Sunday, March 12, 2017

SORRY MADAM -Sehemu ya 39 & 40 (Destination of my enemies)

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWAILIPOISHIA

ILIPOISHIA
“Moja, hakikisha kwamba unaurudisha uhai wa Eddy Godwin”
“Mbili ndani ya masaa 48, Eddy awe amerudi madarakani la sivyo bomu hili litaisambaratisha ikulu yako”
Simu hiyo ikakata, huku video iliyo kuwa inaonekana kwenye tv hiyo ikapotea na kubakisha mwanga wa bluu wa tv hiyo kubwa, watu wote waliomo ndani ya ofisi
hiyo wakabaki wakimtazama raisi Praygod azungumze kitu juu ya hilo.

ENDELEA
Jasho jingi likazidi kumwagika raisi Praygod, hakuwa na jambo la kuweza kuzungunza na wala hakuweza kutambua ni wapi alipo Eddy.
"Muheshimiwa Eddy si amesha kufa sasa itakuwaje?"
Mmoja wa wafanyakazi wake walinuuliza
"Yupo hai"
Kila mmoja akabaki akiduwaa, baada ya kulisikia hilo swala, raisi alipo ligundua hilo akakohoa kidogo.

"Endeleeni na kazi"
Akatoka ndani ya ofisi yake na kuelekea katika eneo lake la kulala, kichwani mwake akazidi kujiuliza ni nani aliye weza kuufanya mchezo huo kwani wataalamu wake walipo jaribu kutafuta ni eneo gani simu hiyo ya vitisho ni wapi ilipo tokea hawakuweza kuipata. Kitu kilicho zidi kumuumiza zaidi ni wapi alipo kuwepo mke wake kipenzi Shamsa, kwani inasadikika tangu atoke jana majira ya asubuhi kutokana na taarifa aliyo pewa, hakuweza kurejea kabisa hadi majira haya ya asubuhi.

Akafungua moja ya droo yake na kutoa vidonge viwili na kuvimeza pasipo hata kunywa maji, akavisukumiza kwa mafumba kazaa ya mate kisha akasimama mbele ya kioo kikubwa kilichopo mbele ya chumba chake na kujitazama uso wake ulio jaa wasiwask, iliyo changanyikana na hasira kali sana.

"EDDY, EDDY, EDDY"
Raisi Praygod alizungumza huku jazba ikizidi kuongezeka kifuani mwake. Taratibu akakisogelea kitanda na kujilaza, huku akihema taratibu taratibu.

***
Mwanga mkali wa jua ukaanza kupenya kwenye macho ya mtubaliye lala kitandani huku mwilini mwake akiwa amebakiwa na boksa tu. Akajaribu kunyanyuka kitandani ila maumivu makali ya paja yakamfanya kurudi tena kitandani. Kwa sekunde kadhaa akatumia kuchunguza kufahanu ni wapi alipo, ila ikawa ni swali gumu sana Kwakwe kuweza kufahamu alipo, kwani chumba hicho kimetawaliwa na mitambo mingi ya kushangza.

Kitanda alicho lalia pembeni yake kuna bomba lililo ning'inizwa dripu ya maji iliyo peleka mrija wake moja kwa moja hadi kwenye mkono wake wa kulia na kisindano kidogo kilicho weza kuunganishwa na mrja huo, kimeingia moja kwa moja kwenye mshipa wake wa damu.

"Hapa ni wapi?"
Alizungunza huku akijaribu kujikaza kunyanyuka, mguh wake ulio fungwa bandeji zilizo badikika rangi kutokana na dawa akiyo pakwa, ukazidi kumuuma.

Akiwa katika kutazama tazama mlango wa chumba hicho kikubwa kinacho onekana kwamba kipo juu ya gorofa kubwa, ukafunguliwa. Akaingia mwanaume aliye valia koti jeupe pamoja na miwani kubwa kiasi. Katika kumtazama kwa haraka haraka ni lazima utagundua kwamba mtu huyo ni daktari.
"Karibu tena duniani Mr Eddy Godwin"
Mtu huyo mwenye asili ya kizungu izungumza kiswahili sahihi kilicho mshangaza hata Eddy mwenyewe.

"Wewe ni nani?"
Lilikuwa ni swali la kwanza la Eddy huku akimkazia macho daktari huyo aliye zidi kupiga hatua kumfwata katika kitanda alicho lala.
"Kuna hofu ya kuhofia, mimi ni rafiki yako wa karibu. Naitwa dokta William"
Alizungumza huku akigeuza geuza dripu linalo endelea kushusha maji kwenye miishipa ya Eddy.

"Unajisikiaje?"
"Nina maumivu kwenye mguu. Kwanza hapa ni wapi?"
"Hapa upo Mosscow Russia"
"Nilifikaje hapa?"
Eddy aliiza huku akizidi kumkazia macho daktari huyo kwani jibu lake tayari lilianza kumpa wasiwasi mkubwa.
"Nilikutoa Tanzania siju chache za nyuma. Niweza kukufwatilia wewe kwa ukaribu mkubwa hadi nikafanikiwa kukupata"

"Ulinijuaje mimi?"
"Nilikujua kupitia mama yako, alikuwa ni rafiki yangu wa karibu sana. Kiufupi mama yako alikuwa ni mwema sana kipindi nilipo kuwa nikiifanya kazi ya kuwafundisha madktari wa jeshi nchini Tanzania.
"Usiwe na shaka kwani Tanzania ni moja ya nchi niliyo ipenda sana na ni nchi ambayo viongozi wake baadhi ni wakatili sana wakiongozwa na raisi Praygod"

Eddy akastuka kusikia jina jilo, katika kumchunguza chunguza dokta William kwa haraka haraka akatambua kwamba ni mtu ambaye hakuwa na nia mbaya sana kwake japo hakuhitaji kuliamini hilo kwa asilimia mia moja.
"Nil stori ndefu sana mimi na Tanzania pamoja na viongozi wake na sasa nipo katika mpango wa kuhakikisha kwamba nina lipa kisasi kwa nchi hiyo."

"Kwa nini unahitaji kulipa kisasi?"
Dokta William akaivua miwani yake taratibu, kwa mbali machozi yakawa yanamlenga lenga, hakuhitaji kuzungumza kitu cha aina yoyote. Akaondoka na kusimama kwenye moja ya mashine inayo ongozwa na kompyuta aina ya Laptop. Akaanza kuiminya minya batani zake kwa mwendo wa kasi akionekana kuseti baadhi ya vitu katika mtambo huo. Kila alivyo zidi kuminya batani za kumpyuta hiyo asira dhidi ya Tanzania hususani raisi Praygod zikazidi kumpanda mara dufu.
***

Kwa mwendo wa boti waliyo kuwa nayo, haikuwasaidia sana kuweza kupasua mawimba makubwa ambayo yanaendelea kuikumba bahari ya hindi mara mwa mara. Upepe mkali na wenye nguvu wa kuyumbisha hata meli kubwa ulizidi kuirusha boti hiyo waliyo panda Shamsa na Briton kutoka upande mmoja kwenda mwengine.

Halo hiyo kikaifanya boti hiyo kuzima gafla, hofu ya kufa ndani ya maji ikaanza kumtawala Shamsa ambaye kwa Mara kadhaa alionekana kumkumbatia Briton huku akilia sana. Alihisi hakuwa na bahati ya kuishi jwani familia yake aliyo kuwa akiitegemea tayari ilisha fariki kuanzia Eddy hadi mtoto wake Junio.

"Bray tunakufa mpenzi wangu"
"No hatuwezi kufa, tusonge Mbele"
Briton alizungumza huku akiendelea kujitahidi kuhakikisha kwamba boti huyo inasonga Mbele. Bahari ikazidi kuchafuka, hats akari ambao walikuwa doria katika maji waka waliamriwa kughairisha msako huyo kwank hali ilitisha sana. Mvua taratibu ikaanza kunyesha jambo lililio zidi kuwachanganya Briton na Shamsa. Radi zikaanza kutawala kila kona. Gafla boti yao ikabenuliwa na kuzamishwa ndani ya maji, kila mmoja akaangukia upande wake. Hali ikazidi kuwa mbaya kwani radio, mawimbi Na upepeo vikazidi kuongezeka kadri ya muda ulivyo zidi kwenda ndivyo ikawa afadhali ya dakika moja nyuma.

Kila mmoja alijikuta akiwa katika upande wake, baridi kali ikazidi kuunynyasa mwili wa Shamsa, maumivu makali ya tumbo yakarejea gafla mwilini mwa Shamsa na kumfanya aanze kuishi wa nguvu, dakika kadhaa mbeleni akapoteza fahamu.
***
Hali ya usalama ikazidi kuimarishwa maeneo mbali mbaali ndanj na nje ya jiji la Dar es Salaam. Wanaanchi kupitia katika vyombo vya habari. Video, redio na magazetini raisi Praygod akatangaza hali ya usalama katika maeneo yote yanchi, akiendelea kuwahakikishia kwamba hakuto kuwa na jambo lolote bays litakalo weza kujitokeza. Wanaanchi pamoja na wafanya biashara wakarudi katika maeneo yao ya kazi.

Kitu kilicho zidi kimchanganya raisi Praygod ni wapi alipo mke wake kipenzi Rahab. Msako wa kuhakikisha kwamba mke wa raisi anapatikana ukazidi kuendelea.

Kwa siku ya pili mfululizo hapakuwa na askari akiye weza kulaza kichwa chake kwenye kitanda chake kama ilivyo siku za nyuma. Kuanzia wakuu wa majeshi hadi waliopo ngazi za chini, kazi ikawa ni kuhakikisha kwamva mke wa raisi anapatikana. Hapakuwa na mtu mwenye wazo la kujua kwamba mke wa raisi yupo kwenye pango ambalo lilitumiwa Na waasi wanawake ambao kwa sasa baadhi yao wapo katika mikono ya wamarekani.
"Madam tutaendelea kukaa humu hadi lini?"
"Hadi siku ambayo nitaamua mimi kutoka ndani ya handaki hili"

"Ika utakuwa unampa wasiwasi muheshimiwa raisi"."Nalitambua hilo ila sinto hitaji kurudi ikulu hadi nihakikishe ninampata Eddy, iwe kwa kuua au kufanya lolote ni kuhakikisha kwamba tunampata Eddy"
Priscar hakuwa na kitu chochote cha kuzungumza zaidi ya kuyasikiliza matakwa ya bosi wake.
"Ila kuna kitu kimoja nahitaji tuweze kukifanya kwa pamoja"
"Kitu gani madam"
"Nilazima kuhakikisha kwamba tunapata pesa tena pesa ya kutosha"

==


Advertisement
Punguzo la Bei 20% msimu huu wa Idd.Agiza saa hii ya Automatic, na lipa mzigo ukifika majiji yote TanzaniaAdvertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )