Monday, May 22, 2017

Mwanasheria Albert Msando aomba msamaha baada ya video yake na Gigy Money kusambaa Wakitomasana

Mwanasheria mkongwe nchini, Albert Msando amewaomba msamaha ndugu, jamaa na rafiki zake waliokwazika na kukerwa baada ya video yake na Gigy Money kusambaa kwenye mitandao ya kijamiii.

Msando kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema anawaomba msamaha wote waliokwazika, wote waliokerwa na video hiyo na kwamba sisi sote ni binadamua na mwisho wa siku maisha lazima yaendelee.

“Nikikaa kimya nitakua mnafiki. Nimekosea. Kilichotokea hakikupaswa kutokea. I will be a man enough and say sorry kwa wote ambao nimewakwaza na kuwaangusha. Am so sorry. But the beauty of all this is we all are human. Kuna watu ambao wamekuwa wepesi kuhukumu. Siwalaumu. Ni sawa na ni haki yao. I made a stupid mistake. I take full responsibility. Mwisho wa siku maisha lazima yaendelee. It could have been worse. And to all those who took time to text I appreciate. Thats friendship. #TheDon #Hennessy #TheClip” aliandika Msando.

Video hiyo ilisambaa jana kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha Msando na Gigy Money wakiwa ndani ya gari, huku Msando akipitisha mkono wake juu ya mwili wa Gigy, wakati huo Gigy Money akikata kiuno huku anacheza muziki.

Baada ya video hiyo kusambaa watu mbalimbali walionyesha kuchukizwa kutokana na wanavyomfahamu Mwanasheria Albert Msando kutokana na heshima kubwa na umaarufu aliojizolea kwenye jamii.
Advertisement
tang
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )