Friday, May 12, 2017

Kitanda cha Sokwe Mtu.....Sehemu ya Kwanza

Na. DOKTA MUNGWA KABILI. 0744000473
HABARI ZENU ?  NINAPENDA  KUWATAARIFU  KUWA  NAKALA  ZA  KITABU CHENU PENDWA  “KITANDA  CHA  SOKWE  MTU “ ZIMECHUKULIWA  ZOTE  TAYARI.  ASILIMIA  TISINI  YA  NAKALA  ZA  KITABU  HIKI  ZILISHACHUKULIWA TAYARI HATA  KABLA  YA  KITABU  HAKIJATOKA  MTAMBONI, NA  ASILIA  KUMI  YA  NAKALA  ZILIZO  BAKI  NDIO  ZOTE  ZIMEMALIZIKA  SIKU  YA  JANA.
BADO  TUNAPOKEA  SIMU  NYINGI  SANA  KUTOKA  KWA  WATU MBALIMBALI  WAKIULIZIA  KITABU  HIKI, TUNAPATA  SHIDA  KUMUELEZEA  KILA  ANAEPIGA  SIMU  KUULIZIA  KITABU NA  NDIO  MAANA  TUMEONA  TUWEKE  TAARIFA  HII  HAPA BLOGUNI.


HATA  HIVYO  KWA  KUWA  WATU  WENGI  BADO  WANAHITAJI  KUSOMA  KITABU  HIKI, NIMEAMUA  KUTOA  OFA  MAALUMU  KWA  KUCHAPISHA  KITABU  HIKI  HAPA  BLOGUNI, AMBAPO  UTAWEZA  KUKISOMA  BURE  KABISA KUANIZA  TOLEO  LA  KWANZA  HADI  LA  MWISHO. UNACGO TAKIWA  KUFANYA  NI  KUTEMBELEA  BLOGUNI  HAPA  KILA  SIKU. SIKU  YA  LEO  TUTAANZA  NA  SEHEMU  YA  KWANZA  YA  KITABU  HIKI.

(  WAKATI  HUO HUO, JIANDAE   KUSOMA  SIMULIZI  KALI  NA  LA  KUSISIMUA  LIITWALO  “  MKATASANDA “ : HILI  NI  SIMULIZI  LA  UKWELI  LA  MAISHA  YA  MTU  AITWAE  “ VIHELAHELA “  AMBAE  UKOO  WAKE  WOTE  ULIMALIZWA   KWA  KUTUMIA   UCHAWI  WA  NDEGE  AJULIKANAE  KAMA “MKATASANDA “.  NI  SIMULIZI  LA  KUSISIMUA  SANA  AMBALO  UTALIPATA  KUPITIA  : WWW.MUNGWAKABILI.BLOGSPOT.COM . NDANI  YA  SIMULIZI  HILO  LITAKALO  TOKA  HIVI  KARIBUNI  UTAPATA  KUFAHAMU  KUHUSU  MAMBO  MBALIMBALI  MAZITO  YA  KICHAWI  PAMOJA  NA  JINSI  YA  KUJIKINGA  NA  KUJIEPUSHA  NAYO.   SIMULIZI  HILI  LITAANZA  KUTOKA  MARA  TU  BAADA  YA  KUMALIZA  KUCHAPISHA  SIMULIZI  LA  “  KITANDA  CHA  SOKWE  MTU “

                            KITANDA  CHA  SOKWE  MTU  SEHEMU  YA  KWANZA

Kabla  ya  sehemu  ya  kwanza  kuna  sehemu  ya  utangulizi  wa  simulizi  hili. Sehemu  ya  utangulizi   wa  simulizi  hili  inaelezea  historia  ya  maisha  ya  Lugwisha  kwa  ufupi, familia  aliyo  toka, jinsi  alivyo  toka  kwao  Tabora  na  kwenda  dar  Es  Salaam  kutafuta  maisha, changamoto  alizo  zipata  hadi  kupata  mafanikio  makubwa  katika  maisha  yake.  Katika  mfululizo wa  machapisho  haya, nitaelezea  matukio  ya  kuanzia  siku  ambayo Lugwisha  alifikishwa  kilingeni  kwangu.

Nakumbuka  ilikuwa  mwaka  2013 . Siku hiyo  nilipokea  simu kutoka  kwa  kijana  aitwae  Willy . Kijana  huyu  alinieleza  kwa  ufupi  kuhusu  rafiki  yake  aitwae  Lugwisha.

Kwa  ufupi  aliniambia  Lugwisha  alikuwa  mfanyabiashara  mwenye  mafanikio  makubwa  sana , lakini  ghafla  amefilisika, kiasi  hata  hela  ya  kula  chakula  inampiga  chenga.

Tulikubaliana na Willy   kuwa, mchana  wa  kesho  yake, angefika  kilingeni  kwangu  Bagamoyo, akiwa  ameongozana na rafiki  yake  ambae  ni  Lugwisha  kwa  ajili  ya  kupata  msaada  wangu

Willy  ni  kijana  aliye  tambulishwa  kwangu  na  dada  ake  ambae  ninamfahamu  kwa  jina  la  Stella.

Mwaka  2011  Stella  aliletwa  kwangu  na  rafiki yake  ambae  alikuwa anafanya  biashara  ya chakula  kwenye  machimbo ya  madini ya  Ruby  yaliyopo  Mtipweshi  huko  nchini  Msumbiji.
 Stella  alitaka  nimtengenezee  dawa  ili  atakapo  fika  huko  Mtipweshi  afanikiwe  katika  biashara  yake.

Miezi  sita  baadae  Stella  akawa  ni  mwanamke  mwenye  mafanikio  makubwa  kupitia biashara  yake  ya  chakula  ambayo  aliifanya  kwenye  machimbo  ya  madini  ya  ruby  huko  nchini  Msumbiji.

Akiwa  nchini  Msumbiji  Stella  alijionea  mwenyewe  jinsi  vijana  wa  kitanzania  wanavyo  pata  mafanikio  ya  kutisha  kupitia  kazi  ya  uchimbaji  na  uuzaji  wa  madini  wa  ruby  huko  Mtipweshi.

Aliamua  kumvuta  kaka  ake  Willy  ili  na  yeye  akajaribu  bahati  yake .
Kabla  ya  kuondoka  nae  Msumbiji, Stella  alimleta  Willy  hai  kilingeni  kwangu nimtengeneze  ili  atakapo  kuwa  machimboni  huko  nchini  Msumbiji  aweze  kupata  mafanikio  makubwa  na  hivyo  kubadilisha  maisha  ya  familia  yao.

Naikumbuka  vizuri  sana  siku  ambayo  Willy  aliletwa  kilingeni  kwangu.  Baada  ya  kusikiliza  kwa  makini  shida  ya  Willy, nilianza  mara  moja  utaratibu  wa  kutengeneza  tambiko  maalumu  kwa  Willy  ili  akafanye  shughuli  ya  uchimbaji  na  uuzaji  wa  madini  akiwa  na  baraka  zote  za  mabibi  na  mababu.

Katika  matambiko  ya  uchimbaji  wa  madini  huwa  kuna  njia  kuu mbili ;

 Njia  ya  kwanza  unafanya  tambiko   la  kumtengeneza  mchimbaji  na  njia  ya  pili  unafanya  tambiko  la  kutengeneza  shimo.

Tambiko  kwa  mchimbaji  hufanyika  ila kumfanyia  mchimbaji  huyo  wepesi  wa  kupata  madini  kila   anapo  ingia  shimoni  kuchimbailhali  tambiko  la  kutengeneza  shimo  hufanyika  kwa  lengo  la  kulifanya  shimo  litapishe  madini   ya  kutosha.

Tambiko  la  kumtengeneza  mchimbaji  madini  huwa  lina  hatua  kuu  ishirini  na  moja.  Hatua  ya  kwanza  huwa  ni  kupima  mwili  wa  mchimbaji, ili  kuona  kama  una  “ uchafu  “  wowote.

Hatua  ya  pili  huwa  ni  kumsafisha   mwili  mchimbaji  husika . Katika kusafisha mwili huwa yapo  matambiko  ya  aina  mbalimbali .

Aina  ya  tambiko  hutegemeana  na  aina  pamoja na   kiwango  cha  uchafu  wa mwili  wa  mhusika.

Hatua  inayo  fuata  baada  ya  kuusafisha  mwili  wa  mchimbaji, ni  kuutengenezea  kinga  ya  mwili.

Kinga  dhidi  ya  majini, masheitwani,  mizimu  michafu  inayopatikana  katika  maeneo  ya  migodi.

Kinga  dhidi  ya  watu  mbalimbali  wenye  husda.  Mtu  huyu  atakuwa  anaenda  kufanikiwa  na  kuwa  tajiri  mkubwa  jambo  ambalo  litanyanyua  uadui  kutoka  kwa  watu  mbalimbali  ambao  hawatapendezwa  na  mafanikio  ya   mchimbaji  huyu.  Wakati mwingine  kama  si  wakati  wote, ndugu, jamaa  na  marafiki  wabaya  wakisikia  Fulani anakwenda  kuchimba  madini  wanaweza  kwenda  kwa  wachawi  kukutengenezea  uchawi  wa  kukuua, ili ionekane  kama  vile  umekufa  kwenye  harakati  za  uchimbaji  madini labda  kwa  kufunikwa  na  kifusi  nakadhalika.

 Hivyo  basi  mchimbaji  huyu  hufanyiwa   tambiko  maalumu  la  kuukinga  mwili  wake  dhidi  ya  maadui na  watu  wabaya  wa  aina  zote.

Baada  ya  hatua  hii  ya  tatu  huwa  zinafuata  hatua  nyingine  kumi  na  saba.

Na  baada  ya  hatua  hizi  kumi  na  saba , zoezi  la  kumtengeneza  mchimbaji  madini  humalizika  kwa  hatua  ya  mwisho  ambayo  huwa  kama  ifuatavyo.

Katika   hatua  hii  huwa  inatafutwa  dawa  inaitwa  Ambari  nyeupe. Ambari  hii  nyeupe  ni  lazima  iwe  ile  orijino.

Zipo  njia  za  kijadi  za  kujua  kama  ambari  uliyo nayo  ni  orijino  ama  sio  orijino.

Hii  ambari nyeupe  ina  uhusiano  mkubwa  sana  na  jinni  wa  baharini  ajulikanae  kama  Nguva  au  Samaki  Mtu  pamoja  na  madini  yanayo  patikana  baharini  ambayo  hujulikana  kama  ruby.

Vitu  vyote  hivi  viwili  yani  ambari nyeupe  pamoja  na  madini  ya  ruby  vina  uhusiano  mkubwa sana  na  huyu   Samaki  mtu.

Ambari  ina  matumizi  mengi  sana  katika  uganga, uchawi  na  tiba  za  asili  au  tiba  mbadala  kwa  jina  lingine.
Katika  tiba  mbadala, ambari  ina  matumizi  mengi  sana  lakini  kubwa  kuliko  yote , ambari inapochanganywa  na  baadhi  ya  dawa  za  porini, hutumika  katika  tiba  ya  kurefusha na  kunenepesha  maumbile  ya  kiume  pamoja  na  kuongeza  nguvu  za  kiume.

Katika  masuala  ya  uganga, ambari   nyeupe  huchanganywa  na  dawa  mbalimbali  na  kutumika  kumchanja  mtu  kwa  ajili ya  kumpa  kinga  ya  mwili  dhidi  ya  wachawi  na  majini  wabaya  pamoja  na  kufukuza  majini  wabaya.

Sifa  kubwa  ya  ambari  ni kwamba, huvuta  maruhani  wazuri  na  majini  wote  wa  heri. Huvuta  maruhani  wakali wa  baharini  wenye  nguvu  sana.  Popote  pale  ambari inapokuwepo  basi  na  maruhani  hawa  huwepo  pia.  Sifa  kuu  ya  hawa  maruhani  wa  baharini  huwa  hawakai  pamoja  na  uchawi  wa  aina  yoyote  ile  wala  majini au masheitwani  wabaya  wa  aina  yoyote  ile.

Hivyo basi  mtu  anapo  chanjiwa  ambari   iliyo  tayarishwa kwa kufuata  taratibu  zake   pamoja  na  vizimba   vyake hupata  ulinzi  mkubwa  sana  wa mwili  wala  hakuna  jinni , pepo, sheitwani  au mchawi  wa  aina  yoyote  ile  anaweza  kumdhuru  kwa  kutumia  uchawi  wa  aina  yoyote  ile.

Lazima  mtu  achanjiwe. Sababu  kubwa  ya  kuchanjiwa ni  kuwaunganisha  maruhani  wa  kwenye  ambari  na  roho  ya  mtu  husika.

Kama  ulikuwa  haufahamu  ni  kwamba, roho  ya  mtu  ipo kwenye  damu  ama  kwa  lugha  nyepesi, uhai  wa  mtu  ni  damu. Na  katika  ulimwengu  wa  kiganga, kuna  kanuni  moja  muhimu  sana ambayo inasema   chochote  kinacho  unganishwa  kwenye  damu  ya  mtu  au  mnyama  kiwe  kizuri  au  kibaya,  basi  huwa  sehemu  ya  damu  hiyo.
Hii ndio  sababu  kubwa  kwanini  watu  huchanjiwa  dawa, iwe kwa  nia  mbaya  au  kwa  nia  nzuri.

Kuwaunganisha  na  kuwafungamanisha  na  maruhani  wazuri  au  majini na  masheitwani  wachafu.

Turudi  kwenye  maelezo yetu  ya  awali. Ukisha  ichukua  hiyo  ambari nyeupe  orijino. Unaiweka  kwenye  kisosi  au chombo  chochote   cheupe  kisicho  na  doa  wala  alama  yoyote  ile, halafu  unasaga  pamoja  na dawa  inaitwa  Nyota  au  Habbat  Nuksi, dawa  hii  ina  umbo  lenye  kufanana  na  nyota  na  huwa  haina  alama  yoyote .

Ni dawa  yenye  matumizi  mengi  sana  katika  ulimwengu  wa  kiganga.
Ukisha  weka  hii  Habbat  Nuksi, unachanganya  na  kizibo kimoja cha  mafuta  ya  usiku. Haya  mafuta  ya  usiku  ni  mafuta  yaliyo  miongoni  mwa  mafuta  makubwa  kabisa katika  ulimwengu  wa  waganga .

Mafuta  haya  ni  mafuta  yenye  nguvu kubwa   sana.  Ni  mafuta  makubwa  yenye  kubeba  majini  na  maruhani  wazito  wazito.  Ipo  namna  ya  jadi  ya  kuyatambua  mafuta  ya usiku.  Ni mafuta  yenye  gharama  kubwa   na  yana  matumizi  mengi  sana.   

Mfano  katika  biashara   ndogondogo , kama  mtu  anataka  kutajirika  kwa  kupitia  biashara  ndogondogo  hususani  ya  kuuza  vitu  vya  kula  kama  vile  vitumbua, maandazi, mamalishe, kuuza  vitu vya  watoto  mashuleni   nakadhalika  basi  ni  lazima  atumie  mafuta  haya.

Ni mafuta yenye  nguvu  za  ajabu  sana. Nikisema  nielezee  matumizi yake  yote  mahali   hapa, basi  nadhani nitalazimika  kuandika kitabu  chenye  kurasa  nyingi  sana.

Sasa  basi  ukisha changanya  mafuta   haya  ya  usiku  kwenye  kisosi  au chombo  chochote kisicho na  doa  hata  moja  ambacho ndani yake  vimesagwa  pamoja  ambari  nyeupe  orijino  pamoja  na  Nyota  au  Habbat  Nuksi,  unaongeza  kijiko  kikubwa  chenye   dawa  moja  hatari  sana  ya  porini.
Kwa  sababu  za  kimaadili  ya  kazi  yangu  ya  uganga, sitaweza  kuutaja mti  huo  hapa, isipokuwa  nitaweka  maelezo  kuuhusu  mti  huo.

Mti  huu  unapatikana porini, mti huo ukikomaa, urefu wake hauzidi wa mtoto wa miaka saba, una magamba kwa mbali na rangi yake ni nyeupe.

Mti huu ukikauka ukausaga unga wake huwa mweupe kama mti wenyewe.

Ukichukua unga wa mti huu halafu ukajipaka usoni unakuwa na uwezo wa kuwaona wachawi.

Ukijipaka unga wa mti huu usoni halafu ukatembea mtaani wakati wa mchana, unaweza kuona mambo yote yanayofanyika katika siri kubwa kama vile wachawi wakiwa wanawanga au wanafanya shughuli zao wakiwa uchi.

Dawa hii itakupa pia uwezo wa kuwaona misukule.

Vilevile mti huu una uwezo wa kukimbiza nyoka mfano ukiwa na kipande cha mti huu mfukoni halafu ukawa unatembea, kama mbele yako kuna nyoka atakimbia kabla hujafika.

Hata ukikaa mahali kama kuna nyoka hawezi kukaa hapo, atakimbia tu.
Ukisha kamilisha  zoezi  hili, unamchukua  huyo mchimbaji  madini  unamchanja  kwenye  pande  zote  saba  za  mwili, na kumpaka  dawa  kwa kutumia  sarafu, halafu  anachinjiwa  punda  pamoja  na  kondoo  ambao  vitu  vyao vitatumika  kutengeneza  azima  ambayo  atapewa mchimbaji  huyo.

Vitu  hivyo  ni  pamoja  na  wadudu  wanao  patikana  kichwani  mwa  kondoo, kwato zake, mkia wake, moyo  wa  punda, mkia, kwato nakadhalika.

Baada  ya  hapo  mtu  huyu  anakuwa  amekamilika  tayari  kwa  shughuli  ya  uchimbaji  wa  madini.

Mtu  aliyefanyiwa  dawa  hii  huwa  na  bahati  kubwa  sana  ya  kupata  madini  au  mawe  kila  anapoingia  kuchimba  shimo.

Mafuta  ya  usiku  pamoja  na  mti  nilio  uelezea  hapo  juu    humpa  uwezo  wa  kuona  mali  moja  kwa  moja  kwa  sababu  mafuta  hayo pamoja  na  mti  huo, pamoja  na kumsaidia  mhusika  katia  mambo mengine,  humpa  mtu  uwezo  wa kuona  vitu  visivyo onekana  ambavyo  vimefichwa kwa kutumia  uchawi  au  ambavyo  vimejificha  vyenyewe  kwa  kutumia  mazingara.

Dawa  hizo  husaidia  kufanya  majini wabaya , masheitwani  wabaya  pamoja  na  mizimu  wabaya  waliopo  katika  maeneo  ya  mgodi  huo wasiweze  kumuona  na  hivyo  kushindwa  kumfichia  mali.

Unajua  kawaida  ya  mali  za  migodini  huwa  ni  kuhamahama. Mali  hizi  haziami  zenyewe  bali  huamishwa  na  majini, masheitwani  na  mizimu  wanao  linda  mali hizo  ambao  hawataki zichukuliwe  na  mtu  yoyote  Yule.

Unaweza  kuchimba  upande  A, kumbe  mali  ipo  upande B. Ukavuka upande  B  ukaenda  upande  C, kumbe  mali  umeiacha  upande B. Hili ni  suala  la  kawaida  kabisa  machimboni.

Hivyo  basi  ili uweze  kuchukua  mali  ni  lazima  ufanye  moja  wapo kati  ya  mambo  makuu  mawili  yafuatayo;

Moja uwafunge  majini  na  mizimu  wa eneo  hilo, wasiwe  na  uwezo  wa  kukuzuia  kuona  na  kuchukua  mali au  pili  uingie  mkataba  na  majini au  mizimu  hao, kuwaomba  wakuruhusu  kuchukua  mali.

Tambiko  hili  linafanya  mambo  makuu  mawili, kwanza   linawafunga  mizimu  na  majini  walio  katika  eneo  la  mgodi  husika  na  kuwafanya  washindwe  kukuzuia  kuchukua  mali  na  pili  linakufungua  macho  ya  kuona  mali  ilipo pamoja  na  kuivuta  mali  mahali  ulipo.

Sio kwamba  utaoteshwa  mali  ipo  sehemu  fulani  nenda  kachimbe, lah  isipokuwa  utaongozwa, kila sehemu  utakayo  enda  kuchimba mali utakuwa  unapata  bahati  ya  kupata  mali.

Ndio  maana  ukienda  migodini,  yupo mtu  anaweza  kufika  mgodini  leo  na  baada  ya  wiki  moja  akapata  mali, na  kuwaacha  watu  ambao  wamekuwa  wakichimba  kila  siku  kwa  miaka  na  miaka  huku  wakiambulia  kupata  hela  ya  kula  tu  na  mwisho  wa  siku watu wanabakia  kujiuliza  huyu  mtu  si  amekuja  juzi tu.

Njia  ya  pili  ni  ya  kutengeneza  shimo. Hapa  kwenye  kutengeneza  shimo  ama  kulifanyia  tambiko  maalumu shimo  kwa  lengo  la  kulifanya  liteme  madini, kuna  hatua  kama  arobaini  za  kufuata.

Ili   uwe  na  uhakika  kwamba, shimo  lako  litatema  madini  ni  lazima, hatua  zote  arobaini  zifuatwe  kwa  kuzingatia  utaratibu uliowekwa.
Si rahisi  kuzielezea  hatua  zote  arobaini, kwa  sababu  maelezo  yake  ni  marefu  sana  na  yafaa  kutengeneza  kitabu chake  peke  yake. Hivyo  basi,  katika  kitabu  hiki  nitaelezea  kwa  ufupi, hatua  ya  mwisho.

Katika  hatua  hii  ya  mwisho, unachukua  ambari orijino ( kama  uliyo itumia  wakati  unamtengeneza  mchimbaji madini ), unachukua  Nyota  au  Habbat  Nuksi,  halafu  unachukua dawa  nyingine  inaitwa  Kishinda  wachawi. Hii  ni  dawa  hatari  sana,. Nchini  Tanzania  inapatikana  Kigoma  tu  na  kwa  ukanda  huu  wa  Afrika  Mashariki  na  Maziwa  makuu, mti huu  unapatikana  mkoani  Kigoma  nchini  Tanzania  na  Kongo  ya  Mashariki.

Mti  huu  una  matumizi  mengi  sana  katika masuala ya  uganga, baadhi  ya  matumizi  hayo ni  pamoja  na  kuua uchawi  wa aina  yoyote  ile  ambao  mtu  amelishwa  au  kutumiwa , kutafuta  mtu  aliepotea  nakadhalika.
Baada  ya  kuweka  kishinda  wachawi  unachanganya  dawa  nyingine  kutoka  kwenye  miti mingine ya  porini   ambayo   idadi  yake  inafika  sabini .

Katika  miti  hiyo, unakuwemo  mti  mmoja  wa  porini  ambao kazi  yake  kubwa  ni  kuvuta  uchawi  na  majini  wote  wa  wabaya. Katika  ulimwengu  wa  kiganga  mti  huu, huitwa  Kikusanya  majini.

Huu  ndio  mti  unaopendwa  na  majini  wabaya  kuliko  mti mwingine  wowote  ule. Majini  wote  wabaya  hukusanyika  katika  mti  huu.

Kama  mtu  anataka  kukusanya  majini  wabaya  kwenye  biashara  yako, basi  atakacho kifanya  anachukua  kipade  cha  mti  huu, na  kuuzika  kwenye  nyumba  yako  au  eneo  lako  la  biashara  au  anauchukua  anausaga  halafu  anakuja  kumwagia  vumbi  lake  kwenye  eneo  lako  la  biashara. Hutochukua  raundi  utafunga  biashara  yako  hiyo  utakimbia  mji  wako, kwa  sababu  majini  wote  wachafu  watakuja  kufanya  makazi  yao  katika  mji  wako  au  eneo  lako  la  biashara.  Na wanapokuja  kuweka  makazi  katika  eneo  lolote, huambatana  na  nukis, mikosi na  mabalaa  yao  yote  waliyo nayo, hivyo basi  endapo  mti huu au  unga  wa  mti  huu  utazikwa  katika  nyumba  yako  ya  kuishi  au eneo  lako  la  biashara,  mikosi, balaa   na  nuksi  zote  za  majini  hao  wabaya  zitakuandama katika  maisha  yako.

 Wakati  mwingine  wachawi  wanaweza  kunyweshwa  au  kukuchanjiw dawa  hiyo  kwa  lengo  la  kukutia  nuksi, balaa  na  mikosi.

Kama  kuna  sehemu  kuna  majini  wabaya. Ukichukua  kipande  cha  mti  huu  ukauzika  mita  chache  kutoka  eneo  lenye  majini  hao  wabaya  basi  majini  wote  wabaya  watahamia  katika  eneo  ambalo  umeuzika  mti  huo  na  hawata toka   katika  eneo mpaka  mti  huo utolewe  kwa  mahali  hapo  kwa  tambiko  maalumu.

Mti  yote  hii  inatengenezwa  hazima au hirizi  halafu inaenda  kuzikwa   mita  chache  toka  eneo  lililo  shimo  lako, kwa  taambiko  maalumu.
Litafanyika  tambiko  maalumu  la  kuwaita  mapepo, majini wabaya  na  mizimu  wabaya  waliopo  katika  eneo  hilo  la mgodi na  kuwafunga  kwenye  shimo ilimowekwa  hazima hiyo.

Hapa  unakuwa  umewafunga  majini wote  wabaya  wasikusumbue  kwenye  utafutaji mali. Majini  hawa  wanakuwa  wamekuachia  wazi  milango ya  kupata mali  kwa  sababu  unakuwa  umewafunga  kwenye  eneo  ambalo  wamekusanyika.

Ukishamaliza  kuwafunga  mizimu  na  majini wabaya  kwenye  shimo  hili  la  pembeni,  unachukua  dawa  za  porini  ambazo  idadi  yake  ni  arobaini.   Baadhi  ya  dawa  hizo  ni  pamoja  na  mwinula,mkasula, mdaula,Nyota, Ufuta ( Sio ufuta  sim sim hapana, kuna  dawa  ya  porini  inaitwa  ufuta  na  haina  uhusiano  wowote  na  ufuta  huu  unao ujua wewe ),mchekea, mfunuo,sakawachawi,karafuu maiti ya kidonge  ambayo  inasagwa  kupata  unga  wake, mwatya,mkola,mlama, mputika  mzima  na  mti mmoja  hatari  sana  ambao  unajulikana  kama  mpapatiko.

Huu  mpapatiko au mpapa  ni  mti  wenye  uchawi  mkubwa  sana.

Hapa  Tanzania  mpapatiko  orijino  unapatikana  katika  mikoa  ya    Tabora na  Tanga  wilaya  ya  Lushoto.  Mti  huu  ni  hatari  sana  katika  masuala  ya  mapenzi,mvuto wa  biashara, uongozi  nakadhalika.

 Katika  ulimwengu  wa  kiganga, mti  wa  mpapatiko  ni  toleo  la  mmea  la  mnyama  aitwae  Ngekewa. Unajua  katika  ulimwengu  wa  uganga  kila  mmea  huwa  una  mnyama, ndege au mdudu  ambae  ni  pacha  wake.

Sasa  basi huu  mmea  wa mpapatiko  ni  pacha  wa  mnayama  anaitwa  Ngekewa. Ukiukata  mti  wa  mpapatiko, baada  ya  dakika kumi  unakuwa  umefunikwa  na  siafu  na  sisimizi. Kwa  ufupi mti huu  una maruhani  wakali  sana  wa  mvuto. Kama  wewe  ni  mfanya  biashara  na  hauna  mti  huu, basi sina uhakika  na faida  unayo ipata  katika  biashara  yako.
Na  kama unataka  kuwavuta  watu  kuwafanya  wakupapatikie  kwenye  mapenzi, biashara, kazi  nakadhalika, mpapatiko  ndio  jibu  lako.

Dawa  zote  hizi arobaini  zinasagwa  halafu zinawekwa  kwenye  chungu  ambacho  kimewekwa  kwenye  mafiga, halafu unachukua  mti  wa jani  nuka  au  kivumbasi .

Mti  huu  wa  kivumbasi  una  matumizi  mengi  sana, kama  vile  kufukuza  mbu, kuogea  kwa ajili ya  kusafisha  mwili, kuchoma  ofisini, kilingeni  au  nyumbani kwa  ajili  ya  kufukuza  na  kudhibiti  majini  wabaya  nakadhalika.,

Mti  huu  wa  kivumbasi  unautengeneza  kama  ufagio, kisha  unakuwa  unachovya  kwenye  dawa na  kuchapa  kwenye  shimo  lako huku  unatamka  maneno  maalumu  ya  kubariki shimo  lako.

Hii dawa  unayo  chapa  kwenye  shimo  la  mgodi, unaweza  kutumia  kuchapa  hata  sehemu zingine  hususani  kama  inasumbuliwa  na  wachawi kama  vile dukani, baa, nyumbani nakadhalika.

Baada  ya  hapo, itafanyika  kafara  maalumu  ya  punda  na  kondoo.
Kazi  ya  kuchimba mgodi  baada  ya  tambiko  hili  inatakiwa  kuanza siku yoyote  ile  isipokuwa  Jumanne  au  Jumamosi.

Jambo  ambalo si  la  kusahau wala  kupuuzia  ni  kuhakikisha  huyu  mchimbaji  anakuwa  na  kinga  ya  mwili pamoja  na  mali  zake.

Hii  ni kwa  sababu  si  watu wote  wanao furahia  mafanikio  ya  mtu.

Watu pekee  wanao  taka  ufanikiwe  katika  dunia  hii  ni baba ako mama  ako  na  watoto  wako.

Hivyo  ni jambo  la  muhimu  sana  kuhakikisha  unakuwa  na  kinga  ya  mwili  wako.

Kwenye  kinga  ya  mwili  zipo  kinga  za  aina  nyingi  sana. Katika  kitabu  hiki  nitaelezea  aina  moja  wapo  ya  kinga  kati ya  kinga  hizo.
Kinga hii  kwanza  itawazuia  wachawi na  watu  wabaya  wasiweze  kukuona  katika  rada zao  za  kichawi.

Wachawi  huwa  hawawezi  kumroga  mtu  ambae  hawawezi  kumuona  kwenye  darubini  zao za  kichawi kwa  sababu  wanakuwa  hawajui  nguvu inayo  mfanya  asionekane.

Lakini  pili  mtu  yoyote  yule  atakae  jaribu  kukuroga  basi  ubaya  wake  utadunda  na  kumrudia   yeye  mwenyewe  ama  atakufa  kabisa. Kama  hautaki  mbaya  wako aliyekujaribu, uchawi  wake  udunde  na  kumrudia  yeye mwenyewe  na  kumuua,  basi  utakapo  kuwa  unafanyiwa  tambiko  hili  usishike  kisu, jambia  wala  panga.

 Ukishika  vitu  hivyo  basi  mtu yoyote  atakae  kufanyia  uchawi, utadunda  na  kumrudia  yeye  mwenyewe kama  alivyo ukusudia  kwako  na  mwisho wa  siku  na  atakufa  ila  kabla  ya  kufa  lazima  augue kupooza  kwa  muda  wa  kuanzia  miezi  sita  hadi mwaka mmoja.

 Lakini  kama  hautaki  afe  basi usishike  panga, kisu  wala  jambia. Uchawi  wake  utadunda  na  kuteleza  na kumrudia  mwenyewe.

Katika  tambiko  hili  huwa  inachukuliwa  ngozi  ya  kenge, gamba  la  nyoka  mkubwa  aliye jivua  mwenyewe, ngozi  ya mnyama  mmoja  wa  baharini au  uume  wake  .

Mnyama  huyu  wa  baharini   huwa  ana sifa  moja  kubwa  na  ya  kipekee  nayo  ni  kuwa  na   hamu  ya  kufanya  mapenzi muda  wote  na  hufanya  mapenzi na  kila  aina  ya  mnyama.

Mnyama huyu  yupo  wa  aina  mbili, kuna  mkubwa  na  mdogo  ( kwa  asili sio kwa  umri ), hapa  unamchukua  mdogo.

Wanyama  hawa  wanapatikana   kwa wingi  sana  ziwa  Tanganyika, na  Ziwa  Kivu nchini  Kongo.  Hata  ziwa  Victoria  pia  wanapatikana  hususani  maeneo  ya  Ukara, Ukerewe  na  Uvinza.

Kitu  kingine  kinacho  tumika  katika  tambiko  hili  ni  kunyanzi  la  mnyamna  mmoja  wa  porini  mwenye  sifa  ya  kuwa  na hasira  sana.

Vitu  vingine  vinavyo  chukuliwa  ni  pamoja  na kipande  cha  kinu  kilicho pasuka  wakati kinatwangiwa  chakula, mizizi ya  turatura  za  aina  zote  tatu. Turatura huwa  zipo za  aina tatu, zipo kubwa, ndogo  na  saizi  ya  kati. Turatura  mbali  na  kutumika  katika  tambiko  hili, lakini  pia  hutumika  katika tiba  mbalimbali  kama  vile  kutibu maradhi  ya  bawaziri  au kutokwa  na  kinyama  sehemu ya  haja  kubwa.

Sasa basi  inachukuliwa  mizizi  ya  turatura  za  aina  zote  tatu, mafuta ya usiku, vipepeo wenye  rangi  saba (  Hapa  sio kipepeo  mmoja  mwenye  rangi  saba  la  hasha. Unachukua  vipepeo saba, kila  mmoja  awe na  rangi yake ), kipande cha mti uliopigwa na  radi, pamoja  na  mti mmoja  wa  porini  ambao  jina  lake ni mwiko kutajwa hadharani   mahali  popote  pale.

Kama  utataka kuujua nitakupa  maelezo kuuhusu  halafu  wewe mwenyewe  utakwenda  kufanya  utafiti  wako  porini.

Huu ni mti  hatari  sana. Ni  mti  wenye  majini  na  maruhani wakali,wenye  nguvu  na  walio  katika  daraja  la  juu  sana  katika  ulimwengu  wa  majini  na  maruhani.

Mti  huu  una sifa  kuu  moja. Unaweza  ukafa  au kunyauka  kuanzia  mizizi  mpaka  matawi. Halafu  ghafla  baada  ya  dakika  kadhaa ukarudi  katika  hali yake  ya  kawaida.  Hii ndio  sifa  kuu  ya  mti  huu. Na  hupatikana  kwenye  mapori  makubwa.

 Usije  ukauchanganya  na  mfausiku. Huu sio Mfausiku. Huu ni mti mwingine  kabisa  tofauti  na  Mfausiku.
Vitu vyote  hivyo  vinachanganywa  kwa  kukaushwa  kisha  kupikwa  pamoja   halafu  mtu  anachukuliwa na  kwenda  kuchanjiwa  baharini, ziwani, mtoni au  sehemu  yoyote  ile  yenye  maji.

Akiwa  kwenye  maji  anakaa  kwenye  jiwe  na  kuchanjiwa  dawa  hii  huku  yakitamkwa  maneno  maalumu  ya  kimitambiko.

Kama   utakuwa  katika  mazingira ambayo hakuna  bahari, ziwa  au mto, zoezi hili  linaweza  kufanyikia  hata  nyumbani.

Unaweka  maji kwenye  beseni  au  sufuria, juu yake  unaweka  jiwe , muhusika  analikalia  halafu   anachanjwa  na  kupakwa  dawa.

Baada  ya  zoezi  hili  kukamilika zinachukuliwa  nywele   za  saluni, mzizi  ulio katisha  njia , tawi  la  mti  unaitwa  Ututukanga. Huu  mti  wa  Ututukanga  huwa  unapatikana  porini na baharini  na  una  sifa  moja  kubwa  ambayo  ni  tofauti  na  miti mingine  yote  duniani,  kwenye  mti  wa  ututukanga  huwa  linaonekana  shina  lake  na  matawi  yake  tu, lakini  mzizi  wake  huwa  hauonekani.

Vitu  vingine  vitakavyo  ongezwa  hapo  ni  pamoja  na  mzizi  wa  mti   unaitwa  Msonihya.

Vitu hivi   vinasagwa  pamoja  na  mti  unaitwa  kishindawachawi.

 Baada  ya  hapo  anachukuliwa  kuku  mweusi, anafungwa kwenye kitambaa  cheusi  bila  kumchinja, unachukua  chungu  cheusi, unamuunguza  mpaka  anakuwa  mkaa, halafu  unamsaga  pamoja  na  miti  iliyo  tajwa  hapo  juu, unachanganya  na  mafuta  ya  simba .
Baada  ya  hapo  unachukua  buja ama  dulya  la  ugali  wa  kilioni  kisha  unachukua kamba  ya  kitanda  alicho  lalia  maiti, au kama  maiti  ipo  kwenye  nyumba  ya  nyasi, unachomoa  nyasi  wakati  maiti  imo  ndani  halafu  naenda  kuchimba  mzizi  wa  mti  unaitwa  mputika  bila  kivuli chako  kugusa mti wala  kuhema  wakati  unauchimba  mti  huu..

Unaunguza   vitu  vyote  hivi   kwa  pamoja  ukiwa  na  kaniki  nyeusi  bila  kuvaa  nguo  yoyote  usiku wa  manane  njia  panda

Ukisha  changanya  vitu  vyote  hivi  unavipika  njia  panda pamoja na  mafuta  ya usiku huku  ukiwa  umevaa  kaniki  nyeusi  bila  nguo  yoyote  ndani.

Baada  ya  hapo, mtu  atachanjiwa  au kujichanja mwenyewe na kuoga au  kuogeshwa dawa hiyo.

Basi wachawi  watakuwa  wakijaribu  kutaka  kukutupia  uchawi, wanakuwa  hawakauoni  kwenye  rada  zao za  kichawi.


Katika  ulimwengu  wa  jadi , kinga  huwa  ni jambo  la  muhimu sana  kuliko  kitu  chochote  kile. Wachawi , majini wabaya  na  watu  wabaya  huanza  kuwafatilia  watu tangu  wakiwa  tumboni  mwa wazazi  wao.

Ndio maana unashauriwa kumtengenezea   mtoto   wako kinga  mara  tu anapo zaliwa.

Familia  zinazo  zingatia  mila na  desturi  watoto  wao huwa  hawasumbuliwi na  wachawi .
Hii ni kwa  sababu  wanajua  namna  ya  kuwakinga  watoto  wao  dhidi  ya  ubaya.

Zipo njia  nyingi  nzuri  na   za  uhakika  za  kuwakinga  watoto  dhidi  ya  uchawi pindi  wanapozaliwa.

Ifuatayo   ni   mojawapo   kati  ya  njia  hizo. Mtoto  akishazaliwa  na  kitovu  kikakatika, basi  kinachukuliwa kitovu hicho, kinafanyiwa  tambiko  maalumu na  kwenda  kuzikwa  kwa  tambiko  maalumu  kwenye mti wa Msufi.

Hakuna  mchawi  yoyote  Yule  atakae  weza  kumloga  mtoto huyo mpaka  anaingia kaburini.

Mti  wa  sufi  una  maruhani  wakali  sana na  wenye  nguvu  sana. Ni mti  unao heshimika  sana  katika  ulimwengu  wa  waganga.

Ukifanya  tambiko la kuzika  kitovu  cha  mwanao  kwenye  mti  wa  sufi, hakuna  mchawi  yoyote  Yule  atakaeweza  kumsumbua  mwanao.

Atajaribu lakini   atashindwa  na  kushindwa  kwake  kutakuwa  kubaya sana.  Zipo  taratibu  za  namna  ya  kufanya  wakati  wa  kufanya  tambiko la kuzika  kitovu  cha  mtoto  mchanga  kwenye  mti  wa  Msufi.

Kama  nilivyo sema  hapo  juu, wachawi  huanza  kuwaloga  watu  toka  wapo  tumboni  mwa  mama  zao.

Mke  wako  akibahatika  kupata  ujauzito  hakikisha  una mtafutia kinga  ya  hali  ya  juu  sana, kwa  sababu  wachawi  au  maadui  zake  hawataweza  kumuacha  ajifungue  salama.

 Wanawake  wengi  sana  wamepoteza  maisha  yao  au  kupata madhara  makubwa  wakati  wa  kujifungua  au  wakati  wakiwa  wajawazito kwa  sababu  ya  kufanyiwa  uchawi  na  maadui  zao.


Hapa  kwenye  ujauzito  hapa, naomba  uwe  makini  sana. Wachawi  huwa  wana tumia  uchawi  mzito  sana .

Nitaelezea  kidogo  hapa jinsi  wanavyo  fanya.  Kwanza  unachukuliwa  mti  mmoja  wa  porini  hatari  sana. Mti  huu una  majini wachafu sana na  ndio  unaotumika  kama  kiungo  katika  mafusho  mabaya  na  machafu  ya  aina  zote.
Mti huu unakaushwa  na  kusagwa, kisha  unachukuliwa  mti unaitwa kishinda wachawi,  uliosagwa pamoja  na  mti  unaitwa  mfalme wa  pori.

Mti  huu  wa mfalme  wa  pori, hutumiwa  na  kila  mganga  mkubwa. Hakuna  mganga  yoyote  mkubwa  ambae  hana  mti  huu  uitwao  mfalme wa  pori.

Baada  ya  hapo  anatafutwa  kinyonga  mwenye  mimba. Anakaushwa kwa moto  akiwa  mzimamzima  hivyo hivyo pamoja  na  mimba yake  hadi  anakuwa  majivu  halafu  ule unga  wake  ama  vumbi  lake  linaenda  kuchanganywa  na  hiyo dawa  ya  kichawi na  kupikwa kwenye  chungu  kwa  damu  ya  kinyonga  mwenye mimba  pamoja na  mafuta  ya  usiku, kisha inachukuliwa  na kufungwa  kwenye  kibuyu kidogo  au kichupa kidogo  sana.

Kitakacho  fuata  baada  ya  hapo  kama  mchawi  anajua  mahali  anapoishi  mwanamke  mjamzito  aliyekusudiwa  , basi  dawa  hiyo  inaenda  kutegwa  kwenye  njia  ambayo  mwanamke  huyo  huwa  anapita au  ambayo lazima  atapita  kwa  namna  yoyote  ile.

Huu  ni uchawi  mbaya  na  mkubwa  sana. Ndio uchawi  unaotumika  kuwatia  wanawake  ugumba. Mwanamke  anapata  mimba baada  ya  mwezi mmmoja au miwili  unatoka  halafu  baada  ya  hapo, ndio hapati ujauzito tena  katika  maisha  yake  yote.

Mwanamke huyu  atahangaika  kwa  waganga  na  waganguzi, madokta  na  matabibu  bila  mafanikio  yoyote.

Hii ni kwa  sababu  anakuwa  amefungwa  kichawi  kwa  kutumia  uchawi  huu  hatari.

Ili afunguliwe  lazima  afanyiwe  tambiko  kubwa  sana.

Huyo  mwanamke  aliye  kusudiwa, akivuka  mahali  hapo, basi ima  mimba yake  itatoka  hapo  hapo  hata  kama  ina  miezi  minane, ima atakufa  hapo  hapo, ima  atakufa  wakati  wa  kujifungua.

Na  akibahatika  mimba  ikitoka  na  akapona  (  Mara  nyingi  wanawake  wanao  pona hapa  ni  wale  wenye  mimba  changa ), basi  hatopata  mimba  tena  katika maisha  yake yote.
Hii ni kwa  sababu  kinyonga  huwa  anapata  mimba  moja tu na  huwa  haonani  na  watoto wake.  Na  ikitokea  mtu aliyetegewa  uchawi  huu  amezaa basi lazima  yeye  atakufa  na  kumuacha  mtoto  wake  yatima.

Kinyonga  akipata mimba, wakati wa  kujifungua  huwa  tumbo  lake linapasuka anakufa  na  watoto  wakitoka  wanaanza  kutembea  na  kuendelea  na  maisha  yao.

Kinyonga  huwa  hakutani  wala  kuonana  na  watoto  wake. Vinyonga  wote  ni  yatima. Hakuna  kinyonga  anae mjua  mama  ake.

 Huyu  huyu  kinyonga  anatumika  katika  tiba  ya  kumfanya  mtoto  atembee  haraka.   Tumbo  la kinyonga  likipasuka, wale watoto  wanachukuliwa  wanachomwa  moto, halafu majivu yao  yanachanganywa  na  dawa nyingine  za  kichawi  mtoto  anachanjiwa . Atatembea  haraka  sana.

Ila  sikushauri  utumie  njia  hii. Ni hatari sana. Kwanza  usitumie  kwa  mtoto  wa  kike  halafu  pili  masharti yake  ni magumu  sana. Ni  bora  utumie  njia  ya  mavi ya  panya  au  miguu  ya  kuku au njingine  ambazo  ni  bora  na  salama  zaidi.

Kinyonga akipasuka  wakati  wa  kujifungua, mkia  wake  huwa  unan’gan’gania  kwenye mti.

Basi  huwa  anachukuliwa na  mti  wake  anaunguzwa  halafu jivu lake linachanganywa  na  dawa  nyingine  za  porini  kisha  linatumikakatika  dawa  ya  kuzindika shamba dhidi ya  wezi.

Mwizi  akiingia  kwenye  shamba  hilo  hatoki. Mtamkuta  hapo hapo. Na  kama  mkichelewa. Mtamkuta  amepasuka.

Hapo  juu  tumeona  njia  moja  wapo ambayo  wachawi  wanatumia  kuwafunga  wanawake  wajawazito  wapate  matatizo  katika  kipindi cha  ujauzito wao  au  wakati wa  kujifungua.

Sasa  tuangalie  njia  ya  pili  kama  mwanamke  aliyekusudiwa  yupo mbali.

Habari  mbaya  ni  kwamba, uchawi huu  unaweza  kumshika  hata  mtu  alie  mbali. Mtu aliye  Bagamoyo anaweza  kufanya  uchawi  huu  ukamdhuru  mtu  aliyepo Ukerewe na  kinyume  chake.
Hivi  ndivyo  wanavyo  fanya ; Kama  mwanamke  mjamzito  aliyekusudiwa  kutegwa  ili apate  ujauzito  yupo  mbali, kama  vile  nje  ya  kijiji, nje  ya  wilaya, nje  ya  mkoa , nje  ya  nchi  na  kadhalika,  ulozi  huwa  unaenda  kufanyika  njia  panda.

Kwa  wale  wasio  fahamu, njia  panda  ndio  mahali  yalipo  malango  ya  kwenda  kuzimu.

Ni jambo  linalo  julikana  kwa  wachawi   wote  kuwa  njia  panda  zote duniani   zinajuana.

Njia  panda  husemezana  na  njia  panda, ni  methali  maarufu  katika  ulimwengu  wa  waganga  na  wachawi, na  mara  nyingi  hutumika  pindi  mganga  au  mchawi  anapokuwa  anataka  kushughulika  na  mtu  aliye  mbali  nae  hususani  alie  nje  ya  wilaya, mkoa, nchi  nakadhalika.

Njia  panda  hutumika  kufanya  kafara  nyingi  sana  za  kiganga  na  kichawi , moja  kati ya  kafara  hizo  ni  pamoja  na  kuvuta  watu  walio  mbali. 

Njia  panda  zote  duniani  zinajuana. Wewe  hata  kama  umekimbilia  tuseme  Nigeria, mchawi  aliyepo  Tanzania  anaweza  kutega  uchawi  kwenye  njia  panda  ya    Tanzania  kwa  kukukusudia  wewe  ulie  kimbilia  Nigeria, na  ukivuka  njia  panda  yoyote  ile  huko  nchini  Nigeria, basi  inakuwa  ni  sawa  sawa  na  umevuka  njia panda  ya  Tanzania ambayo umetegewa  uchawi  wa kukudhuru.

Madhara  yaliyo kusudiwa  kwako  hapa  Tanzania  yatakufuata  huko  huko  Nigeria.  Hata  kama  usipopatwa  na  uchawi kwa  kwa  kutegeshewa  njia  panda,  kivuli  chako  kitavutwa  hadi  kwenye  njia  panda  iliyo  kusudiwa  na  kushughulikiwa.

 Njia  panda  huwa  kuna  majini  na  masheitwani  wa  aina  zote  wabaya  kwa wazuri.  Kila  aina  ya  majini  wana   muda  na  siku  yao  maalumu  ya  kukaa  njia  panda.

Wachawi  hutumia  njia  panda  kufanya  mambo  mbalimbali  ya  ulozi.  Sasa  basi   inapotokea  wachawi  wamekusudia   kumloga  mjamzito   aliye  mbali  kama  vile  nje  ya  wilaya, mkoa  au  nchi, wachawi  hufanya  kama  ifuatavyo :

Mchawi  atakwenda  njia  panda  na  dawa  niliyo  itaja  hapo  juu  hapo  pamoja  na  fimbo  iliyo tengenezwa  kwa  mti  unaitwa  mkomoro.

Huu mti wa  mkomoro  ni  mti  wa  hatari  sana. Ni miongoni  kati  ya  miti  iliyo  katika  daraja  la  juu  kabisa  katika  ufalme  wa  wachawi.

Moja  kati  ya  matumizi  yake  ni  pamoja  na  kutumika  katika  kufufua  na  kuamsha roho  za  wafu.

Mchawi  huyo  au  wachawi  hayo  watakwenda  njia  panda  hapo, siku  maalumu  na  saa  maalumu, huku  wakiwa  wamevaa  mavazi  maalumu  yanayo  endana  na  tukio.  

Kabla  ya  kutoka  nyumbani  kuelekea  hapo  njia  panda  watatoka  wakiwa  wamejipaka  dawa  maalumu  zinazo  endana  na tukio  la siku  hiyo.

Wakifika  njia  panda  wataanza  watapiga  hodi, watatjitambulisha  kisha  watawaamsha  majini  ambao watakuwa  njia  panda  siku  hiyo na  wakati  huo, watatoa  kafara  yao  ambayo  mara  nyingi  huwa  ni  ya  ndege  au  mnyama  kisha  watatoa  maombi  yao halafu  baada  ya  hapo  watazungumza  maneno mbalimbali  ya  kichawi  kwa  muda  wa  dakika  arobaini. Baadhi  ya  maneno  hayo  ni  pamoja  na  :
“  NJIA  PANDA, WEWE  NDIO  MLANGO  MKUU  WA  KUINGIA  KATIKA  MAKAO   MAKUU  YA  UFALME  WA  DUNIANI .WEWE  UNALINDWA  NA  MAJINI  WOTE  WABAYA  KWA  WAZURI.   HAKUNA  KITU  CHOCHOTE  KILICHOPO  KATIKA  DUNIA  HII  AMBACHO  KIPO  MBALI  NA  UPEO WA  MACHO  YAKO. IMA KIWE  KASKAZINI, IMA  KIWE  KUSINI, IMA  KIWE  MASHARIKI, IMA  KIWE  MAGHARIBI, IMA  KIWE  ARDHINI.  POPOTE  KILIPO, WEWE  WAKIONA  NA  UNAYO  MAMLAKA  NA  UWEZO  WA  KUKIVUTA  NA KUKILETA  MAHALI  HAPA  NA  KUKIFANYA  VILE  UTAKAVYO. SASA  BASI  TUNATEGA  UCHAWI  HAPA  KATIKA  NJIA  PANDA  HII  TUKUFU TUKIWA  TUMEMKUSUDIA   FULANI  BIN FULANI, APATE  MATATIZO  WAKATI  WA  KUJIFUNGUA.  KAMA  YUPO  MASHARIKI, BASI  TUNAMVUTA  HAPA  NJIA  PANDA,HAPA  NDIO KATIKATI  NA  HAPA  NDIO  MAKUTANO ” ( Wakati  anasema  hivyo  anakuwa  anachora  kwa  kutumia  fimbo  ya  mkomoro  kwa  kufuata  uelekeo   wa msahariki ),

“ KAMA  YUPO  MAGHARIBI  TUNAMVUTA  HADI  HAPA  NJIA  PANDA, KAMA  YUPO  KUSINI  TUNAMVUTA  HADI  HAPA, KAMA  YUPO  MASHARIKI, TUNAMVUTA  HADI HAPA  NJIA  PANDA”

Baada   ya  hapo, hufanyika  masuala  mengine  ya  kikonikoni au  ya  kichawi.  Basi  unaambiwa  uchawi  huu  utamfuata  na  kumdhuru  mkusudiwa  mahali  popote  alipo. Kitakacho weza  kumuokoa  ni  eidha  awe  na  kinga  kubwa dhidi  ya  uchawi  huo  au  awe  Mcha  Mungu.

Kinga  ya jadi kwa  wanawake  wajawazito  zipo za  aina  nyingi.

 Katika  kitabu  hiki  nitaelezea  moja. Kwanza  anapewa  kinga  ya mwili  ambayo  watu wote  hupewa  lakini  pili, anachanjiwa  dawa  maalumu  ya  kuhakikisha  anajifungua  salama  na  mimba  haitoki.

Tiba  hii  inawasaidia  sana  hata  wale  wanawake  wenye  tatizo  la  mimba  kutoka  mara  kwa  mara.

Unachukua  dawa inaitwa  kishinda  wachawi, unasaga  pamoja  na  dawa  ya  mfalme  wa  pori,  mti  mkuu  pamoja  na  shanga  saba  nyeusi,  halafu  unatafuta  nge  saba  wenye  mimba.

Vitu  vyote  hivi  vinasagwa  pamoja  na  hiyo  dawa  na  kisha  mwanamke mwenye  shida  ya  kuchoropoka  mimba.

Akidaka  ujauzito  tu, unamchukua  unamchanja  kwenye  kinena  na  kiunoni.   Mimba  haiwezi kuchoropoka.
Atajifungua  salama  bila tatizo  lolote.

Katika  viumbe  wote  wa  Mwenyezi Mungu. Ni nge  pekee  ndio  kiumbe  ambae  akipata  ujauzito  wake  hauwezi  kutoka  hata  kitokee  kitu  gani…

Maadui  wakishindwa kukuroga  kwa  njia  ya  kukutupia  uchawi  basi  watajaribu  kukulisha  sumu  za  kichawi.
Sumu  za  kichawi   ni  mchanganyiko  wa  madawa  ya  kichawi ambayo  mtu hulishwa kwa  lengo  la  kumsababishia  maradhi  ambayo  kwa  kiasi kikubwa  dalili  zake  hufanana na  maradhi  mbalimbali  ya  kibinadamu  kama  vile  ukimwi, matende ,  kifafa  na  magonjwa  ya  akili kwa  kutaja  machache.

 Baada   ya zoezi  hili  kukamilika. Mwenye  kesi  atalala  kilingeni kwa  mganga  halafu  kesho  yake  atarudi  nyumbani.

Siku  moja  kabla  ya  kesi , ataamka  alfajiri  ya  saa  kumi  na  moja. Atafungua  mlango na  kuchukua  dawa ya  kishinda   wachawi kisha   kupuliza  pande  zote nne , huku  akitamka  maneno  maalumu  ya  kiganga  ambayo  ataelekezwa  na  mganga.  Akisha  kamilisha  zoezi  la  kupuliza  dawa  hiyo, atarudi zake chumbani  kulala  hadi  jua  litakapo  chomoza.

Jua  likichomoza  tu. Aamke  aende  kusikiliza  kesi  kama  ni  mahakamani  aende  mahamakani  na  kama  ni  kikao  cha  ofisini  au  kazini  aende  akasikilize kesi  yake  ambako  atakuta  kesi   yote  imekufa.

SEHEMU  YA  PILI  ITAFUATA  KESHO
Advertisement
tang
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )