Saturday, January 28, 2017

Kasi ya uokoaji watu 14 waliofukiwa mgodini yazidi kupamba moto

Bado kazi ya uokoaji wa watu 14 waliofukiwa na kifusi katika Mgodi wa Dhahabu wa Kampuni ya RZ Union Mining Ltd uliopo Kata ya Nyarugusu mkoani Geita inaendelea, na hadi jana waokoaji hawajafanikiwa kuokoa mtu yoyote.

Pamoja na juhudi hizo za uokoaji, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Ezekiel Kyunga amesema kuwa ana imani watu hao wataokolewa wakiwa hai.

Amesema kuwa jana imefanyika kazi kubwa ya kuchimba kifusi ili kutafuta njia ya kuwafikia waathirika huku mipira zaidi ya Oxygen ikiingizwa chini ya mgodi waliko watu hao ili kuwaongezea hewa.

Aidha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Latson Mponjoli amesema juhudi za uokoaji zinaendelea kwa ushirikiano wa vikosi vya uokoaji vya Kampuni ya Geita Gold Mine (GCM), Jeshi la Zimamoto na Polisi pamoja na kikosi cha ukoaji cha Sekta ya Madini.

Amesema hali ni shwari katika eneo hilo na wana matumaini ya kuwafikia watu hao wakiwa hai.

Pia, Kampuni inayoendesha mgodi huo imesema kutokana na kitabu cha orodha ya watu wanaojiandikisha kuingia mgodini, kuna majina ya Watanzania 12 na Mchina mmoja waliofukiwa kifusini. Ilielezwa kuwa watu pia waliomshuhudia Mtanzania mmoja akingia mgodini humo bila kujiandikisha na hivyo kufanya waliofukiwa kufikia 14.

Watanzania 13 na raia mmoja wa China walifukiwa na kifusi juzi usiku baada ya udongo kuziba mlango waliokuwa wakitumia kuingia na kutoka.
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )