Monday, March 6, 2017

Mabasi Happy Nation na Abood yagongana na lori Mlima Kitonga na Kujeruhi Watu 12

Watu 12 wamejeruhiwa na watatu kati yao wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa baada ya kutokea ajali iliyohusisha magari mawili ya abiria na lori moja, katika eneo la Mlima wa Kitonga wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.

Akizungumza  baada ya kutokea kwa ajali hiyo ,  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Julius Mjengi alisema magari yote matatu yaliyohusika kwenye ajali hiyo yalikuwa yakienda jijini Dar es Salaam.

Ameyataja mabasi yaliyohusika kwenye ajali hiyo kuwa ni ya Kampuni ya Happy Nations, Abood na gari moja la mzigo.

Mjengi amesema katika ajali hiyo watu 12 walipata majeraha na watatu kati yao wamefikishwa Hospitali ya Rufaa ya mkoani Iringa kwa matibabu na tisa kati yao walitibiwa na kuruhusiwa kutoka hospitali.

Kamanda huyo ametaja chanzo cha ajali kuwa ni dereva wa gari la Abood lililokuwa nyuma ambaye aliligonga basi la Happy nations ambalo nalo liligonga gari lilikuwa mbele yake na kusababisha magari yote kuserereka na kutoka pembeni mwa barabara.

==


Advertisement
Punguzo la Bei 20% msimu huu wa Idd.Agiza saa hii ya Automatic, na lipa mzigo ukifika majiji yote TanzaniaAdvertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )