Saturday, October 1, 2016

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 17 & 18


MWANDISHI : EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA...
Samson alizungumza kwa sauti ya ukali, huku akimtumbulia mimacho Rahab
“Unaniuliza wewe kama nani?”
“Sio ninakuuliza kama nani, ila nataka kujua unataoka wapi kumbuka kwamba hapa upo kwangu?”
“Hupaswi kujua, mwehu nini wewe?”
Samson akanyanyuka kwa hasira na kumzaba Rahab kibao cha shavuni kilicho myumbisha hadi kikamuangusha chini

ENDELEA...
Rahab akasimama kwa hasira, akarusha ngumi ambayo Samson aliidaka kwa mkono wake mmoja na kuachia kibaoa kingine kizoto kilicho myumbisha Rahaba na kumuangusha chini.
“Sikiliza wewe mwanamke, hata siku mmoja huto weza kunipiga sawa”
Samson alizungumza kwa kujiamini huku akimtazama Rahab anaye jifikiria kunyanyuka kutoka katika sehemu aliyo angukia.Rahba akarusha teke akikusudia kuipiga miguu ya Samson, ila Samsona akaruka juu na kutua chini, akamnyanyua Rahab kwa mkono mmoja na kumvuta karibu yake
“Nitakuumiza”

Rahab akajaribu kumpiga Samson igoti cha tumbo ila Samson akawahi kurudi nyuma, huku akimsukumiza  nyuma Rahab.Rahab kwa hasira akarusha teke, akiwa hewani Samson akamuwahi kwa kupiga tele la mbavu lililo sababisha Rahab kuangukia kitandani huku akihema
“Usijaribu tena siku nyingine”

Samson alizungumza huku akimtazama Rahab anaye ugulia maumivu ya mbavu zake.Rahab akamtazama Samson kwa jicho kali lililo jaa maswali na mashaka mengi juu ya Samson kwani kwa jinsi alivyokuwa anamchukulia sivyo jinsi Samson alivyo

“Wewe ni nani?” Rahab aliuliza
“Mimi ni Samson, au unahisi mimi ni nani?”
“Ninamaanisha unafanya kazi gani?”
“Haaaa mimi si fundi baiskeli”

Samson akafungua boksi lake la kuhifadhia nguo zake, akatoa bastola mbili na kumkabidhi Rahab,
“Nenda kafanye kazi yako kwa umakini”
Samson alizungumza huku akijilaza pembeni ya Rahab, huku akijifungua vifungo vya shati lake.Rahab akaichunguza moja ya bastola zake na kuikuta ikiwa na risasi za kutosha, kwa haraka akajigeuza na kumkala tumboni Samson na kumuweka bastola ya kichwa.
“Sema wewe ni nani?”

Rahab alizungumza huku jasho jingi likimwagika, Samsona akamtazama kwa umakini Rahab kisha akaunyanyua mkono wake wa kushoto pasipo kuwa na waga na kuushika mkono  wa Rahab alio shika bastola yake na kuusogeza pembeni, mkono wa kulia wa Samson ukapakishika kiuno cha Rahab na kumvuta chini taratibu na sura zao zikawa zimesogeleana kwa ukaribu sana
“Mimi ni fundi baiskeli”

Samson alizungumza kwa sauti ya upole iliyo jaa hisia nyingi za mapenzi, kisha taratibu akaukutanisha mdomo waka nawa Rahab, na kuanza kubadilishaa ladha ya mate yao, kila mmoja akajikuta mwili wake ukisisimka kwa kiasi cha kuzidi kuziinua hisia zao za mapenzi huku kila mmoja akijitahidi kumnyonya mwenzake vilivyo, wakaanza kuvuana nguo moja baada ya nyingine na kujikuta wakizama katika dimbwi kubwa la mapenzi, huku kila mmoja akionekana kuwa na furaha ya kupata penzi la mwenzake
                                                                                         
Ndege maalumu ya jeshi ikawekwa tayari kwa safari ya kuwasafirisha Fetty, Halima, Anna na Agnes, ambao tangu wakamatwe maisha yao yamekuwa ni yakufungwa vitambaa vyeusi machoni, huku mikononi na miguuni wakiwa wamefungwa cheni nzzito ambazo si rahisi kwa wao kuweza kuzifungua.Wakavalishwa mavazi ya rangi ya chungwa, yanayo endana na mavazi ya mafundi gereji wengi.Safari ikapangwa kuondoka nchini usiku wa saa nne

Waandishi wa habar pamoja na wananchi wenye hasira kali na wasichana hawa, wamejipanga pembezoni mwa barabara wakisubiria kuwaona wasichana hao wakipelekwa katika uwanja wa ndege kwa ajili ya kuanza safari ya kupelekwa mahakama kuu ya magaidi.Kila mmoja moyoni mwake akawa na sala kubwa ya kuomba wahukumiwe kifungo cha maisha kwani ukatili ambao wameufanya ni mkubwa, ambao haukuwahi kutokea katika nchi inayosifika kwamba ni nchi ya amani.

Kikosi maalumu cha wanajeshi wapatao ishirini na tano, wakiwa na bunduki zao mikononi, wamesimama nje ya magari kumi aina ya GVC yanayotumiwa kusafirishia wahalifu harari, Sifa ta magari haya ni kwamba hayaingii risasi na yametengeneza kwa uwezo mkubwa wa kuhimiili mikiki mikiki ya majambazi endapo wanaweza kuvamia msafara wao.Nitukio la kihistoria nchini Tanzania kwani haijawahi kutokea ndio maana watu wengi pamoja na waandishi wa habari wanaamu ya kushuhudia jinsi msafara huo utakavyokuwa na ulinzi mkali kupita misafara yote ya magaidi walio wahi kukamatwa na jeshi la polisi

Magari yote kumi yakawa yapo tayari kwa safari, wanajeshi hao wakiwa wanasubiria kuletwa kwa magaidi hao walio chini ya ulinzi mkali wa askari.Simu ya IGP Bwana G.Nyangoi inata zikiwa zimesalia dakika tano tu kabla hawajawafungulia magaidi kutoka kwenye chumba maalimu kilicho tengenezwa kwa kuta za chuma, na  kuwakabidhi katika kikosi maalumu cha jeshi

“Ndio mkuu” Bwana Nyangoi alizungumza baada ya kuipokea simu yake
“Wahalifu , wabadilishieni msafara”
“Muheshimiwa mbona kila kitu tumeshakiweka kwenye utaratibu”
“Hii ni amri na sio ombi, wasafirisheni na sabmarine”
                                                                       
Rahab na Samson, wakiwa wamevalia nguo za wahudumu wa ndege ya raisi aina ya Air Force, wanafnikiwa kuingia katika ndege, pasipo kustukiwa huku Samson akiwa ametengeneza vitambulisho bandia vinavyo endana na wahudumu kwenye ndege ya Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dokta Praygod MakuyaMbaya zaidi katika siku hii, mtaalamu anaye kagua watu wanao ingia kwenye ndege ya raisi kwa kutumia mashine maalumu, anaumwa sana kiasi kwamba ameshindwa kuwemo katika ndege hii ya raisi, na watu wengine hawana utaalamu wa kuitumia mashine hii kutoka ndege ni mpya katika maisha yao.Samson katika mfuko wake wa nyuma wa suruali ameweka kipakti kidogo chenye madawa ya kulevya yenye nguvu kubwa ya kumlewesha mtu katika muda wa dakika tano tuu

Watu wengi wamezoea kumuona Samson kama fundi baiskeli, na ndivyo jinsi watu wengi wanavyo aminni katika hilo, ila sivyo kama watu wengi wanavyo dhania.Samson ni miongoni mwa wapelelezi wa hatari kutoka nchini Somalia katika kundi la Al-Shabab, Wazazi wake ambao kwa sasa ni marehemu ni watanzania na ameishi Tanzani tangu akiwa mtoto mdogo na kupata elimu yake ya msingi katika shule ya St. Mary, ila alipo timiza umri wa miaka kumi na mbili aliwashuhudia wazizi wake, baba na mama wakiuwa kinyama na Bwana Praygod Makuya ambaye kwa kipindi hicho alikuwa ni waziri wa mambo ya nje, wazazi wake walikuwa ni walikuwa ni miongoni mwa wanasiasa mashuhuri nchini Tanzania kutoka katika chama pinzani, kinachokichua chama kilichopo madarakani katika nafasi za kugombania madaraka ya uraisi.


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )