Monday, July 3, 2017

Yaliyojiri Bungeni Wakati Wa Uwasilishwaji Wa Maoni Na Ushauri Wa Kamati Ya Bunge Ya Pamoja Kuhusu Muswada Wa Sheria Ya Mamlaka Ya Nchi Kuhusiana Na Umiliki Wa Maliasili

*YALIYOJIRI BUNGENI WAKATI WA UWASILISHWAJI WA MAONI NA USHAURI WA KAMATI YA BUNGE YA PAMOJA KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA MAMLAKA YA NCHI KUHUSIANA NA UMILIKI WA MALIASILI WA MWAKA 2017,LEO TAREHE 03 JULAI, 2017*.

==>Mhe. Spika aliunda Kamati ya pamoja iliyojumuisha Kamati nne za Bunge.

#Kamati hizo ni:

(a) Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini;

(b) Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria;

(c)Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii; na

(d) Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo.

==>Maudhui ya Muswada huu yanalenga kuzingatia matakwa ya kisheria ambavyo yanawekwa na Ibara ya 27 ya Katiba inayotoa wajibu kwa kila Mtanzania kulinda na kusimamia rasilimali za Umma.

==>Uchambuzi wa Muswada huu ulishirikisha wadau wa aina mbalimbali waliotoa maoni kwa njia ya majadaliano ya pamoja kwa moja kwa moja na kwa njia ya maandishi.

==>Kamati inashauri Serikali kuhakikisha utungaji wa Kanuni unafanyika mapema ili kuwezesha utekelezaji bora na wa haraka wa sheria itakayotokana na Muswada huu.

==>Serikali ianze haraka mchakato wa ujenzi wa mitambo ya kuchakata/kuchenjua Mali ghafi za raslimali nchini,ili kuwezesha wavunaji na raslimali hizo kupata huduma hiyo hapa nchini.

==>Serikali iimarishe Mfumo wa utendaji wa benki na taasisi za kifedha ili kuongeza ufanisi katika kuhudumia taasisi mbalimbali na makampuni makubwa ya uwekezaji nchini.

==>Serikali iboreshe zaidi mifumo na uwezo wa Mahakama na vyombo vingine vya utoaji haki nchini ili viweze kushughulikia mashauri yanayojitokeza na yatakayoweza kujitokeza kutokana na masharti ya uwekezaji yanayotamkwa katika Muswada huu.

*Imeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO*.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )