Friday, February 17, 2017

Mose Iyobo amchana tena Harmorapa

Dancer Mose Iyobo ambaye ni mpenzi wa Aunty Ezekiel amefunguka na kusema kuwa yeye haamini kama Harmorapa ana jina kubwa na wala hajawahi kusikia kazi yake yoyote ile na kusema hana ushauri wowote kwake, huku akimchana kuwa amekurupuka kwenye muziki.

Mose Iyobo alisema hayo kupitia eNewz ya EATV  na kudai kuwa muziki unahitaji mtu kujipanga ili uweze kumlipa lakini siyo kukurupuka kama ambavyo Harmorapa amefanya.

"Mimi ni mtu ambaye nipo kwenye muziki muda mrefu, kila siku nyimbo mpya zinapotoka ziwe za watu maarufu hata wasio maarufu nazisikia lakini mimi sijawahi kusikia kazi yoyote ya Harmorapa, kwa hiyo sina cha kumshauri ila hiyo kazi anayofanya inahitaji mtu makini, anayeenda na wakati na siyo kukurupuka tu na kufanya ghafla sababu hiyo kazi ina pesa nyingi sana na inatia umasikini kwa haraka sana kama haufanyi vile inavyotakiwa" alisema Mose Iyobo

Hii ni mara ya pili kwa Mose, kumchana Harmorapa, mara ya kwanza, alitoa kauli ya kumfananisha harmorapa na 'nyani'
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )