Monday, August 29, 2016

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 31 & 32 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )


Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa


Ilipoishia...
Emmy akanikaribisha kwenye sehemu anayo ishi ambayo yenye vitu vingi vya dhamani ya hali ya juu.Taratibu emmy akaanza kuvua nguo zake moja baada ya nyingine na kunifanya nibaki nikiwa nimemshangaa kwani sikujua ana maana gani na imekuwaje amevua nguo mbele yangu na kubakiwa na chupi wakati mimi na yeye hatuna mahusiano ya namna yoyote

Endelea...
Emmy akachukua taulo na kujifunga kisha akaingia bafuni na kuniacha mimi nikiwa nimekaa kwenye sofa nikiyatadhimini mazingira ya ndani kwake.Baada ya muda kidogo emmy akatoka bafuni.

“umeshindwa hata kuwasha tv?”
“ahaa hakuna tatizo sana”
“ok ngoja nivae nguo tuelekee hospitalini ukamuone mama”
“sawa”
“ila unajua wodi aliyo lazwa?”
“hapana siijui”
“ok basi tutajua huko huko”

Emmy akaingia ndani kwake na akatoka akiwa amevalia mavazi mazuri kiasi kwamba tamaa za mapenzi zikaanza kunitawala na kujikuta nikimtazama emmy kwa macho ya matamanio
“eddy twende zetu”
“mmmmm”
“twende zetu mbon unanishangaa?”
“ahaa hakuna kitu”

Nikanyanyuka na nikatangulia kutoka nje ila kutokana na baridi kali ikanilazimu kumuomba emmy koti na akarudi ndani na kunichukulia koti lake kubwa na sote tukaingia kwenye lifti na kushuka chini gorofani.
“twende huku kwenye maegesho ya magari”
Tukafika sehemu yenye maegesho ya magari mengi na emmy akafungua gari moja na kuniomba niingie.Safari ikaanza huku kila mmoja akiwa kimya ndani ya gari ila emmy akaamua kuvunja ukimya.

“hivi tanzania wewe unafanya kazi?”
“mimi ni mwanafunzi wa a leve bado”
“ohh kumbe unasoma?”
“ndio”
“kombi gani?”
“pcb”
“mungu wangu pcb wewe....Mbona unaonekana kama hkl?”
“hahaa pcb  halisi...Aafu mbona ndege leo imetua kwenye uwanja wa maputo international airport imekuwaje kutokana tumetua mozambique?”

“ndege ilipata itilafu kwa watu kama sisi tunao jua ndio tumegundua hilo ila ukiwa ni mgeni huwezi kujua kama ndege imeshindwa kuendelea na safari”
“sasa si wangetulipa fidia kwa kwa abiria inakuwaje ndege inakuwa haina uwezo wa kumaliza msafara wake?”
“mimi niliamua tuondoke kutokana wewe umeseme unahitaji kumuona mama yako ila kwa walio baki wakisubiria ndege kutengenezwa watakuwa wamelipwa fidia na kama siku ukiondoka utakwenda kupanda ndege uwanja wa kimataifa wa cape town”
“sawa”

Safari ya kwenda hospitalini haikuchukua muda sana hii nikutokana na wingi wa barabara nyingi zinazo punguza msongamano wa magari.Tukafia hospitalini na moja kwa maja emmy akaenda kwenye katabu kinacho onyesha orodha ya wagonjwa waliopo hapa hospitalini na nikamtajia jina la mama kishha akatumi kama dakika tano kulitafuta na akalipata.

“kumbe mama yako ni waziri?”
“ndio”
“twende ukamuone”
“moja kwa moja tukealekea kwenye chumba alicho lazwa mama na kabla hatujaingia nikamkuta askari mmoja akiwa amesimama nje ya chumba alicho lazwa mama

“hamuruhusiwi kuingia humu ndani nyinyi ni kina nani na munahitaji nini?”
“mimi naitwa dokta emmy samson na mfanyakazi wa hii hospitali”
“naomba kitambulisho chako”
Emmy akatoa kitambulisho chake na kumpa askari aliye simama mlangoni na akakisoma kwa muda kisha akamrushu emmy kuingia ndani na mimi nikataka kuingia ndani ila akanizuia kuingia
“na wewe ni nani?”
“mimi ni mtoto wa huyo mama huko ndani?”
“mbona hatuna maelezo ya aina yoyote kuhusiana kama mgonjwa ana mtoto?”

“mimi ni mwanaye unadhani nitafunga safari kutoka tanzania hadi hapa nije kujipendekeza kwa mama yangu?”
Nilizungumza kwa hasira kiasi kwamba watu walipo karibu na eneo la mlango wa kuingia kwenye chumba alicho lazwa wakaanza kunishangaa
“eddy kuwa mpole ngoja nikamuone mama”
“kijana ninakuoma usimame mbali na hili enoa la sivyo nitakuitia walinzi waje wakutoe”
“eddy tafadhali nakuomba uwe mpole nitazungumza na mama na utamuona tu”

Nijaitahidi kutulia hasira zangu na kusimama pembeni kidogo na chumba alicho lazwa mama huku sura yangu ni kiwa nimeikunja.Emmy akaingia ndani ya chumba na baada ya muda akatoka na kumnong’oneza askari kisha kwa ishara emmy akaniita na nikanyanyuka kwa haraka hadi sehemu waliyo simama kisha askari akaniruhusu kuingia ndani.Macho yangu yakatizamana na mama ambaye kwa muonekana hali yake sio nzuri sana japo nimemkuta amaekaa kitako kwa mwendo wa haraka nikamfwata mama na kumkumbatia huku machozi yakinimwagika.

Tukabaki tumekumbatiana na mama ndani ya dakika kadhaa kisha nikamuachia na kuiona sura yake ikiwa imelowana kwa machozi mengi,mama akanishika mashavuni na kunibusu kwenye paji la uso huku akinichunguza sehemu mbali mbali za mwili mwangu na kunifanya nizidi kububujikwa na machozi
“eddy ni nini kilicho kupata mwanagu?”

Mama aliniuliza huku akiwa anabubujikwa na machozi kiasi kwamba nikashindwa kulijibu swali lake hadi ndani ya dakika tano ndipo nikaanza kumuadisia kila kitu kilicho tokea na jinsi baba alivyo nifanyia kiasi kwamb hadi ninamalizia nikamshuhudia emmy akiinama chini huku akitokwa na machozi.
“eddy mwanagu nakuomba unisamehe”
“nikusamehena nini mama?”
“eddy najua siku zote ulikuwa unahitaji kujua ukweli juu ya baba yako na mimi nikawa nimekuficha ila....”
“mama nimesha lijua hilo kuwa pacha wa baba ndio baba yangu”

“nani amekuambia hivyo?”
“mama dunia haina siri tena hili swala nimeambia na mtu baki kabisa tena ni muandishi wa habari”
“basi eddy tuliache hilo mwanagu kwa maana unazidi kunipa uchungua katika hilo”
Ikanibidi nibadilishe mada ya kuzungu na kuzungumza na kuanza kupiga story za kupoteza mawazo hadi mama na emmy wakaanza kucheka ila sikumuambia mama kuhusiana na swala la shule yetu kuingia kwenye matatizo.

==>Endelea Nayo <<Kwa Kubofya Hapa>>
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )