Tuesday, May 23, 2017

Rais Dkt Magufuli ateua Naibu Kamishna Mkuu wa TRA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Uteuzi wa Bw. Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru umeanza  tarehe 22 Mei, 2017.

Kabla ya uteuzi huo Bw. Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru alikuwa Kamishna wa Sera, Wizara ya Fedha na Mipango.

Bw. Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Charles Edward Kichere ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa Kamishna Mkuu wa TRA.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
Advertisement
tang
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )