Friday, October 7, 2016

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 21 & 22

MWANDISHI : EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA...
“TATU, MBILI, MOJA”
Mlipuko mkubwa ulio ambatana na moto ukasikika machoni masikioni na watazamaji wa Tv walio kuwa wakilifwatilia tukio zima, na Tv zao zote, ndani ya sekunde mbili zikabadilika na kuwa chenga jambo lililo waacha midomo wazi Watanzania wengine na wengine kushindwa kustamihili ujasiri na kujikuta wakiangua vilio hadharani

ENDELEA...
Ukimya ukatawala miongoni mwa watu wengi walio kuwa wakitazama taarifa ya hivi punde, juu ya Raisi Praygod Makuya kutekwa na kulipuliwa kwenye ndege yake na watu ambao hadi sasa hivi hawajajulikana ni kina nani.Kila mmoja akaanza kuhisi kwamba ni ndoto ya asubuhi ila ndio ukweli halisi kwao, Tv zao zote zikaendelea kuonyesha chenga, jambo ambalo kwa kipindi hicho cha nchi ya Tanzania kutumiamfumo wa ‘Digital’ ni ngumu sana, kuziona chenga za namna hii kama ilivyo kuwa kipindi cha ‘Analogia’

Viongozi wote walio kuwa wamejikusanya kwenye chumba cha mikutano wakifanya wawasiliano namkuu wa jeshi la anga nchini Marekanani, wanabaki midomo wazi huku wengine wenye mioyo myepesi wakijikuta wakimwagikwa na machozi pasipo wao kutarajia.

“Mmmm”
Makamu wa raisi bwana Gift Kalunde anaguna nia yake ni kuwastua ambao bado wamepigwa na bumbuwazi.
“Jamani, kila mmoja amejionea kilicho tokea.Ila niawaomba muendelee na kazi”

Muheshimiwa Gift alizungumza kwa sauti ya unyonge yenye simanzi ndani yake, akajizoa kimya kimya na kutoka ndani ya ukumbi na kuingia kwenye moja ya chumba akajifungia na kuanza kushangilia hadi jasho la mwili likaanza kumwagika.Furaha yake si kuwa raisi wa muda ila furaha yake ni kuona adui yake namba moja ameondoka kwenye hii dunia.
                                                                                                   Anna baada ya kuvuta pumzi ya kutosha akajinyanyua na kushuka kitandani, akapiga hatua hadi mlangoni, akaufunga mlango kwa ndani kisha akarudi kwenye meza yenye computer kadhaa, akazitumbulia mimacho na kuwaona wezake wakiwa kwenye moja ya chumba, akaaendelea kuchunguza chunguza kwenye kila computer, akagundua wapo kwenye Nyambizi ya kijeshi(Submarine)
“Tutatokaje humu?”

Anna alijiuliza swali, huku akitazama kila sehemu ya chumba alichopo, akapiga hatua hadi kwenye moja ya kabati kubwa, akalifungua na kukuta shehena kubwa ya silaha zilizo pangwa vzuri, akachukua moja ya bastola aina ya ‘browning SFS’ na kuichomoa magazine akakuta risasi za kutosha, bila ya kupoteza muda akaanza kukusanya bastola ambazo anaweza kuzibeba kwa wakati mmoja, ambazo zote ni zaaina moja, akaiokota nguo yake na kukuta ikiwa imechanika sana kiasi cha kutowezekana kuvaliwa, Akayazungusha macho yake kwenye kila pande ya chumba na kukuta nguo za Mathias ambazo ni za jeshi zikiwa zimening’inizwa kwenye moja ya msumari, akachukua shati moja, na kulivaa, ambalo ukubwa wake kwake ukawa kama gauni,
“Ni nzuri”

Anna alijisemea mwenyewe kimoyo moyo huku akijitazama kwenye kioo kikubwa cha kabati.Akachukua mkanda wa suruali wa Mathias na kujifunga kiunoni, kutokana na wembamba ikamlazimu kutoboa tobo jipya katika mkanda huo, ili umbane vizuri.Akazichomeka bastola nane kiunoni mwake zote zikiwa zimeajaa lisaha za kutosha, kisha yeye mwenyewe akashika bastola mbili mkononi mwake ambazo zimefungwa viwambo vya kuzuia mlio.
“Bye muheshimiwa tumbo”

Anna alizungumza huku akifyatua risasi kadhaa zilizo tua kwenye tumbo la Mathias Reymond ambaye hadi tayari amesha fariki dunia, alipo ridhika, akashusha pumzi nyingi na kuanza kupiga hatua za haraka kuelekea ulipo mlango, akakishika taratibu kitasa cha mlango na kuanza kuuvuta polepole, akachungulia na kumkuta askari mmoja mwenye mwili mkubwa akiwa amesimama nje ya mlango huku mikono yake akiwa aimeweka kwa nyuma, kama sheria mojawapo ya kijeshi.
“Huyu ndio aliye nileta humu”

Anna alijisemea kimoyo moyo, bila hata ya kupoteza muda akafyatua risasi mbili zilizo ingia kwa nyuma kwenye kichwa askari huyo, na akaanguka kama gunia la chumvi huku kichwa chake kikichanguka kwa nyuma.Anna akaanza kutembea kwa umakini akiifwata njia iliyo nyooka yenye vyumba huku na huku, akiwa katikati ya kordo ndefu gafla mlio mkali wa sauti ya king’ora cha hatari, ikaanza kulia kwa nguvu akaanza kukimbia kabla hajafika mbali.

Gafla akakutana na askari wanne wakiwa na bunduki mikononi mwao na kumuamrisha Anna kunyoosha mikono juu, wazo la haraka likamjia Anna kichwani mwake, akapandishia shati lake juu, na kuziacha sehemu zake za siri wazi na kuwafanya askari hao kubaki wakishangaa, huku baadhi wakimeza mafumba ya mate kwa uchu mkali wa kuto kukutana na mwanamke kimwili katika kipindi kirefu cha wao kushinda ndani ya maji baharini kwenye nyambizi yao.

Sauti ya king’ora cha hatari kikaanza kuwastua Fetty na wezake wawili ambao hadi sasa hivi wapo ndani ya chumba ambacho hawajui ni wapi, walipo
“Nini hicho?” Halima aliuliza
“King’ora cha hatari hicho”

 Fetty alijibu huku akiandelea kusimama katikati ya chumba, huku kichwa chake kikiwa bado kimefunikwa na kofia jeusi, ambalo hadi muda huu wameshindwa kujivua kutokana na mikono yao kufungwa kwa nyuma na pingu.
Askari mmmoja akafungua ndani ya chumba walipo Fetty na wezake kuangalia kama wapo,
“Wewe mpumbavu rudi ukae chini”

Askari alizungumza huku akimfwata Fetty kwenye sehemu aliyo simama, kitendo cha kumsogelea Fetty ikawa ni koso lake kubwa, kwa kutumia hisia kali Fetty aliweza kujirusha na kumtandika askari kichwa kimoja kikali cha pua na kumfanya aanguke chini, kwa hasira askari akampiga mtama Fetty na kumuangusha chini, akamkalia Fetty tumboni na kunza kumshambulia kwa  kumtandika vibao mfululizo vya kichwani.


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )