Monday, August 22, 2016

Audio: Godbless Lema (Mb) amjibu Waziri Mwigulu Nchemba kuhusu Maandamano Septemba 1


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba amezungumza na kusema kuwa CHADEMA wasithubutu kuandamana kwani kwa kufanya hivyo si kuwa watakuwa wanatingisha kiberiti cha njiti, bali watakuwa  wanachezea gesi. Amesema kuwa sio kila kitu mtu anatakiwa kujaribu kwa sababu vingine huenda vikakuumiza.

Waziri ameyasema maneno hayo akiwaasa viongozi wa CHADEMA kutupilia mbali mpango wa maandamano na mikutano ya siasa nchi nzima Septemba Mosi.

Kufuatia kauli hiyo ya Waziri, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema haya. Msikilize hapa chini.

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )