Monday, March 27, 2017

Rais Magufuli ateua Makamishna sita wa Jeshi la Uhamiaji

Rais John Pombe Magufuli amewapandisha vyeo maafisa sita wa Uhamiaji kuwa Makamishna kuanzia februari 28, mwaka 2017 na kuwateua kushika nyadhifa mbalimbali katika Jeshi hilo.

Wateule hao ni Mrakibu wa Uhamiaji (SI) Edward Peter Chogero kuwa Kamishna wa Divisheni ya Fedha na Utawala pamoja na Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji (SSI) Samwel Rhobby Magweiga kuwa Kamishna wa Divisheni ya Udhibiti na Uongozi wa Mipaka.

Wengine ni Mrakibu Mwandamizi (SSI) wa Uhamiaji Gerald John Kihinga kuwa Kamishna wa Divisheni ya Pasipoti na Uraia, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji (SSI) Musanga Mbusuro Etimba ambaye anakuwa Kamishna wa Divisheni ya Hati za Ukaazi na Pasi.

Aidha Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji (SSI) Hennerole Morgan Manyanga ameteuliwa kuwa Kamishna wa Divisheni ya Sheria.

Rais amemteua pia naibu Kamishna wa Uhamiaji Mourice David Kitinusa kuwa Kamishna Chuo cha Uhamiaji  cha kikanda (TRITA)

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja Jenerali Projest Rwegasira, amesema kuwa uteuzi huo unaanzia februari 28, mwaka 2017.
Advertisement
tang
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )