Sunday, June 4, 2017

SORRY MADAM -Sehemu ya 66 & 67 (Destination of my enemies)

 MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWAILIPOISHIA

ILIPOISHIA
Ukelele wa kulia kwa uchungu ulio tokea juu kabisa ya gorofa ukawafanya wote watatu kustuka hususani Shamsa ndio alishtuka zaidi, akajitoa mikononi mwa madam Mery na kuanza kukimbilia kuelekea gorofani, huku Madam Mery na Sa Yoo wakimfwata kwa nyuma. Wote watatu wakamkuta Black Shadow akiwa amepiga magoti chini, akilia kama mtoto huku sura yake akiwa ameiinamisha kwenye mwili wa Sabogo ulio lala chini kwa kunyooka ukishiria kwamba Sabogo amepoteza maisha.
“Babyyyy……..”
Shamsa aliita huku akikimbilia sehemu alipo Black Shadow, na kuwaacha Sa Yoo na Madam Mery wakiwa wamesimama wasijue ni nini cha kufanya.

ENDELEA
Shamsa akazidi kumsogelea Black Shadow, taratibu akamgusa begani jambo lililo mfanya Black Shadow kujiifikiria kwa muda kabla hajainyanyua sura yake kwa maana anamtambua vizuri Shamsa kwamba ni mwanae wa kumlea japo Shamsa hatambui ukweli wa aina yoyote.

‘Liwalo na liwe’
Black Shadow alizungumza huku taratibu akinyanyua kichwa chake kutoka katika mwili wa Sabogo aliye iaga dunia kwa kupigwa risasi na Lee Si. Taratibu Black Shadow akaigeuza sura yake na kumtazama Shamsa aliye stuka na kuyatoa macho yake, mstuko huo haukuwa kwa Shamsa peke yake, bali Madam Mery pamoja na Sa Yoo nao wakabaki wakimkodolea macho Eddy kwani wote walili wanamtambua vizuri hususani madam Mery aliye kuwa mwalimu wa Eddy tangu akiwa kijana mdogo.
“EDDY………”
Shamsa aliita huku akiwa bado hayaamini macho yake, mwili mzima Shamsa akahisi unamuishia nguvu. Taratibu Shamsa akajikuta akianguka kwenda chini, kabla hajafika chini Eddy akamdaka, Shamsa akazimia.

“Shamsa, Shamsa, Shamsaa”
Eddy alimuita Shamsa ila hakuitika kwa haraka Eddy akamnyanyua Shamsa na kumuweka begani mwake na kuanza kutoka kushuka kwenye jengo hilo huku Madam Mery na Sa Yoo wakifwata kwa nyuma wote wakionekana kuchanganyikikwa. Wakafika chini Eddy akataka kupanda pikipiki yake, ila Sa Yoo akamuomba watumie gari ambalo walikuja nalo.

“Lete funguo”
Eddy alizungumza mara baada ya kumuingiza Shamsa ndani ya gari, Sa Yoo akamkabidhi Eddy funguo na wote wakaingia kwenye gari, wakaondoka eneo hilo. Hapalukwa na mtu aliye weza kuzungumza kitu cha aina yoyote, kila mmoja alimfikiria Shamsa aliye laza kichwa mapajani mwa Madam Mery huku Sa Yoo akiwa siti ya mbele mara kwa mara aligeuka nyuma kuwez akumuangalia Shamsa.

“Unaelekea wapi?”
Sa Yoo aliuliza baada ya kuona wanaelekea nje ya mji. Eddy hakujibu kitu chochote zaidi ya kuongeza mwendo kasi wa gari hadi wakafika kwenye msitu mmoja mkubwa. Eddy akakunja kushoto kwenye barabara ndogo iliyo jaa nyasi nyingi. Akaongeza mwendo kasi hadi wakafanikiwa kufika kwenye pango kubwa, ambapo Eddy kwa haraka akshuka kwenye gari na kumtoa Shamsa, akambeba begani, Madam Mery na Sa Yoo wakamfwata kwa nyuma pasipo kuuliza ni wapi wanapo ingizwa.

Madam Mery na Sa Yoo wakaonekana kushangaa mazingira ya ndani ya pango hilo lililo jengwa kwa ndani vizuri na kuna taa nyingi ambazo zinapendezesha mandhari ya ndnai ya pango hilo.
Eddy akamlaza Shamsa kwenye moja ya sofa, lililopo sebleni. Akamfungua kifungo cha suruali yake kisha akamvua tisheti aliyo vaa akabakiwa na sidiria.
“Mpeni muda wa kupumzika amepoteza fahamu huyo”
Eddy alizungumza huku jasho likimwagika usoni mwake, akashusha punzi na kuanza kuwatazama Madam Mery pamoja na Sa Yoo binti aliye msaidia kipindi anatafutwa na askari wa hapa nchini Japan.
“Kweli wewe ndio Black Shadow?”
Sa Yoo aliuliza huku macho yake akiwa amemtumbulia Eddy.
“Ndio mimi”

Eddy akamtazama Madam Mery ambaye anaonekana anajambo ambalo anahitaji kuzungumza ila anashindwa kulizungumza kwa wakati huo kutokana na uwepo wa Sa Yoo. Eddy baada ya kuligundua hilo akaanza kutembea kuelekea nje na Madam Mery akamfwata kwa nyuma.
“Umefikaje huku?”
Eddy alimuuliza Madam Mery kwa sauti nzito iliyo jaa hasira ndani yake, kwa maana kumbukumbu ya chanzo cha mtu aliye haribu maisha yake, ikamjia Eddy kichwani na Madam Mery ndio muhusika mkuu wa maisha ya Eddy kuharibika wakishirikiana na Mzee Godwin.

Taratibu Madam Mery akapiga magoti chini, huku machozi yakimwagika, kwani anamuelewa Eddy vizuri na anatambua hali aliyo kuwa nayo kwa sasa ni hali ya hasira na endapo atazungumza jambo baya basi maisha yake yapo hatarini kuondoka.
“Eddy, ninahaki ya kufa mikononi mwako, nipo tayari hata sasa hivi maisha yangu yatoke, ila nina kitu kimoja ninahitaji kuzungumza na wewe kabla hujaniua”

Madam mery alizungumza kwa sauti ya unyonge, machozi yakiendelea kumwagika usoni mwake. Kitendo cha sauti ya Madam Mery kupenya masikioni mwa Eddy kikazidisha hasira yake na kujikuta akikunja ngumi, mkono wa kulia huku mmkono wa kushoto ukimtetemeka sana.
“Sinto hitaji kusikia kitu chochote kutoka kwako, niliyaacha maisha yako kwa mara ya kwanza kwa kuheshimu msiba wa mke wangu, mwanangu na mama yangu. Ila kwa sasa nitakuua kisha atafwata Godwin”

Eddy alizungumza huku akimgeukia Madam Mery aliyepiga magoti pembeni yake. Akatamani alichomoe koo la Madam Mery kwa mkono wake wa kushoto unao tetemeka kwa hasira, ila akajikuta mkono huo ukiwa ni mzito sana kufanya jambo hilo. Madam Mery akatulia kimya, huku macho yake ameyafumba kwani anatambua ni nini anacho stahili kufanyiwa. Zikapita sekunde kadhaa za ukimya, Madam Mery akayafumbua macho yake na kumuona Eddy akiwa anaondoka kuingia ndani ya pango hilo na hajamfanya kitu chochote.
“Eddy tunatakliwa kumuua Godwin”

Eddy akasimama, kisha akageuka taratibu na kumtazama Madam Mery aliye piga magoti. Macho ya Eddy yaliyo jaa uwekundu wa hasira huku kwa mbali yakilengwa lengwa na machozi ya hasira, yakaanza kumpandisha na kumshusha madam Mery. Kisha sauti mbili moyoni mwake zikawa zinabishana kwenye kufanya maamuzi. Sauti yake ya kwanza inamtuma kumuua madam Mery muda huo huo, huku sauti yake ya piliikimuomba asifanye mauaji ya mwana mama huyo na amsikilize kwa kile ambacho Madam Mery anahitaji kumuambia.
“Tanzania pamoja na raisi Praygod wapo matatani, muda wowote na saa yoyote wanaweza kupoteza maisha……”
“Kutokana Godwin amekuwa……….Raisi wa nchini Tanzania”
“NINI…..?”
Eddy alistuka sana kusikia habari hiyo ambayo ni mbaya sana ndani ya masikio yake. Akamfwata Madam Mery kwa kasi hadi sehemu alipo piga magoti, jambo lililo mfanya madam Mery ajikute amekaa chini kutokana na kumuogopa Eddy.

“Umesemaje………..?”
“Ni…nini….memee..eeesema baa…ba yak…o Go…d……win amekuwa raisi wa Tanzania”
Madam Mery alizungumza huku mwili mzima ukimtetemeka, japo kuna baridi Eddy akajikuta jasho likimwagika kwa hasira. Kila alicho kifikiria juu ya Mzee Godwin kilimchanganya akilini mwake.
“Na Phid….aya bado yupo hai”
Maneno ya Madam Mery yakazidi kumumshangaza Eddy akilini mwake na kuanza kumkumbuka Nesi Phidaya ambaye alimfananisha na mke wake ila kitu kilicho mchanganya ni kwamba tayari alisha mzika mkewe Phidaya.
                                                                                                            ***
    Matajario mazuri ya watanzania juu ya uongozi wa Raisi Godwin, yakaanza kupotea kadri siku zilivyo zidi kwenda. WWengi walitarajia ugumu wa maisha utapungua ila ndio kwanza ukazidi kuongezeka mara kumi ya awali walivyo kuwa.

Nchi haikuwa ya watanzania wote bali, ikageuka kuwa nchi ya watanzania wachache, wenye nguvu ya kipesa na wenye maamuzi ya kufanya chochote kwa wakati wowote na kwamtu yoyote. Uonevu ukazidi kuongezeka kwa wananchi wa hali za chini, watu wote walio msaidia mzee Godwin kuingia madarakani, walikabidhiwa madaraka makubwa ambayo, hata watu wengine walio kua katika serikali ya raisi Praygod na kumuunga mkono, waliweza kupigwa chini, huku baadhi yao wakibambikiwa kesi na kusekwa magerezani, huku wengine wakifilisiwa na kubaki kuwa masikini kabisaa.

“Mzee tunatakiwa kidogo tuwajali wananchi, hata miaka mingine mitano ukigombania uraisi wakupatie kura zao”
Mshauri wa raisi wa Mzee Godwin, alizungumza huku akimtazama raisi Godwin usoni mwake. Mzee Godwin akatabasamu kidogo kisha akaachia kicheko cha dharau na kumtazama mshauri wake bwala Mgwira
“Ni nani aliye kudanganya kwamba kutakuwa na kupiga kura tena nchini Tanzania?”

“Una maana gani muheshimiwa?”
“Maana yangu ni kwamba hakuna mtu ambaye atanitoa madarakani kwa kupiga kura. Hii nchi kwa sasa ni yangu na nitaiongoza hadi pale nitakapo fariki na endapo itatokea nitakufa basi atakaye tawala atakuwa ni Manka mwanangu kipenzi”
Bwana Mgwira akabaki amemtumbulia macho mzee Godwin, anaye zungumza kwa kujiamini sana.
“Nahitaji nchi hii nibadilishe mfumo wa utawala, uwe utawala wa kifalme na si utawala wa kiraisi”
“Muheshimiwa……………..!!!”
“Ndio, na tena wasiliana na viongozi wote kesho ninahitaji kufanya nao mkutano sawa”

“Sawa muheshimiwa”
Mzee Mgwira hakuwa na kitu cha kuzungumza zaidi ya kukubaliana na raisi Praygod ambaye siku zote akizungumza haitaji mtu yoyote aweze kukipinga. Manka akaingia kwenye sebule ya baba yake na kumkuta akiwa amekaa na Mzee Mgwira, ambaye baada ya kumuona Manka akanyanyuka na kuondoka, kuwapisha baba na mwana kuzungumza.
“Baba mbona unaonekana leo una furaha sana?”
“Ninafuraha mwanangu kwa maana nimefikiria kitu ambacho nina imani kitakuweka wewe kwenye mazingira mazuri sana”
“Kitu gani hicho baba, wakati unamiliki kila kitu kwa sasa?”
“Ninakwenda kubadilisha mfumo wa serikali kutoka katika mfumo wa serikali ya uraisi na kuingia katika serikali ya ufalme”

Mzee Godwin alizungumza huku akifurahia sana.
“Ufalme, ufalme wa aina gani?”
“Nahitaji kuwa mfalme, nitakuwa nikiongoza katika maisha yangu yote na hata mimi nikifa basi wewe mwanangu utatawala katika kiti cha ufalme na utakuwa ni malkia”
Manka naye aklajikuta akitabasamu na kufurahi sana, juu ya wazo ambalo baba yake amelifikiria. Kwa nguvu walio kuwa nayo walijiamini kwamba kila kitu ndani ya Tanzania ni chakwao.
“Wezako wanaendeleaje?”
“Wapo salama tu, kila mtu anaendelea na majukumu yake kwenye wizara ambayo umewapatia”

“Basi wasiliana nao na kesho uwaambie kwamba nina kikao ambacho kitakuwa kinakwenda kuihalalisha serikali ninayo ifikiria”
“Sawa baba”
Manka akanyanyuka kwenye sofa alilo kalia akamsogelea baba yake na kumbusu shavuni na kuondoka zake sebleni na kumuacha Mzee Godwin akifikiria mambo yake.
   Siku iliyo fwata, mkutano wa viongozi wote ndani ya serikali ya Mzee Godwin wakakutana kwenye kikoa ambacho kila mmoja alishangazwa na ukubwa wa kikao hicho kwa maana tangu uongozi wa raisi Godwin uanze hajawahi kuitisha kikao kikubwa kama hicho.

“Habari za asubu”
Raisi Godwin alizungumza kupitia kipaza sauti kilichopo kwenye meza yake, kila kiongozi aliye kuwepo kwenye eneo hilo aliitikia. Raisi Godwin akawatizama viongozi walio chini yake kisha akakohoa kidogo na kuanza kuzungumza kitu ambacho alikusudia kukizungumza.
“Ninahitaji kubadilisha mfumo wa serikali”
“Serikali ambayo ninahitaji iwe kwa sasa, itakuwa ni serikali ya ufalme, na hili swala sinto hitaji mtu wa iana yoyote kuweza kulipinga hili”

Minong’ono ya chini chini ikaanza kutawala ndani ya chumba cha mkutano, kila mmoja aliweza kuzungumza chake juu ya kitu kilicho zungumza na Raisi Godwin.
“Kuna baadhi ya sekta nitazifuta rasmi kuanzia leo na sekta ya kwanza itakuwa ni Tume ya taifa ya uchaguzi”
“Eheee bwana Luka unahitaji kuzungumza nini?”
“Muheshimiwa raisi wazo lako ulilo litoa si baya, ila itakuwaje kwa hao wananchi ambao tuna waongoza, watakubaliana kweli na hili?”

“Jeshi tunalo, nguvu ya pesa tunayo ni nani anayewezakupinga kauli yangu?”
Raisi Godwin alizungumza na kuwafanya viongozi wote kuwa kimya wasizungumze neno la aina yoyote.
“Ninaagiza waziri wa mawasiliano, vijulishe vyombo vya habari namuwatangazie juu ya hili nililo zungumza sawa”
“Sawa mkuu”
“Na kitu cha mwisho ambacho labda nitawahurumia wananchi wangu, waweze ku[iga kura za ndio na hapana kupitisha serikali ninayo itaka na watakao kataa. NITAJUA NI NINI CHAKUFANYA”

==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )