Sunday, April 2, 2017

SORRY MADAM -Sehemu ya 45 & 46 (Destination of my enemies)

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWAILIPOISHIA
ILIPOISHIA
Makachero wanao uongoza msafara huo wakashuka kwenye magari yao kila mmoja akiwa na bastola iliyo jaa risasi mkononi mwake. Wakatembea kwa tahafhari kubwa wakijaribu kuchunguza kila sehemu ya msitu huo kwa umakini wa hali ya juu. Umakini wao ulizidi kuongezeka kwani wana kiongozi wao mkubwa wa nchi. Wakafika hadi eneo la handaki. Makachero wawili wakaingia ndani ya handaki hilo. Gafla milio mingi ya risasi ikasikika ndani ya handaki hilo jambo lililo wachanganya raisi na watu wake walio baki nje ya handaki.

ENDELEA
   Milio hiyo ya risasi ikawafanya makachero wengine kumzunguka raisi Praygod Makuya kuzuia hata kama kuna tatizo baya litatokea waweze kumlinda. Ikawalazimu makachero wawili kuingia katika handaki bastola zao zikiwa mikononi mwao. Cha kushangaza wakawakuta wezao wakiwa wamesimaa huku wanatetemeka mithili ya watu walio mwagiwa maji ya baridi  na kusimamishwa kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro.

Wakajaribu kuwauliza kwa ishara ni kitu gani kimepelekea hadi wakawa wanafyatua risasi ovyo ovyo. Ila hakuna aliye weza kutoa jibu kati yao zaidi ya wao kuendelea kutetemeka.  Ikawalazimu wezao hao wawili kuanza kutembea taratibu ndani ya handaki hilo kuchunguza ni nini ambacho kimetokea.

Wakaingia kwenye moja ya chumba ambapo cha kwanza kukutana nacho chini ni damu nyingi za mwanadamu. Katika kupitisha pitisha macho yao huku na huku. Wakamkuta mke wa raisi akiwa amelala juu ya kitanda huku damu nyingi zikiwa zinamwagika mwilini mwake, akikaribia kuiaga dunia.

 ***
 Kitu kisicho onekana kikazidi kuwateketeza makachero walio mshambulia Priscar hadi wote wakafa.
Katika hali ya kumshangaza Priscar akajikuta akivutwa nje ya gari na kulazwa pembeni pasipo kumuona mtu anaye mfanyia mambo yote hayo. Jeraha la risasi iliyo mpiga ndani ya dakika moja likawa limekauka na mwili wake ukarudi katika hali yake ya kawaida.
“Wewe ni nani unaye nifanyia haya yote”
Ilimbidi Priscar kuuliza kwani hisia za kusnikwa na mtu huyo asiye oenekana kwenye mwili wake mara kadhaa, anazihisi ila tatizo ni mboni zake za macho haziwezi kumuona mtu huyo.

Hakuna ambacho aliweza kuambulia kujibiwa. Gari lake ambalo limeingia kwa nyuma ndani ya mtaro akashangaa likisitolewa taratibu na kusimamishwa barabarani. Kisha akajikuta akishikwa mkono wa kulia akikokotwa hadi kwenye mlango wa kuingilia ndani ya gari hilo. Mlango ukafunguliwa bila hata ya kupenda akajikuta akinyanyuliwa na kuingizwa kwenye gari na kukalishwa kwenye siti ya dereva.

Akafungwa mkanda, gari ikawashwa na mikono yake ikashikishwa kwenye mskani wa gari hiyo na mlango ukafungwa. Ikiashiria aondoke katika eneo hilo haraka iwezekanavyo kwani kuna gari baadhi za polisi zinakuja kuwapa nguvu makachero wanao pambana na mtu aliye hitaji kuuvamia msafara wa raisi.

 ***
Dokta akamuachia simu Shamsa kisha yeye akazidi kusonga mbele. Kulifwata gari lililo kosa kosa kuwagonga.  Shamsa kabla hajafika hatua nyingi simu hiyo ikaita kuangalia vizuri akakuta ni jina la baba yake, hakuona haja ya kuelekea anapo kwenda dokta wake. Akaipokea na kuiweka sikioni mwake.

“Baba habari”
“Ohoo Salama binti yangu, mumefika salama”
“Ndio baba hapa tumefika hospitalini”
“Mbona unazungumza kwa furaha sana?”
“Hpana baba kidogo nimebadilisha mazingira, kidogo ninafurahi sana”
Shamsa akiendelea kuzungumza na simu tayari dokta wale alisha fika kwenye  gari na kukutana na binti anaye mfahamu akitokea ndani ya gari hilo huku akimwagikwa na machozi.
“Sa Yoo unatatizo gani?”
Daktari alimuuliza huku  hasira yake ikiwa imebubujika kifuani mwake mithili ya barafu la maji liwekwapo juani
“Bibi yangu hali yake ni mbaya”

Dokta baada ya kusikia hiyo na kutokana anamfahamu vizuri binti huyo pamoja na bibi yake ambaye pia alisha wahi kumuhudumia katika maswala ya saikolojia, hakuwa na budi zaidi ya kuondoka na Sa Yoo wakielekea ndani. Wakaungana na Shamsa kuingia ndani ya hospoitali hiyo pasipo Eddy kumjua binti wa tatu anaye ingia na kina Sa Yoo ni nani, kwani binti huyo ameziachia nywele zake ndefu kwa nyuma nakuizuia sura yake kuweza kuonekana vizuri kwa mbele

Kutokana na uhalifu alio ufanya Eddy, ikamuwia ugumu kushuka ndani ya gari kuhofia kuingia mikononi mwa polisi, moja ni lazima astakiwe kwa kusa la kuwapiga polisi, mbili ni lazima atakabidhiwa katika ubalozi wa Tanzania aweze kurudishwa Tanzania, jambo ambalo hakuhitaji kuweza kulisikia kwa wakati huo.
Sa Yoo na daktari wakakimbilia kwenye  chumba cha wagonjwa mahututi huku wakimuacha Shamsa akiwa amekaa sehemu maalumu ya mapokezi akimsubiria mwenyeji wake afike. Shamsa akaitumia nafasi hiyo kuweza kumfikiria ni wapi ambapo anaweza kumpata Eddy.

Mwanaume anaye muheshimu kama baba yake, wazo la kurudi kwenye familia ya magaidi wa Al-Shabab likaanza kumpotea taratibu kichwani mwake, akaanza kufikiria kuungana tena na Eddy ambaye aliamini kwamba amekufa na hilo ndio jambo ambalo lilimfanya akubali kurudi katika familia ya Al-Shabab watu walio muulia wazazi wake baba na mama akiwa mdogo kisha akachukuliwa mateka na kuwa miongoni mwa askari wakikosi  hicho akiwa mdogo sana.
“Nilazima niwaue Al-Shabab wote”
Shamsa alizungumza huku picha ya askari wa kikosi hicho ikiwajia jia kichwani mwake. Hasira dhidi ya kikosi hicho ikazidi kumpanda moyoni mwake hadi mwili mzima ukaanza kumtetemeka.

Kwa kupitia kioo cha pembeni cha gari alilomo Eddy, akaona gari mbili za polisi zikija katia maeneo ya maegesho ya hospitalini hapo. Wasiwasi mwingi ukazidi kumpanda, akataka kushuka na kukimbia akaoona itakuwa ni hatari sana kwake na itakuwa ni rahisi kwa yeye kuweza kukamatwa na askari hao. Gari hizo zikazidi kulisogelea gari ambalo Eddy yupo, kwa haraka ikamlazimu kuweza kuinama ndani gari hilo ili asiweze kuonekana.
Gari hizo za polisi zikasimama karibu kabisa na gari alilopo. Wakashuka askari wanne walio valia nguo nyeusi huku viunoni mwao wakiwa wamening’iniza pingu pamoja na kuchomeka bastola zao zilizomo kwenye vifuko maalumu vya kuchomekea bastola.

   Askari hao wakatizama tizama kila sehemu ya maegesho ya magari hayo wakionekana kwamba kuna gari wanaitafuta, mmoja wao akaanza kupiga hatua za kulifwata gari hilo taratibu huku akijaribu kutazama namba ya usajili ya gari hilo kwani ni gari lililo mbebea muhalifu anayetafutwa ndani ya Japan nzima.
                                                                                              ***
  Miliyo ya risasi ilipo kata ndani ya handaki makachero wote walio nje ya handaki wakiongozwa na raisi Praygod wakaingia ndani huku wakionekana kuwa na shauku kubwa ya kujua ni kitu gani kinacho endelea ndani ya handaki. Wakawakuta makachero wa kwanza wakiwa hai huku wamesimama, hata kabla hawajawauliza wakawaona makachero wengine  wakitoka ndani ya chumba kimoja huku wakiwa wamembeba Rahab anaye endelea kuvujwa na damu nyingi.
Ikabaki nusu Raisi Praygod kuchanganyikiwa baada ya kumuona Rahab akiwa katika hali hiyo.

“Ah…aaa aahme faafaanyaa nini mke wangu”
Raisi Praygod aliuliza huku mwili ukimtetemeka, makachero walio tangulia kuingia ndani ya handaki hilo wakakosa jibu la kuzungumza na fika wanatambu kwamba wao ndio wameusika katika kumpiga risasi Rahab baada ya Rahab kuanza kufanya jaribio la kuwashambulia makachero hao ila akashindwa na kujikuta akipigwa risasi kadhaa zilizo mfanya kuingia ndani ya chumba huku hali yake ikiwa mbaya sana.
Kutokana hapakuwa na jibu kwa makachero hao, raisi Praygod akatoa amri ya mke wake awaishwe mara moja kwenye gari wampeleke hospitali.

Safari ya kurudi jijini Dar es Salaam ikaanza huku gari hizo zikiendeshwa kwa mwendo kasi. Ndani ya dakika arobaini na tano wakawa wameingia ndani  ya hospitali ya taifa muhimbili huku hali ya raabu kizidi kuwa mbaya kila jinsi dakika zilivyo zidi kwenda.
Madaktari wakaanza kazi ya kumuhudumia mke wa raisi, raisi Praygod akashindwa kuyazuai machozi yake.kumwagika. Hakujali kama ni kiongozi wa nchi alicho kihitaji kwa wakati huo ni kusikia mke wake anaendelea vizuri.

Madaktari ndani ya chumba cha upasuaji wakafanikiwa kutoa risasi zote sita zilizo ingia ndani ya mwili wa Rahab.
“Dokta…….”
Nesi mmoja alimuita daktari kiongozi wa opereshini hiyo, macho yao wote yakatua kwenye mwili wa Rahab, hapakuwa na mtu aliye weza kuamini kitu walicho kiona, woga kati yao ukazidi kutawala madaktari wote sita pamoja na nesi mmoja waliomo ndani ya chumba hicho.  Vidonda vilivyo kuwa kwenye mwili wa Rahab vilijiziba na kurudi katika hali ya kawaida.

Kitendo cha Rahab kuyafumbua macho yake yaliyo mekundu mithili ya damu kikawafanya madaktari wpte waliomo ndani ya chumba kuanza kukimbilia mlangoni, kila mmoja akijaribu kuyaokoa maisha yake. Hadi wanafika mlangoni tayari Rahab alisha simama wima na kuchomo sindano zote za madripu zilizo kuwa zimechomwa mwilini mwake. Kila walipo jaribu kuufungua mlango haukufunguka na taa zilizomo ndani ya chumba hicho zikaanza kufifia na kigiza cha mbali kikaanza kutawala ndani ya chumba.

***
   Njia nzima Priscar akajikuta akijiuliza maswali ni kitui gani kilicho weza kutoke katika muda mchache uliopita.

“Au naota?”
Swali hilo alilipatia jibu akilini mwake kwamba kila kitu kinacho tokea kwa wakati huo si ndoto bali ni hali alisi inayo jitokeza.
“Madam”
Priscar aliwaza sehemu alipo mucha Rahab, ikamlazimu kuongeza mwendo kasi wa gari lake kuelekea nje ya jiji la Dar es Salaam. Hadi anafika katika maeneo ya hamdaki ikamlazimu kusimaisha gari lake mbali kidogo na sehemu na lilipo hamdaki, akashuka na kuanza kukimbia kuelekea sehemu ya handaki, kabla hajalifikia akasikia milio kadhaa ya risasi ikirindima ndani ya handaki hilo.

Alipo chunguza vizuri akaziona gari za ikulu zikiwa zimesimama nje ya handaki hilo, huku Raisi Praygod akiwa wamezungukwa na walinzi wake. Baada ya milio ya risasi kunyamaza akawashuhudia walinzi hao wakiongozana na raisi wakiingi ndani ya handaki hilo. Baada ya dakika tano mbeleni akawaona wakitoka wakiwa wamembeba Rahab akionekana akiwa katika hali mbaya.
Priscar akataka kujitokeza ili  akasaidiane nao ila akaona itakuwa ni hatari kwake, akaendelea kujibanza kwenye mti huo hadi wakaondoka kwa kasi katika eneo hilo.
Kudhibitisha ni kitu gani kilicho weza kutokea ndani ya handaki hilo, kwa haraka akakimbia nje ya handaki hilo kutazama ni nini kilicho tokea.

Hakuamini macho yake baada ya kukuta damu nyingi zikiwa chini ya sakafu zikitokea katika chumba alipo ingia akazidikuta zikiwa nyingi jkuu ya kitanda. Jasho likaanza kumtirirka akifikiria ni kitu gani ambacho kimetokea bosi wake.
 
Kwa haraka akatoka ndani ya handaki na kurudi alipo liacha gari lake. Akaingia ndani ya gari na kuanza kuelekea Dar es Salaam akiamini kwamba ni lazima Rahab atakuwa amepelekwa kwenye moja ya hospitali iliyopo jijini Dar es Salaam.

==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )