Saturday, February 18, 2017

Serikali yajipanga kuzuia uvutaji sigara hadharani

Wizara ya Afya ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema ipo katika hatua za mwisho za kutayarisha mwongozo wa kupiga marufuku matumizi ya uvutaji wa sigara hadharani ili kudhibiti maradhi yasiyoambukiza yanayotokana na sigara.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo wakati akitoa ufafanuzi kuhusu uvutaji wa sigara hadharani katika sehemu za mkusanyiko na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi.

Alisema tayari Wizara ya Afya imewasilisha muswada wa kulinda afya ya jamii ambao moja ya kazi yake kubwa ni kupambana na matumizi ya sigara katika jamii na sehemu za mkusanyiko.

Akifafanua zaidi, alisema utafiti uliofanywa kuhusu maradhi yasiyoambukiza unaonesha kwamba upo kwa asilimia 38 ambayo yanahusishwa na uvutaji wa sigara.

Kombo alisema mwongozo huo ukikamilika utaletwa mbele ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na wajumbe kutoa maoni yao kabla ya kufanya kazi na kuwa sheria inayotakiwa kutekelezwa na kusimamiwa.

Alisema yapo matumizi mabaya ya uvutaji wa sigara hadharani ikiwemo sehemu za mikusanyiko ya watu kama hospitalini na sehemu za kusubiri usafiri wa abiria na kusababisha madhara makubwa ambayo hayaonekani kwa mara moja.
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )