Friday, February 24, 2017

SORRY MADAM -Sehemu ya 35 & 36 (Destination of my enemies)

MWANDISHI:EDDAZARIA G.MSULWAILIPOISHIA

 ILIPOISHIA
‘Ina maana huyu mshenzi bado yupo hai?’
Raisi Praygod alizungumza kimoyo moyo huku akiutazama mwili wa Lukuman kwa hasira kali
“Irudisheni sura yake halisi na mutangaze waziri Eddy Godwin amefariki dunia. Hii si ombi bali ni amri”
Raisi Praygod alizungumza kwa msisitizo kisha akatoka ndani ya chumba hicho kwa hasira na kumuacha mkemia mkuu wa serikali akiwa ameduwaa uamuzi huo ulio chukuliwa na muheshimiwa raisi.

ENDELEA
  ***
Vishindo vikazidi kusikika nje ya mlango wa chumba cha siri walimo Eddy aliye poteza fahamu pamoja na Samson ambaye macho yake yote ameyaelekezea kwenye mlango huo, gafla mlango huo ukafunguka, na wanajeshi wane wakajikuta wakiingia ndani pamoja na mlango huo. Samson kwa haraka akaanza kuwashambulia wanajeshi hao kwa kuwavunja shingo zao, huku baadhi yao wakitoa vilio vya maumivu makali.

Wanajeshi wengine walio kuwa nje wakajikuta wakifyatua risasi hovyo hovyo pasipo kujua ni nani anaye washambuli. Samson akatoka kwa mwendo wa kasi na kupita katikati yao na kuanza kuwashambulia kwa kuwaua kinyama pasipo huruma. Idadi ya wanajeshi wote walio weza kufika nyumbanbi kwa Eddy, wakauawa.

Bila ya kupoteza muda Samson akarudi ndani ya chumba na kumchukua Eddy aliyekuwa amemuhifadhi kwenye sehemu ambayo haikuwa ni raisi kwa risasi kuweza kumfikia. Akamuingia kwenye gari yao na kuondoka maeneo ya jumba hilo la kifahari.

Kila simu ya upepo iliyokuwa ikipigwa  kwa kiongozi wa kikosi hicho kujua ni nini kinacho endelea katika eneo hilo haikuweza kupokelewa, ikabidi watumwe wanajeshi wengine watano kwenda kutazama ni kitu gani ambacho kinaendelea kwenye eneo la tukio.

Wanajeshi walio fika kwenye eneo la tukio hawakuamini macho yao kuwakuta wezao wote wakiwa wamelala chini huku wakiwa wameuwa kifo kinacho onyesha muuaji hakuweza kutumi silaha bali ni kitu chenye ncha kali kama kucha, zilizo weza kuwaparuza wengi wao kwenye sehemu mbalimbali za miili yao.

     ***
Mkemia mkuu wa serikali bwana Ignatus Mkama, hakuwa na jinsi yoyote yakufanya kwani amri aliyo pewa na raisi Praygod alilazimika kuweza kuitekeleza mara moja. Akaitisha mkutano na waandishi wa habari walio weza kuweka kambi katika hospitali ya muhimbili kujua ni kitu gani kinacho endelea kuhusiana na kifo cha waziri wa ulinzi Eddy Godwin.

“Nimedhibitisha ya kwamba aliye kuwa ni waziri wa ulinzi na mtoto wa waziri mkuu mstafu. Eddy Gdowin, amefariki dunia”
Waandishi wa habari wa magazeti, redio na televishion hawakusita kuuliza maswali kwa bwana Ingatus Mkama.

“Je kifo chake kimesababishwa na nini?”
“Kifo chake kimetokana na kupigizwa chini sehemu ya nyuma ya kichwa chake, ambapo kulipelekea mpasuko mkubwa kwenye ubungo wake na damu iliweza kuvuja na kupelekea ubongo wake kuweza kuganda na ndipo mauti yalipo chukua mauti yake”

  ***
“Kijana usipo weza kuzungumza kitu cha aina yoyote hakika unaweza ukafia katika mikono yetu”
Mmoja wa askari wapelelezi aliye ingia kwenye chumba cha mahojiano kumuhoji Briton huku akiendelea kumzunguka Briton aliye kalishwa kwenye kiti huku miguu na mikono yake ikiwa imefungwa pingu.

Briton hakuzungumza kitu cha aina yoyote tangu akamatwe kwenye chumba hicho, macho yake makali na yaliyo jaa dharau akaendelea kumtazama mpelelezi huyo ambaye mara kadhaa alimuhoji maswali ambayo hakuwa tayari kuweza kujibu.

“Ninaimani wapo watu ambao wapo nyuma yako si ndio, hembu niambie ni kina nani hao ili niweze kuwatambua”
“Nina weza kukuamini?”
Briton alimuuliza mpelelezi huyo ambaye kwa haraka akaweza kukaa kwenye kiti kilichopo mbele ya meza kumsikiliza Briton aliye patiwa matesi makali ila hakuweza kuzungumza kitu cha aina yoyote.

“Ndio kwa maana mimi siwezi kuwa kinyume na wewe, na ukiniambia ukweli basi nina uhakika nitakuwa upande wako”
“Kwa maana sisi tunahitaji watu ambao wapo nyuma yako, au unahitaji kusema kwamba waziri Eddy ndio alikuwa kiongozi wenu mkubwa au?”

Briton akatabasamu na kucheka kichoko kidogo cha dharau, akakitazama chumba chote na kukuta kameza mbili za ulinzi zikiwa katika kona tofauti katika chumba hicho, kwa uzoefu wake akatambua kabisa mazungumzo hayo yanarekodiwa na kutazamwa na watu wengi, waliopo nyuma ya kioo kikubwa ambacho hakionyeshi nje ila watu wa nje wanaweza kuona ndani.

“Kuna mtu nahitaji kuonana naye hapa hapa ndani ya Tanzania”
Maneno hayo ya Briton alipo kuwa akiyazungumza Bwana Mgwira naye ndio alikuwa amefika kwenye ofisi ya kusikilizia mahojianop hayo yanayo fanywa upande wa pili wa chumba hicho.

“Ni nani huyo?”
Mapigo ya bwana Mgwira yakaanza kumuenda mbio, kwani hakujua ni nani ambaye Biton anakwenda kumtaja, na endapo atakuwa ni yeye basi siri ya D.F.E inaweza kufichuka kwani yeye naye anaweza kufanyiwa mahojiano ili kuzungumza ana mahusiano gani na Briton.

Briton akakaa kwa muda huku akianza kukumbuka baadhi ya matukio yaliyo tokea kipindi cha nyuma akiwa ndio anaingia kwenye kundi la Al-Shabab akiwa kijana mdogo, akamkumbuka jinsi alivyo weza kuishi na Shamsa, hadi wakapotezana kwenye moja ya kazi ambayo walipewa kwenda kuvamia moja ya nyumba iliyo sadikika kwamba ina watu wanao tafutwa na bosi wao katika kipindi hicho. Akakumbuka pia jinsi jana usiku alivyo weza kukutana na Shamsa anaye amini ni wake.

Akakumbuka jinsi Shamsa alivyo muita Eddy baba, taratibu picha ikaanza kumjia kichwani mwake na kuamini kwamba mtu aliye weza kuishi na Shamsa kwa kipindi chote hicho ni Eddy.

Briton akashusha pumzi nyingi huku akimtazama mpelelezi huyo, taratibu akajinyoosha, huku maumivu makali ya kipigo alicho kipata yakiendelea kuutesa mwili wake.
“Nahitaji kuonana na binti mmoja hivi, yupo ndani ya Tanzania”
Bwana Mgwira akashusha pumzi nyingi kusikilizia ni nani huyo binti.

“Anaitwa nani?”
“Shamsa”
“Shamsa……Ila ndani ya Tanzania wasichana waoa itwa Shamsa ni wengi?”
“Nalijua hilo, ila nahitaji kuonana na huyo la sivyo hakuna chochote ambacho munaweza kukijua kuhusiana na mimi, mutanipiga hadi nife, ila sinto kuwa tayari kuzungumza chochote”
Briton akakaa kimya na kuwaahia kazi nzito wapelelezi walio pewa kazi ya kuweza kumpeleleza na kuweza kupata ukweli kuhusiana na kazi yake ya kigaidi anayo ifanya.

***
“What……..!!!!?(Nini…………..!!!!?)
Raisi Praygod alizungumza huku akiwa katika hali ya mshangao
“Ndio muheshimiwa wanajeshi wote wameuawa”
“Wameuawa kivipi?”
Raisi Praygod alibabaika huku akiwa ndani ya gari akielekea ikulu akitokea hospitali ya Taifa.
“Hata sisi wenyewe hatufahamu muheshimiwa”
“Dereva geuza gari tunaelekea nyumbani kwa waziri Eddy”

Raisi Praygod alizungumza huku akiikata simu hiyo, kichwani mwake alihisi kuchanganyikiwa. Mawasiliano yakafanywa kwa madereva wote walipo kwenye msafara wa raisi, gari zote nane zilizo ongezeka baada ya walinzi wengine kugundua raisi aliondoka ikulu kisiri pasipo wao kujua, zikageuzwa kwa mtindo ulio wafanya  wananchi wengi walio kuwa karibu na barabara hiyo kushangaa, kwani ziligeuzwa kwa mwendo wa kasi sana.

Ving’ora vya gari zote zilizo tangulia mbele vikawashwa, madereva wote wagari zilizopo barabara ambayo raisi Praygod anapita, walizisogeza pembeni gari zoa, ikiwa ni amri endapo msafara wa raisi unapo pita.

Haikumchukua muda sana Raisi Praygod akafika kwenye jumba la Eddy akiwa na msafara wake na walinzi wakutosha, waandishi wa hhabari pamoja na wananchi walio kuwa karibu na eneo la jumba hilo waliweza kukushanyika nje ya geti kubwa wakishuhudia tukio jengine ambalo hapakuwa na aliye elewa ni kitu gani kilicho tokea, huku baadhi yao walio hojiwa na waandishi wa habari walidai kwamba walisikia milio ya risasi majira ya alfajiri, ila hawakuweza kutoka kohofia maisha yao, kwani tukio la jana tu liliweza kuwaogopesha kila mmoja aliye sikia au kuadisiwa.

Raisi Praygod moja kwa moja akapelekwa kwenye maiti zilizo funikwa za wanajeshi walio weza kupoteza maisha, ikafuniliwa maiti moja iliyo weza kutolewa koromeo, Raisi Praygod akajikuta akifumba macho pasipo kupenda kwa maana maiti hiyo inatisha sana.

“Muheshimiwa hadi sasa hivi hatujaweza kujua ni nani aliye weza kufanya tukio hili kwa maana hapakuwa na alama yoyote ya risasi kwenye miili ya maiti zote”
“Hakikisheni munatafuta na kutambua ni nani aliye weza kuhusika na haya mauaji”
“Sawa muheshimiwa”

***
Habari za kifo cha waziri Eddy, zikapokelewa kwa mitazamo tofauti toafauti na wananchi wa Tanzania, wengine waliweza kushangilia kwa kifo hicho kilicho dhibitishwa na mchunguzi mkuu wa serikali na kutangazwa hadharani kupitia vyombo vya hatai.

Wananchi wengine waliweza kuipokea taarifa hiyo kwa unyonge haswa wale wana mtambua waziri Eddy. Baadhi yao wakabaki na maswali mengi wakijiuliza ni kwanini kiongozi huyo aliweza kufanya tukio hilo la kuwaangamiza wananchi wasio kuwa na hatia. Shamsa akawa ni miongoni mwa wananchi walio weza kushuhudia taarifa hiyo kwenye sehemu hiyo aliyo kaa, yenye Tv ndogo kwa ajili ya watu wanao jipumzisha katika eneo hilo.

Shamsa akajikuta akipata nguvu na kunyanyuka, kijana aliye kuwa akimsaidia tayari alisha ondoka, baada ya kuitwa na baba yake walio fika kutazama dada yake aliye jeruhiwa katika tukio la kigaidi Mlimani City.

Akaanza kutembea kuelekea kwenye chumba cha kutazama maiti, akajitahidi kutembea hivyo hiyo, akijkaza kikike. Alipo hisi kuchoka, alitafuta sehemu akapumzika kwa dakika kadhaa kisha akaendelea na safari yake hiyo hadi akafanikiwa kufika kwenye jengo hilo la kuhifadhia maiti, akakuta watu wengi wakiwa wamekaa kwenye eneo hilo, baadhi yao wakimwagikwa na machozi akatambua kwamba hao ni miongoni mwa watu walio ondokewa na ndugu zao.

Ulinzi mkali wa polisi ulizidi kuimarishwa eneo zima eneo hilo la jengo la kuhifadhia maiti, hususani katika chumba alicho lazwa Lukuma ambaye anasidikika kuwa ndio Eddy.
“Samahani dokta”
Shamsa alizungumza kwa sauti ya kinyonge sana.
“Bila samahani?”
“Nahitaji kuona maiti ya baba yangu?”
“Kusema kweli mimi sihusiki na sehemu hii, kwa kukusaidia nenda pale kwenye dirisha la mapokezi ukizungumza utaweza kuonyeshwa maiti yako”

Daktari huyo baada ya kuzungumza hivyo akaondoka zake na kumuacha Shamsa akitazana kundi kubwa la watu walio kusanyika kwenye dirisha hilo, kila mmoja akijaribu kujua kama ndugu yake yupo kwenye jumba hilo. Akajikongoja hadi kwenye dirisha hilo, akasimama kwa muda kutazama kama anaweza kupata msaada wa kuuliza jina la Eddy, lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba anamuona Eddy aliye fariki, kwa bahati nzuri akafanikiwa kupata kijiupenyo akafanikiwa kufika kwa dirishani.

“Namuulizia Eddy Godwin”
Shamsa alizungumza kwa sauti ya chini
“Nani hembu zungumza kwa sauti ya juu usilete lete mapozi”
Jamaa huyo aliye onekena kuchoshwa na kuti kubwa la watu alizungumza kwa hasira
“EDDY GODWIN”
Shamsa alizungumza kwa sauti ya juu, na kumfanya jamaa huyo kuanza kuchambua faili lake kwa haraka, akihisi binti huyo atakuwa anamuulizia Eddy mwengine kwani Eddy anaye mfahamu yeye anahisi ahusiani na binti huyu mwenye asili ya kiarabu.

“Binti hakuna jina kama hilo”
“Baba yangu ni waziri aliye kufa Eddy Godwin, unataka kusema humjui wewe”
Shamsa alizungumza kwa sauti ya ukali huku machozi yakimlenga lenga, na mkono wake mmoja akiwa amejishika tumboni mwake akijaribu kuyazuia maumivu makali anayo yapata. Baadhi ya watu waliyo yasikia maneno ya Shamsa wakajikuta wakimtazama marambili mbili, wengine wakianza kunong’onezana na mmoja wao akaropoka

“Jamani huyu ni mototo wa gaidi”
Kitendo cha jamaa huyo kuzungumza hivyo akamfwata     Shamsa kwa nyuma na kumsukumia pembeni, na kuanza kuzua vurumai, iliyo wabidi polisi kuweza kuwahi katika eneo la tukio na kumchomoa Shamsa, aliye anza kushambuliwa kwa makofi na mangumi na wananchi hao walio kuwa na hasira dhidi ya Eddy Godwin aliye waulia ndugu zao.

 
Advertisement
tang
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )