Monday, May 8, 2017

Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa Amenunua Hisa Za Vodacom Zenye Thamani Ya Tsh Milioni 20

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa amenunua hisa za kampuni ya Vodacom Tanzania PLC zenye thamani ya Tsh. milioni 10 pamoja na nyingine za Tsh. milioni 10 kwa ajili ya mke wake, Mary Majaliwa ili kuwahamisha watanzania kuwekeza katika uchumi unaokuwa kwa kasi.

Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo Ijumaa, Mei 5, mwaka huu wakati akizungumza na waandishi wa habari mbele ya wakuu wa Masoko ya Hisa na Dhamana; Soko la Hisa la Dar es Salaam, viongozi wa Baraza la Uwezeshaji na kampuni ya Vodacom katika ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amewasihi Watanzania walioko ndani na nje ya nchi wachangamkie fursa ya kununua hisa hizo ili waweze kuwa wamiliki wa kampuni kupitia hisa zao. “Hii ni fursa kwa Watanzania kumiliki kampuni. Ukinunua hisa, unashiriki kikamilifu kumiliki kampuni na pia unaboresha uchumi wako binafsi. Ninawasihi Watanzania wote tumieni fursa hii kununua hisa hizo kabla muda haujaisha ili kuboresha uchumi wetu,” alisisitiza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao alimhakikishia Waziri Mkuu kuwa Vodacom Tanzania itaendelea kuimarisha teknolojia yake ili kuwaunganisha watanzania na kuwezesha kukuza uchumi binafsi. Vodacom Tanzania ilianza kuuza hisa za awali mwezi Machi mwaka huu na mwisho wa kuuza hisa hizo itakuwa ni Mei 11, 2017.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa  akielekezwa jinsi ya kujaza fomu  za kununua hisa  za Vodacom Tanzania PLC na Mkurugenzi wa wakala wa hisa wa Orbit Securities,Gerase Kamugisha  (kushoto) wakati alipokuwa akinunua hisa zake na mke wake Mary Majaliwa(hayupo pichani)zenye thamani ya shilingi milioni 20 katika hafla fupi  iliyofanyika ofisini kwake  jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwekezaji,Bi.Beng’i Issa  na Mkurugenzi  Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC,Ian Ferrao.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa  akiongea wakati wa hafla ya ununuzi wa hisa za Vodacom Tanzania PLC  iliyofanyika Ijumaa ofisini kwake jijini Dar es Salaam, wapili kutoka kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwekezaji Bi.Beng’i Issa ,Mkurugenzi  Mtendaji  wa Vodacom Tanzania  PLC,Ian Ferrao na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn Mworia.

Unaweza kununua hisa kupitia mawakala walioidhinishwa na Mamlaka ya Masoko na Mitaji (CMSA), Benki ya NBC au kupitia M-Pesa kwa kubonyeza *150*36#. Tembelea vda.cm/vodacomshares kufahamu mawakala hao na kupata maelezo zaidi.
 

Makundi mbalimbali ya watu wanaendelea kununua hisa za vodacom kwa ajili ya maisha ya baadae. Uuzwaji wa hisa za awali bado unaendelea hadi tarehe 11/05/2017. Waziri Mkuu kaonesha amechangamkia fursa nasi tusibaki nyuma tuwekeze katika uchumi unaokuwa kwa kasi.

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )