Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, July 6, 2017

IGP Sirro: Siku za Waharifu Kibiti Zinahesabika

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro amesema siku zinahesabika kwa wahalifu wote waliojificha mkoani Pwani ambao wamekuwa wakifanya matukio ya uhalifu ikiwa pamoja na kufanya mauaji kwa baadhi ya viongozi na askari polisi nchini.

IGP Sirro amesema hayo  jana  alipokuwa katika ukumbi wa Police Officer's Mess, Oysterbay Dar es Salaam wakati akikabidhiwa magari manne na kampuni ya kichina ya Great Wall Motors and Haval na kudai kuwa magari hayo yatasaidia kupambana na uhalifu  nchini.

"Si kawaida yangu kusema sema ila muda si mrefu nitatoa majibu ya mauaji ya Pwani" alisema Simon Sirro

Pia Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya kichina ya Great Wall Motors and Haval alisema msaada huo wa magari ambao wameutoa kwa jeshi la polisi nchini ni sehemu ya kuunga mkono juhudi kubwa za jeshi hilo katika kupambana na uhalifu nchini.

Mpaka sasa ni zaidi ya watu 30 wamepoteza maisha mkoani Pwani kwa kuuliwa na watu wasiojulikana huku wengine kadhaa wakiwa wamejuruhiwa kwa risasi na watu hao.
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )