Thursday, March 9, 2017

Mbowe alivyoshiriki msiba wa Mama Mdogo wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete

Msiba wa mama mdogo wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, umewakutanisha kwa mara ya kwanza hadharani kiongozi huyo wa Serikali ya awamu ya nne, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Bernard Membe.

Wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, viongozi hao walionekana mahasimu zaidi baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, jina lake kukatwa katika kinyang’anyiro cha mbio za urais ndani ya CCM na kuhamia Chadema.

Baada ya Uchaguzi Mkuu kumalizika, Rais huyo mstaafu hakuwahi kuonekana hadharani akiwa na viongozi hao wa upinzani, huku Membe yeye akiwa haonekani kabisa kwenye mambo ya siasa wala mikusanyiko yoyote ile.

Lakini jana mazishi ya mama huyo, Nuru Khalfan, mbali ya kuwakutanisha viongozi hao, yaliwakutanisha pia Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda na Waziri wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni, Nape Nnauye.

Wengine walioudhuria ni Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo.

Waziri mkuu, Kassim Majaliwa, ndiye aliyeongoza mamia ya waombolezaji kwenye mazishi hayo yaliyofanyika Bagamoyo mkoani Pwani.

Mara baada ya kumalizika kwa mazishi hayo, Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, aliwashukuru wananchi wote waliojitokeza kushirikiana nao kwenye msiba huo.

Alisema madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Muhimbili wamefanya kazi kubwa katika kipindi alichokuwa bibi yake amelazwa.

"Naomba niwashukuru madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa sababu wamefanya kazi kubwa sana katika kipindi chote ambacho mgonjwa amelazwa hadi alipofariki," alisema Ridhiwani.
==


Advertisement
Punguzo la Bei 20% msimu huu wa Idd.Agiza saa hii ya Automatic, na lipa mzigo ukifika majiji yote TanzaniaAdvertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )