Monday, September 12, 2016

Rais Magufuli Aahirisha Safari Yake Ya ZambiaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha ziara yake  ya siku tatu Nchini Zambia  ambapo pamoja na mambo mengine ilikuwa ahudhurie Sherehe  za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu, ili aweze kushughulikia tatizo laTetemeko la ardhi lililosababisha vifo vya watu 16, mamia wakiwa wamejeruhiwa na nyumba kadhaa  zimebomoka Mkoania Kagera

Kufuatia kuahirishwa kwa ziara hiyo Mheshimiwa Rais Dkt.Magufuli amemtuma Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Kumuwakilisha katika Sherehe hizo za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu

Sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu zinatarajiwa kufanyika kesho tarehe 13 Septemba, 2016 katika jiji la Lusaka


Jaffar Haniu
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi
Dar es salaamAdvertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )