Wednesday, May 31, 2017

Rais Magufuli afanya uteuzi wa Naibu Magavana wawili wa Benki Kuu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 31 Mei, 2017 amefanya uteuzi wa Naibu Magavana wawili wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Yamungu Kayandabila kuwa Naibu Gavana anayeshughulikia Uchumi na Fedha (Economic and Financial Policies – EFP).

Kabla ya uteuzi huu Dkt. Yamungu Kayandabila alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazina anachukua nafasi iliyoachwa na Dkt. Natu E. Mwamba ambaye amemaliza muda wake.

Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Bernard Yohana Kibese kuwa Naibu Gavana anayeshughulikia Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha (Financial Stability and Deepening – FSD).

Kabla ya Uteuzi huo Dkt. Bernard Yohana Kibese alikuwa ni Mtaalamu wa Uchumi na Fedha wa BOT na anachukua nafasi iliyoachwa na Lila H. Mkila ambaye amemaliza muda wake.

Uteuzi huu unaanza mara moja.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
31 Mei, 2017
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )