Saturday, February 25, 2017

Bodaboda Dar es Salaam mwisho saa 6 usiku

Jeshi ya Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limetoa wito kwa madereva bodaboda katika Jijini la Dar es salaam, kuacha kufanya shughuli hiyo ifikapo majira ya saa 6 usiku ili kupunguza uhalifu.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Simon Sirro, amesema kuwa jeshi hilo limebaini wahalifu wengi hutumia mwanya katika muda huo kutenda uhalifu ikiwa ni pamoja na kuwadhuru waendesha pikipiki.

Aidha, Kamanda Sirro, amesema, kuanzia Februari 18 hadi 23 Jeshi la Polisi Usalama Barabarani limefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi milioni 460 kutokana na makosa mbalimbali ya barabarani pamoja na kukamata pikipiki 1,280 kati ya hizo pikipiki 30 zimekamatwa kutokana na kupita katika njia ya mabasi yaendayo haraka huku madereva 27 wakifikishwa mahakamani.

Kuhusu suala la dawa za kulevya, Sirro aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mpaka sasa limefanikiwa kukamata jumla watuhumiwa 257 pamoja na kete za dawa za kulevya 1,526, puli 112 na misokoto ya bangi 247 kutokana na oparesheni inayoendelea.

Alisema baadhi ya watuhumiwa bado awajafikishwa mahakamani kwani upelelezi bado haujakamilika na mara baada ya upelelezi kukamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )