Monday, January 30, 2017

Wanachama 200 Waikimbia CHADEMA na Kujiunga CCM

Chama   cha  Demokrasia  na Maendeleo (Chadema), kimeendelea  kupata  pigo  baada  ya  wanachama  200, wakiwamo  viongozi  wa Kitongoji  cha Kwemghogho Mahezangulu kujitoa  na  kujiunga  na  Chama Cha Mapinduzi (CCM) .

Akizungumza  baaada ya  kupokea  wanachama  hao, Mbunge wa  Bumbuli, January Makamba (CCM),  alisema  wananchama  hao  wameamua  kurudi  wenyewe nyumbani   kutokana  na   kuona  ahadi  nyingi  za maendeleo zimetekelezwa  kwa  kiasi kikubwa.

Alisema  chama  chake kimefanya mambo mengi  hivyo  haoni  ajabu  ya  kupokea  wanachama kutoka  vyama  vingine  vya  upinzani.

January, ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, alisema  hivi sasa kuna kazi kubwa ya kuendelea kuleta maendeleo ambayo yanahitaji umoja  na mshikamano.

Alisema migogoro, majungu na fitina inatokana na kambi  zilizokuwapo huku akiwasisitiza wana CCM watambue ni hema kubwa na linavumilia tofauti za watu.

Aliyekuwa  Mwenyekiti wa  Chadema  Kitongoji cha Kwemghogho, Shabani Kahema,  aliwataka   vijana  na  wanachama  wengine  kubadilika kwa kuwa CCM ndiyo chama chenye ilani inayotekelezeka.
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )