Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, August 15, 2017

Eneo la Maonyesho ya nanenane Dodoma sasa kujengwa viwanda

Eneo la maonyesho ya nanenane lililopo Nzuguni nje kidogo ya mjini wa Dodoma litamegwa kwa ajili ya kuanzisha viwanda.

Uamuzi huo umetangazwa leo Jumanne na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jodarn Rugimbana wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini hapa.

"Tutagawa eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 400 kwa ajili ya viwanda na litakalobakia litatengenezwa uwe uwanja wa kimataifa,"amesema.

Amesema katika maonyesho yaliyomalizika wiki iliyopita ambayo yamesimamiwa na mkoa baada ya kuondolewa kwenye usimamizi wa Chama cha wakulima (Taso) wamefanikiwa kukusanya Sh 226 milioni.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )