Monday, July 31, 2017

Mbowe Aitaka Serikali Iweke Hadharani ripoti zote mbili za madini ili Kila Mtu Azisome

Serikali imetakiwa kuweka hadharani ripoti zote mbili za madini zilizoandaliwa na kamati zilizoundwa na Rais John Magufuli kuchunguza uendeshaji wa sekta ya madini nchini.

Hayo yamesemwa jijini dar es Salaam leo na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, katika mkutano na vyombo vya habari ambao ulijikita kuelezea masuala ya uchumi.

Mbowe amesema Tanzania imegeuka kituko baada Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuipatia kampuni ya Acacia ankara ya malimbikizi ya kodi yanayozidi Sh400 trilioni.

"Serikali iziweke hadharani ripoti zote za madini ili kila mtu asome na kujua kuna nini kwenye ripoti hizo. Kiasi cha kodi wanachodaiwa Acacia ni bajeti ya Tanzania kwa zaidi ya miaka 20. Hiki ni kituko," amesema.

Mbowe amesisitiza kwanza chama chake ndicho kilikuwa cha kwanza kudai mabadiliko katika sekta ya madini lakini kile kilichofanywa na serikali hakilingani na mabadiliko ambayo waliyapendekeza.

Akifafanua, amebainisha kuwa mabadiliko yaliyofanyika bungeni yamefanyika kwa papara na hayatalinufaisha taifa.
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )