna lolote ni tamaa na wivu vinavyomsumbua.
 
"umefanikiwa kuniumiza moyo wangu Doreen mpaka najuta kukufahamu.... haya Fanya lolote utakalo tena ili kunyang'anya haki yangu ya mapenzi... do it!" alisema Dorice kwa kwikwi kwani alishindwa kuzuia kilio chake kutokana na maumivu makali aliyoyapata moyoni mwake kwani maneno ya Doreen yalikuwa kama mkuki wenye sumu katikati ya moyo wake.
 
"hata Mimi najuta kukutana na mwanaharamu wewe, Kwa usalama wako achana na Eddy... sijui unanielewa?"
 
Dorice hakusema chochote zaidi ya kumkazia macho ya hasira Doreen, bila kujua kuwa kutazamana na Doreen kwa wakati ule ilikuwa ni kujikaanga kwa mafuta yake mwenyewe kwani Doreen aliitumia nafasi ile vizuri sana. 

Alijibadilisha macho yakawa ya kutisha sana kisha kila alipomtazama Dorice machoni alimhamishia vitu Fulani visivyoeleweka, kisha baada ya hapo Doreen alimsogelea Dorice na kumzodoa lakini haikuwa kumzodoa kwa kawaida Bali alimpaka vitu kama kamasi USO mzima na kumfanya Dorice atie kinyaa sana bila yeye mwenyewe kujitambua.
 
"hebu niondokee hapa mpuuzi wewe na ushukuru Mungu sijakufanya kitu kibaya" alisema Doreen baada ya kuhakikisha amekamilisha kazi yake aliyokusudia kwani sio siri Doreen alipania kumpata Eddy kwa vyovyote vile.
 
Dorice alitembea taratibu na kumfuata Eddy darasani huku akiendelea kulia.

==>Endelea nayo <<Kwa Kubofya Hapa>>

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )