Tuesday, June 6, 2017

Anna Mgwira kuapishwa leo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro

Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli anatarajia kumuapisha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mteule Anna Elisha Mghwira leo Juni 6, 2017 saa 3:30 asubuhi hii Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Anna Mghwira anaapishwa leo baada ya kuteuliwa wiki iliyopita kuchukua nafasi ya Said Meck Sadick aliyeomba kujiuzulu.

Hadi wakati huu hakuna taarifa rasmi iliyokuwa imetolewa na Chama cha ACT Wazalendo kuhusu uteuzi wa mwenyekiti wao, na wala mteule huyo hajazungumza jambo lolote.
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )