Saturday, October 22, 2016

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 75 & 76 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

MWANDISHI : EDDAZARIA

ILIPOISHIA
Macho yangu yakakutana na macho ya Lutfia, aliye pembeni ya mwili wa baba yake, aliye fariki dunia. Nikatembea kwa haraka hadi ulipo mwili wa chifu, kabla sijaugusa, nikastukia, Lutfia akinisukuma kwa nguvu na, nikaanguka chini
"Eddy, hupaswi kuugusa mwili wa baba yangu. Haya yote wewe ndio chanzo. Umekisababishia kijiji changu matatizo...."

"Lutfia ila si mimi niliye waua hawa wote"
"Wewe, ni chanzo Eddy, nakuanzi sasa hivi ninakuomba uondoke kijijini kwangu, la sivyo utakwenda kuungana na kifo cha hawa wote walio tangulia mbele za haki"
Lutfia alizungumza kwa msisitizo, huku machozi yakimwagika, ñà kifua chake kikipanda na kushuka kwa kasi akionekana kujawa na jazba kubwa dhidi yangu.

ENDELEA SASA
"Lu....."
"Eddy nimesema ondoka"
Lutfia alizungumza kwa kupaza sauti, hadi wanakijiji wote wakatutizama sisi, natambua hawajui lugha tunayo izungumza ila, matendo yanaashiria kwamba Lutfia hataki kuniona mbele ya macho yake. Nikamtazama Chifu, huku machozi yakinilenga lenga. Midomo ya Lutfia, inatetemeka kwa kufura kwa hasira, uzuri wake alio kua nao umetoweka kabisa.

Taratibu nikauweka chini upanga wangu, kisha nikasimama na kutazamana na Lutfia aliye nitumbulia mimacho kiasi cha kunifanya nimuogope. Kila mwana kijiji ninaye mtazama sura yake imetawaliwa na majonzi mengi, wamama wengine wakiwa wanalia kwa uchungu huku wakigara gara kwenye vumbi, wakionyesha ni jinsi gàni, walivyo umizwa na tukio zima lililo tokea muda mchache ulio pita.

Sikumuangali mtu yoyote usoni zaidi ya kugeuka na kuanza kutembea kwa mwendo wa haraka, ulio changanyika na hasira kali. Nikafika kwenye kijumba changu, nikachukua kibuyu changu, ninacho hifadhia maji ya kunywa, nikachukua na kisu changu cha akiba, na kutoka nje ya kibanda changu. Nikautizama mji jinsi unavyo teketea kwa moto, hasira dhidi ya John ikazi kunipanda. Nikaanzà kutokomea msituni, nikijaribu kutafuta njia ya kutokea kwenye kijiji hiki, kutokana na hasira pamoja na uchungu ulio nitawala moyoni mwangu, nikajikuta nikitembea hadi kuna pambazuka, pasipo kuchoka.

  Nikafika kwenye moja ya mlima mrefu, ulio zingirwa na miti mingi, kwa mbali nikaanza kusikia mngurumo wa gari, likipita eneo la karibu na mlima huu, kwa haraka nikashuka, nikiufwatisha mgurumo huo ni wapi unapo tokea. Kwabahati nzuri nikaiona barabara ya lami, iliyo chongwa kwenye mlima huu. Matunaini ya kufika ninapo pahitaji yakaanza kunijia moyoni mwangu.

Nikasimama, katikati ya barabara. Sikuona aibu kwa jinsi nilivyo vaa nusu uchi, huku sehemu zangu za siri, zikiwa nimezifunika na ngozi ya chui. Mlio wa gari sikuusikia tena, kwani ninahisi lilisha pita, kabla ya mimi kuifikia barabara. Nikaendemea kuzunguka zunguka maeneo ya barabara, nikijaribu kusubiria kama ninaweza kupata usafiri.

Gafla gari moja ndogo, likapita kwa kasi pasipo kufanikiwa kulipungia mkono, ila halikufika mbali sana, likasimama. Dereva wa gari hilo akaanza kulirudisha nyuma kwa kasi, hadi sehemu nilipo simama. Kioo cha upande wa dereva kikashuka, nikamuona mvulana mmija wa kizungu, àkiwa na mchumba wake, wakabaki wakinishangaa kwa jinsi nilivyo vaa.
Binti wa kizungu akatoa kamera yake, aina ya digital, na kuanza kunipiga picha, huku akiwa amesimama upande wa lili wa gari, nikaanza kuwafwata taratibu

"Casey get in the car"(Casey ingia ndani ya gari)
Mvulana huyu, alizungumza kwa haraka baada ya mimi kilikaribia gari lao, kabla hajafanya chochote, nikawahi kuingiza mkono kupitia upenyo wa kioo alicho kifungua. Nikachomoa funguo ya gari lao, nakulifanya lizime. Jamaa akashuka, huku akiwa amekasirika, akajaribu kunirukia, ila nikamuwahi kumtuliza kwa ngumi ya shingo iliyo muangusha chini na kuzimia hapo hapo.

Msichana akajaribu, kukimbia ila nikamuwahi na kumdaka, nikambeba begani na kumrudisha ndani ya gari. Nikachomoa kisu changu na kumuwekea kooni mwake huku kidole changu kimoja kikimpa ishara ya kukaa kimya la sivyo nitamkata kichwa. Nikaufunga mlango wake, ña kuzunguka upande wa pili, sehemu alipo anguka mpenzi wake. Kwa haraka nikamvua nguo mpenzi wake, na kuzivaa mimi japo hazinitoshi sana ila nikazilazimisha kukaa mwilini mwangu.

Nikachukua soksi za jamaa, na kumkandamiza nazo mdomoni, kisha nikamnyanua na kufungua, uoande wa pili wa gari. Kwa bahati nzuri nikakuta kamba, kwa haraka nikamfunga miguuni na mikononi. Kisha nikamuwena vizuri nyuma ya gari, hii yenye viandishi vidogo vilivyo andikwa Verosa, kisha nikafunga, nikarudi alipo mpenzi wake.
Nikamkuta akihangaika na simu yake, akijaribu kupiga namba anazo zijua yeye, kwa bahati mbaya, maeneo tuliyopo hakuna mawasiliano.

Nikampokonya simu yake na kuiweka mfukoni mwangu
"Ukijaribu kufanya ujinga wowote, nitakuu"
Nilizungumza kwa sauti ya ukali nikitumia lugha ya kingereza, jambo lililo mfanya binti huyo kushangaa, kwani nahisi alijua kwamba mimi ni mtu misiye jua lugha yoyote zaidi ya lugha ya jamii niliyo tokea
Nikawasha gari na kuondoka, huku mara kwa mara niki muamrisha binti huyu kunielekeza barabara ya kufika kwenye mji wowote. Mwendo wa karibia masaa tisa, tukafika kwenye moja ya mji wenye nyumba, nyingi sana zilizo tengenezwa kwa mbao
"Hapa ni wapi?"
"Soweto"

Casey alinijibu kwa kifupi huku, akiwa amenuna, kwani hajafurahishwa na uwepo wangu mimi, ndani ya gari hili. Nikasimamisha gari nje ya baa moja, iliyo tulia sana,
"Mbona umesimamisha gari?"
"Nahisi njaa, nahitaji kula, nipatie pesa"
Casey akanitazama kwa woga, taratibu akaingiza mkono wake kwenye, mfuko wa suruali aliyo ivaa, akatoa noti moja ya dola mia na kunikabidhi, nikafungua mlango, kabla sijashuka, nikamgeukia Casey.
"Shuka ndani ya gari, tuongozane"
Casey hakuwa na kipingamizi zaidi yakushuka kwenye gari, tukaingia ndani ya baa hii kwa bahati nzuri tukakuta, sehemu wanauza chakula

"Wewe unaitwa nani?"
Casey aliniuliza kwa sauti ya chini, huku tukiendelea kukisubiria chakula tulicho kiagiza
"Eddy"
"Una jina kama la mchumba wangu"
"Yupi, huyo niliye mfungia kwenye buti ya gari?"
"Hapana, huyo ni kaka yangu, mpenzi wangu yupo hospitali"
"Anaumwa na nini?"
"Alishambuliwa na majambazi, wiki moja iliyo pita"
"Ohoo pole saña, ila hali yake inaendeleaje?"
"Sio nzuri, kwani yupo chini ya uangalizi wa madaktari, kwani alipigwa risasi nne za kifua, alipokua anapeleka pesa benki"

==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )