Monday, June 26, 2017

SORRY MADAM -Sehemu ya 74 & 75 (Destination of my enemies)

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
  Hisia za mapenzi zikazidi kupanda kati yao, mikono ya Eddy ikawa na kazi ya kupita kila kona ya mwili wa Phidaya. Kwa nguvu alizo nazo akamnyanyua na kumkalisha kwenye sehemu maalumu ya kunawia mikono. Hapakuwa na mtu aliye kuwa na kipingamizi cha kumpatia mwenzake denda la kutosha.
Kwa haraka Phidaya akaanza kuufungua mkanda wa suruali ya Eddy, hakuishia hapo akafungua na zipu ya suruali hiyo na kiganja chake akakiingiza sehemu lilipo tango lililo simama kidedea.
Viganga vya Eddy vikawa na kazi ya kuyaminya minya mziwa ya Phidaya yaliyo simama vizuri.
“Eddy tizama nyuma yakoooo”
Phidaya alizungumza kwa sauti ya juu huku macho yakimtoka huku kiganja chake akikitoa sehemu lilipo tango la Eddy

ENDELEA
Kitendo cha Eddy kugeuka nyuma, akakutana na ngumi nzito iliyo tua usoni mwake na kumfanya apate kizunguzungu cha gafla. Kwa haraka Phidaya akaiweka nguo yake vizuri, huku macho yake yopte yakiwa kwa mwanaume aliye jazia misuli.

Mwanaume huyo aliye ingia ndani ya choo hicho, kwa lengo la kujisaidia haja ndogo. Ila alipo iona sura ya Eddy, akatambua ya kwamba ndio mtu wanaye mtafuta katika kundi lao lenye watu wengi karibia dunia nzima. Eddy akajaribu kusimama, ila mwanaume huyo aliye na umbo refu kwenda juu na mwenye kifua kilicho gawanyika kwa mazoezi makali aliyo yafanya. Akampiga Eddy teke moja lililo tua kwenye mbavu na kumfanya Eddy kutoa ukelele mkali wa maumivu.

Phidaya bila ya kujifikiria mara mbili akamrukia mwanaume huyo mgongoni na kunaza kumpiga makofi ambayo kwa ukakamavu wa mwanaume huyo hayakuwa na maumivu ya aina yoyote. Kwa nguvu alizo nazo mwanaume huyo akamshika Phidaya kwa mikono yake yote miwili na kumrushia kwenye moja ya kioo cha ukutani mwa  choo hicho, kitendo kilicho mfanya Phidaya kugugumia kwa maumivu makali huku damu zakimtoka kwenye upande wake wa kushoto ambao alipigizwa kwenye kioo hicho kilicho pasuka.

   Mwanaume huyo hakutaka kudili sana na Phidaya, akamsogelea Eddy ambaye anajizoa zoa kunyanyuka kutoka chini. Akamshika kwa mikono yake yote miwili na kumyanyua usawa wake. Akampiga Eddy kichwa kimoja cha uso kilicho mzidisha Eddy kulegea kwa kukosa nguvu.

Akiwa emeendelea kumshikilia Eddy akamtandika kichwa cha pili cha uso kilicho mfanya Eddy kutulia tuli na kupoteza fahamu. Mwanaume huyo pasipo kuchelewa, akamuweka Eddy begani mwake, akamtazama Phidaya anaye gugumia kwa muamivu makali chini alipo lala. Akataka kutoa bastola na kumpiga Phidaya, ila akamuonea huruma kwa maana si muhusika katika sekeseke hilo.

Akafungua mlango wa kutokea kwenye choo hicho. Akachungulia pande zote mbili za kordo hiyo ndefu ila hakuona mtu yoyote akikatiza. Alipo hakikisha usalama upo, taratibu akaanza kutoka na kutembea kwenye kordo hiyo kuelekea nje, huku Eddy akiwa amembeba begani.

    Mwaname huyo mwenye asili ya kiarabu, aliye changanyia na asili ya Kirusi(Russia). Akazidi kutembea kwa kwa kujiamini kwenye kordo hiyo hadi akafanikiwa kufika sehemu ya mapokezi ambapo ndipo kuna lango la kutokea kwenye hospitali hiyo. Manesi na watu walipo kwenye eneo hilo, wakabaki wakimshanga mwanaume huyo.
“Samahani muheshimiwa, mtu huyo unampeleka wapi?”
Askari mmoja wa ulinzi wa eneo hilo alimsimamisha mwanaume huyo, aliye mbeba Eddy.

“Ni ndugu yangu nimekuja kumchukua nimrudishe nyumbani”
“Mbona huyo ni mwafrika na wewe si muafrika imekuwaje akawa ni ndugu yako?”
Mwanaume huyo akaka kimya huku akiwatazama askari wawili wanao sogelea eneo hilo, baada ya kumuona mwenzao akimuhoji mwanaume huyo mwaswali. Mwanaume huyo akamtazama askari huyo anaye muhoji maswali anayo hisi yanampotezea wakati. Taratibu akaurudisha mkono wake wa kulia nyuma, ili kuichomoa bastola yake aliyo ifunika na jaketi lake zito.

“Ahaaaaaaaaaa bastolaaaaaaa”
Binti mmoja aliye kaa kiti cha nyuma ya jamaa huyo aliweza kuona kitendo anacho taka kukifanya jamaa huyo. Askari wawili ambao wanao mfwata jamaa huyo wakaongeza mwendo huku kila mmoja akijaribiu kuwahi kuichomoa bastola yake kiunoni mwake. Kufumba na kufumbua wakastukia wakitupiwa Eddy, ikawabidi wamdake na wote wakaanguka chini. Askari aliye simama karibu yake aliye kuwa akimuhoji maswali, alistukia akitandikwa teke la sehemu za siri lililo mfanya ajikunje huku akilia kwa maumivu makali sana.

Askari wengine walipo eneo hilo wakaongezeka kukabiliana na mwanaume huyo, ambaye tayari alisha ichomoa bastola yake na kuanza kukabiliana na askari wanamfwata huku wakiwa wameshikilia mitutu ya bunduki. Watu wote waliopo katika eneo hilo la mapokezi walijikuta wakilala chini huku wachache wakiamua kukimbilia nje kuyaokoa maisha yao.

Mashambulizi ya polisi na mwauamue huyo yalizidi kuwa makali, baada ya mwanaume huyo kujibanza kwenye moja ya nguzo iliyopo katika eneo hilo. Iliyo msaidia kukinga risasi zinazo toka kwa askari. Macho ya mwanaume huyo muda mwingi yaliweza kumtazama Eddy aliye lala mita chacha kutoka sehemu alipo jificha na ni ngumu kwa yeye kuweza kumchukua kwa maana akifanya hivyo basi risasi za askari wanao ongeze kila muda basi zinaweza kuishia kwenye mwili wake.

Mwaname huyo aliye fika hospitalini hapo kwa lengo la kumtembelea bibi yeka, aliye lazwa kwenye hospitali hiyo, lengo lake liliweza kuvunjika baada ya kuibanwa na haja ndogo na kuingia kwenye moja ya choo ambacho pasipo kutazama kama kimewekewa tangazo la matengenezo, alijikuta akiingia tu kuitua haja yake hiyo na ndipo hapo alipo weza kumuona Eddy akiwa na Phidaya kwenye choo hicho wakiendelea kuogelea kwenye dibwi zito la mahaba. Alipo hakikisha kwamba mtu huyo ndio wanaye mtafuta baada ya kuiangalia picha ya Eddy kwenye simu yake, ndipo alipo amua kufanya shambulizi lililo mzidi Eddy na kumchukua kiurahisi.
“F……k”
Mwanaume huyo alizungumza huku akimtazama Eddy kwa macho ya hasira. Akachomoa magazine ya bastola yake na kukuta ikiwa imesalia na risasi tano tu na wingi wa askari hao ni mkubwa kuliko wingi wa risasi zake.

“I wiil be back”(Nitarudi tena)
Mwanaume huyo alizungumza huku akijiandaa kukimbia kwa kutokea kwenye moja  mlango mmoja wa kioo uliopo mbele yake. Akaikoki bastola yake vizuri akafyatua risaasi mbili kuelekea walipo askari, kisha akachomoka kwa kasi kubwa, na kuwaacha askari wakifyatua risasi ambazo zote zilipita pembeni. Mwaume huyo akadandia pikipiki yake kubwa aliyo kuja nayo na kuondoka eneo hilo la hospitaloi kwa mwnedo  kasi.
                                                                                                       ***
   Milio ya risasi iliweza kusikika eneo zima la hospitalini. Mlinzi mmoja anaye linda jengo la kuhifadhia maiti(Mochwari). Kwa woga akajikuta akifungua mlango na kuingia ndani ya jengo hilo huku akihema. Kitendo cha mlinzi huyo kuingia ndani ya jengo hilo Shamsa aliweza kuona  sehemu mwanga wa mlango ulipo tokea na mtu huyo kuingia ambaye hakujua kwamba ni nani. Kwa haraka Shamsa akaanza kutembea kwa haraka kuelekea eneo la mlango huku akiomba msaada.

Mlinzi huyo akasikilizia sauti ya msichana huyo inayo omba msaada akahisi labda ni wenge la woga wake, kwa maana tangu afanye kazi hiyo ni mwaka wa kumi na mbili hajawahi kusikia wala kuona kitendo kama hicho kilichopo mbele yake. Kwa haraka mlinzi akakimbilia swichi ya kuwashia taa. Kwa haraka akawasha taa, eneo zima la ndani likatawala mwanga.

Macho ya mlinzi yakakutana na macho ya Shamsa, ambaye alishuhudia akiingizwa humu ndani maasaa machache yaliyo pita, ikisadikia kwamba amefariki dunia.
“Usinisogelee”
Mlinzi huyo alumuambia Shamsa huku akiwa ameishia bastola yake mkononi na mwili mzima akitetemeka kwa woga.
“Naomba unisaidie kaka yangu”
Shamsa alizungumza huku akiwa amesimama, akifwata amri ya mlinzi huyo anaye onekana kuwa na woga mwingi.
“Wewe umekufa”
“Nimekufa!?”
“Ndio umekufaaa”

Mlinzi huyo alizungumza hivyo huku akijikaza tu, ila miguu yake na mikono yake ilionyesha kwamba anashindwa kusimama kutokana na woga mwingi ulio mjaa. Shamsa akatazama eneo alilopo, hapo ndipo akaelewa kwamba sehemu aliyopo ni katika chumba cha kuhifadhia maiti.
“Ahaa……ka…aaka mi sijafaaa”
Shamsa alizungumza huku machozi yakimlenga lenga.
“Tazama viungo vyangu sijafa kabisa, ona niniatembea”
Shamsa akapiga hatua mbili mbele na kiumfanya mlinzi kuishikilia vizuri bastola yake na kumuamrisha tena asimama alipo kwa maana haamini kama Shamsa ni binadamu wa kawaida.
“Ukisogea nakumwaga ubongo zombie mkubwa weee”
Mlinzi huyo alizungumza huku akirudi rudi nyuma kuufwata mlango wa kutokea sehemu ulipo.       
                                                                                                        ***
   Sa Yoo na Raisi Praygod walibiki wakisikilizia milio hiyo ya risasi wakiwa nje ya chumba alicho ingizwa Rahab kwa ajili ya kufanyiwa matibabu.
“Kumevamiwa”
Raisi Praygod alizungumza huku akihema kwa woga, wakawaona askari kadhaa wakikatiza mbele yao wakikimbilia sehemu kunapotekea milio ya risasi. Sa Yoo baada ya kuona hivyo na yeye akaanza kufwata kwa nyuma.

“Wee Sa Yoo rudi hapa”
Raisi Praygod alijaribu kuita ila Sa Yoo tayari alisha fika mbali. Sa Yoo akafika sehemu ya mapokezi. Katika kuangaza angaza Sa Yoo akamuona Eddy akiwa amelala chini akiwa hajitambui. Mapigo ya moyo yakaanza kumenda mbio. Kwani hakujua ni kitu gani kimempata Eddy, kila alivyo tizama jinsi askari wakirushiana risasi na mtu aliye jificha nyuma ya nguzo moja kubwa, huku Eddy akiwa amelala pembeni, alihisi kuchanganyikiwa.

Akataka kwenda ila risasi moja ikatua karibu na askari aliye kaa naye pembeni na kumfanya askari huyo kudoka chini na kanza kuvujwa damu. Sa Yoo kuona hivyo na yeye akalala chini huku akizidi kuchanganyikiwa. Kitu kilicho zidi kumuumiza kichwa zaidi ni jinsi Eddy alivyo baki katika sura yake ya kawaida na hakuina sura ya bandia ambayo alitengenezewa akiwa Japani.

  Sa Yoo akafanikiwa kuweza kumuona mwanaume aliye kuwa akifyatua risasi nyingi, akichomoka kwa kasi na kutoka nje katika eneo hilo. Kwa haraka Sa Yoo akanyanyuka kutoka katika eneo aliko kuwa amelala na kuanza kukimbia kueleka sehemu alipo lala Eddy. Kwa haraka akapiga magoti chini, kuitazama hali ya Eddy. Sa Yoo akaanza kuuchunguza mwili wa Eddy kama umejeruhiwa na risasi, ila hakukuta damu yoyote, ila usoni mwa Eddy kidogo kukawa na mabadiliko. Pua ya Eddy kidogo iliuweza kuvimba hakujua ni nini kilicho ifanya pua hiyo kuvimba.

“Msaadaa jamani”
Sa Yoo alizungumza kwa sauti ya juu. Menesi na madaktari wakaanza kuwashuhulikia askari majeruhi walio jeruhiwa kwa risasi ikiwemo na Eddy. Sa Yoo hakutaka kukaa mbali na Eddy akanza kufwata nyuma kitanda cha matairi alicho lazwa Eddy kinacho sukumwa na manesi wawili.
Eddy akaingizwa kwenye chumba cha huduma ya kwanza, akawekewe mirija ya gesi puani mwake. Sa Yoo hakuruhusiwa kuingia kwenye chumba hicho.
“Madam Phidaya”

Sa Yoo alikumbuka huku akiangaza macho yake huku na kule, hakujua ni wapi alipo. Kumbu kumbu ya mwisho aliyo ikumbuka ni jinsi Eddy alivyo ondoka na Phidaya huku akimburuta kutoka katika eneo la ugomvi.  Kwa haraka Sa Yoo akaanza kutembea kuelekea katika sehemu ambayo walimiucha madam Mery. Hakutumia dakika nyingi akawa amesha fika katika eneo hilo ambapo akamkuta Madam Mery akiwa amejiinamia kwenye kitia alicho kaa.
“Madam Mery umemuona wapi Madam Phidaya?”
Sa Yoo aliuliza swali ambalo fika alitambua kwamba hato jibiwa sahihi. Madam Mery akanyanyua sura yake na kumtazama Sa Yoo kisha akajibu kwa kutingisha kichwa kwamba hatambui ni wapi alipo.

“Mungu wangu, sasa itakuwaje?”
Sa Yoo alizungumza huku jasho likimwagika. Madam Mery akamtazama Sa Yoo usoni mwake na kutambua kuna kitu ambacho kinaendelea kwa maana sura yake imejawa na masha makubwa sana.
“Kuna nini kimetokea?”
“Eddy amevamiwa na majambazi”
“Ehheee……..!!?”
Madma Mery alishaanga huku akisimama kwenye kiti, habari hiyo fika ilionyesha kumstua sana Madam Mery.
“Yuu…….uuuu..po wapi Edddy”
“Yupo wodini anashuhulikiwa, hapa ninamtafuta madam Phidaya”

Kutokana na mawazo mengi Madam Mery aliisikia miliio ya risasi ila hakujishuhulisha nayo, alihisi labda ni mawazo yake ndio yanayo mtuma hivyo.  Sa Yoo akaitazama korodo ambayo Eddy na Phiday waliondoka pamoja.

Bila hata ya kuuliza akaanza kutembea kwa mwendo wa haraka kuifwata kordo hiyo iliyo ndefu na iliyo tulia, huku  madam Mery naye akifwata kwa nyuma. Wakapita kwenye mlango wa choo, kilicho wekwa tangazo kwamba kipo katika matengenezo. Sa Yoo hakukitilia maanani sana, hatua mbili mbel, akasikia sauti ya mtu akigugumia kwa maumivu kutoka katika choo hicho.

“Vipi?”
Madam Mery aliuliza baada ya kumuona Sa Yoo akisimama na kugeuka nyuma. Sa Yoo hakujibu chochote zaidi ya kuanza kurudi taratibu huku masikio yake yote na macho akiwa amevielekezea inapo tokea sauto hiyo. Akautazama vizuri mlango wa kuingilia chumba hicho, akakuta ukiwa wazi kidogo, taratibu akausukuma na kuingia ndani. Hakuamini macho yake baada ya kumkuta Phidaya akiwa amekaa kitako akijitahidi kunyanyuka. Vipande vya vioo vilivyo anguka chini vilizidi kumkata kata Phidaya pale alipo jaribu kuweka mikono yake chini ili anyanyuke.

“Madam”
Sa Yoo alizungumza huku kwa haraka huku akimfwata Phidaya. Kwa kusaidiana na Madam Mery wakamnyanyua.
“Eddy ametekwa jamani”
Phidaya alizungumza kwa shinda huku akimtazama Sa Yoo usoni.
“Yupo yupo tayari amesha okolewa na polisi”
Sa Yoo alijibu kwa haraka. Madam Meri aliweza kuiona sura ya bandia ya Eddy aliyopo juu ya sinki la kunawia mikono. Akaiokota kisha wakatoka katika choo hicho. Madam Mery hakujali tofauti zilizopo kati yake na Phidaya. Moja kwa moja wakaeleka katika chumba ambacho Eddy anapatiwa huduma ya kwanza. Manesi wakampokea na Phidaya, wakaanza kumshuhulikia.

Advertisement
tang
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )