Thursday, August 17, 2017

Mahakama Kuu Yatupilia Mbali Tena Ombi la wale Wabunge 8 wa CUF aliotimulia na Lipumba

Wabunge wanane waliofukuzwa uanachama na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, anayetambuliwa na Msajili wa vyama vya Siasa nchini, Prof Ibrahim Lipumba, jana waliondoka vichwa chini baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam kutupilia mbali ombi lao la zuio la kupinga kuapishwa kwa wabunge wapya.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji wa mahakama hiyo, Lugano Mwandambo baada ya kusikiliza hoja zote za pande mbili, ambapo amesema kuwa mahakama imetupilia mbali hoja za walalamikaji za kuweka pingamizi kutaka wabunge wapya wasiapishwe mpaka kesi ya msingi isikilizwe.

Aidha, Mwandambo amesema kuwa mahakama itasikiliza pingamizi la walalamikaji walilofungua kupinga kufukuzwa uanachama wa chama cha wananchi CUF na mwenykiti wao Prof. Ibrahim Lipumba.

Katika maombi yao walalamikaji wanaomba kutoapishwa kwa wabunge wanane walioteuliwa na kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuziba nafasi zilizoachwa wazi na wabunge hao kwa mujibu wa katiba.

Advertisement
==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )