Saturday, July 29, 2017

Dongote ameporomoka kwenye Orodha ya matajiri wa Dunia

Bilionea raia wa Nigeria Aliko Dangote ameporomoka kwenye nafasi za watu tajiri duniani hadi 105 kutoka nafasi ya 51. 

Kwa mujibu wa Jarida la Forbes limeripoti kwamba utajiri wa Dangote umepungua kutoka dola bilioni 15.4 mwaka 2016 hadi dola bilioni 12.2 mwaka huu kutokana na kushuka thamani kwa pesa ya Nigeria.

 Dangote alijipatia utajiri wake kupitia uzalishaji wa saruji, sukari, na unga wa ngano. Aligonga vichwa vya habari 2016 wakati aliposema kuwa alitaka kuinunua klabu ya soka ya Arsenal katika kipindi cha miaka minne ijayo.

Hapo juzi  Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Amazon Jeff Bezos alimpiku Bill Gates kwa muda mfupi kama mtu tajiri duniani kabla ya kushuka hadi nafasi ya pili.


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )