Thursday, July 28, 2016

Rais Magufuli Atengua Uteuzi Wa Mwenyekiti Wa Bodi Ya Mfuko Wa Barabara, Dkt. James Wanyanza Na Kumteua Bw. Joseph Odo Haule Kushika Nafasi Hiyo


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (Road Fund Board) Dkt. James Munanka Wanyancha.

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi iliyotolewa leo Mjini Dodoma imeeleza kuwa Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kuanzia leo tarehe 28 Julai, 2016.

Kufuatia kutenguliwa kwa uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua Bw. Joseph Odo Haule kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Mfuko wa Barabara.

Uteuzi wa Bw. Joseph Odo Haule umeanza leo tarehe 28 Julai, 2016.

Kabla ya uteuzi huo Bw. Joseph Odo Haule alikuwa Meneja wa Mfuko wa Barabara (Road Fund).

Wajumbe wengine wa Bodi ya Mfuko wa Barabara wanaendelea katika nafasi zao.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma

28 Julai, 2016
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )