Friday, March 10, 2017

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aisifu Tanzania

Katibu  Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres ameisifu Serikali ya Tanzania kwa jitihada zake za kutafuta amani nchini Burundi.

Guterres alitoa pongezi hizo wakati aliposimama kwa muda katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wa jijini Dar es Salaam akitokea Kenya.

Katibu Mkuu huyo mpya wa UN alisimama kwa ajili ya kufanya mazunguzmo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk Augustine Mahiga.

Pamoja na mambo mengine Guterres alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa serikali kwa juhudi zake za kutafuta amani nchini Burundi kupitia kwa Msuluhishi wa mgogoro huo, Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa.

“Tanzania imekuwa kinara wa amani Afrika na duniani na naipongeza kwa dhati katika jitihada zake inazozifanya za kutafuta amani ya Burundi na katika nchi nyinge za ukanda huu,” alisema Guterres.

Aidha alisema anatambua mzigo mkubwa inaoupata kama nchi kutokana na kuendelea kupokea wakimbizi kutoka Burundi, na kuahidi UN kuendelea kuunga mkono jitihada za kutafuta suluhu ya kisiasa nchini humo.

Kwa upande wake; Balozi Mahiga aliwasilisha salamu maalum kutoka kwa Rais John Magufuli kuhusiana na hatua iliyofikiwa ya usuluhishi wa mgogoro wa Burundi na ushiriki wa Tanzania katika vikosi vya Umoja wa Mataifa vya ulinzi wa amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Balozi Mahiga pia alisema Tanzania imefurahishwa na ujio wake na Rais amempa mwaliko rasmi wa kufanya ziara nchini.

Aidha alimweleza kuwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), katika mkutano wao ujao wana mpango wa kuwasilisha hoja maalum kuhusu hali ya kisiasa nchini DRC.

Mbali na kufanya ziara nchini Kenya, Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alitembelea Somalia na kukutana na Rais mpya wa nchi hiyo, Hassan Sheikh Mohamud, ambapo aliagiza Jumuiya ya Kimataifa kuchukua hatua kuepusha balaa la njaa nchini humo, kutokana na hali mbaya ya ukame.

==


Advertisement
Punguzo la Bei 20% msimu huu wa Idd.Agiza saa hii ya Automatic, na lipa mzigo ukifika majiji yote TanzaniaAdvertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )