Friday, January 27, 2017

Huyu Ndio Mshindi Wa Tecno #kamambele…kampeni Ya Kipekee Iliyofunga Mwaka 2016

Kampuni inayoongoza kwa kutengeneza na kuuza simu bora barani Afrika, Tecno Mobile imemtangaza mshindi wa kampeni ya #KAMAMBELE kuwa ni Bw. Goodluck Massawe mwanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Ardhi baada ya kupata kura zaidi ya 6,000 zilizopigwa na mashabiki ambapo mshindi alitakiwa kueleza sababu kwanini anaipenda simu yake ya Tecno. 

Kampeni ya hiyo iliyozinduliwa mwaka jana mwishoni kwa lengo la kuwapatia wateja wake nafasi ya kuzuru nchini Uingereza na kushuhudia mabingwa mara 4 wa Ligi Kuu ya Uingereza klabu ya Manchester City wakicheza dhidi ya mahasimu wao Manchester United. 

Tecno Mobile hivi karibuni ilitiliana sahihi makubaliano ya kufanya kazi na klabu ya Manchester City kama “Official Mobile Partner”

Kampeni hiyo iliwashirikisha Idris Sultan, mshindi wa Big Brother Africa - Hotshots mwaka 2014 na Hamisa Mobetto mwanamitindo maarufu ambao walikuwa kwenye usukani wa #KamaMbele ambapo Idris aliibuka kinara kupitia kura za Watanzania hivyo ataongozana na mshindi Bwana Goodluck Massawe.
 
Katika ubunifu wa aina yake Tecno Mobile ilifanya mahojiano mubashara kupitia ukurasa wake wa Facebook ambapo Idris na Hamisa walipata kupiga stori na mashabiki wao. Mahojiano hayo yaliendeshwa na DJ Lil Ommy ambaye ni mtangazaji katika Radio ya Times FM na kufana kwa kiasi kikubwa.
 
Mshindi wa #KamaMbele alipatikana mwezi Januari 2017 baada ya kupita mchujo wa washiriki zaidi ya 5,000 na kubaki washiriki wanne tu. Baada ya mchujo huo washiriki hao walitakiwa kuomba kura kutoka kwa Watanzania kupitia video zilizotumwa kupitia kurasa za mitandao ya kijamii ya Tecno Mobile na hatimaye Bw Goodluck Massawe kuibuka mshindi. 

Safari ya Idris na mshindi Goodluck Massawe inatarajiwa kufanyika katikati ya mwezi Februari na kufikia kilele chake tarehe 25 mwezi huo huo ambapo watapata nafasi ya kwenda kuangalia mtanange baina ya Manchester City na mahasimu wao Manchester United mubashara jijini Manchester, Uingereza.
 
Huu ni mwanzo tu wa zawadi kutokana na ushirikiano huu baina ya Tecno Mobile na Manchester City, unaweza kujiunga na kutembelea kurasa za kijamii za Tecno Mobile ili kupata habari njema kila zinapotokea. 
 


==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )