Saturday, August 12, 2017

Mbowe Afunguka Mazito Sakata la Madiwani wa CHADEMA Kuhamia CCM

Mwenyekiti wa (CHADEMA) na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe amefunguka na kusema ni upambavu mkubwa kutumia zaidi ya milioni mia saba kwa ajili ya kufanya marudio ya uchaguzi wa udiwani wa kata tatu baada ya madiwani wa CHADEMA kudaiwa kununuliwa na CCM.

Mbowe amesema hayo juzi alipokuwa akiongea na wakazi wa Machame Uroki akiwa kwenye ziara yake jimboni Hai na kusema fedha ambazo zinakwenda kwa ajili ya uchaguzi wa marudio zingeweza kufanya mambo mengine ya msingi.

"Gharama ya kurudia uchaguzi wa diwani mmoja ni shilingi milioni mia mbili hamsini, madiwani watatu waliopewa fedha wakaikimbia CHADEMA wakawaacha wananchi huo ni usaliti gharama ya kurudia uchaguzi kwenye kata tatu ni milioni mia saba na hamsini. 

"Hizi ni pesa zenu, hizi ni pesa za Watanzania pesa hizi zingetumia kujenga shule ya msingi kwa Kasagile, hizi ni pesa zingetumika kujenga barabara, tunaacha kujenga hospitali tunakwenda kuzitumia fedha hizi kwenye uchaguzi milioni mia saba na hamsini ni upumbavu mkubwa" alisema Mbowe
Hata hivyo Mbowe amesema kuwa licha ya madiwani hao kununuliwa hata uchaguzi ukifanyika kesho anaamini kuwa chama chake kitaibuka na ushindi kwa kata zote tatu

"Niwaambie tu CCM haki ya Mungu hizo Kata tatu haiondoki hata moja labda watu wa Uroki mniambie mko tayari tuwaachie hizo Kata, tutakesha usiku tutakesha mchana haipotei Kata hata moja waite uchaguzi hata kesho, kuna watu wanafika bei tuachane nao tuna mambo ya kupigana katika maisha yetu" alisisitiza Mbowe

Madiwani wa tatu wa jimbo la Hai walijiuzulu nafasi zao na kusema wanamuunga mkono Rais Magufuli na serikali ya awamu ya tano kutokana na utendaji wake madiwani hao ni pamoja na Diwani wa Kata ya Machame Magharibi, Goodluck Kimaro, Diwani wa Kata ya Weruweru, na  Diwani wa Kata ya Mnadani, Everist Peter Kimati ambao wote wamejiunga na CCM.
Advertisement
tang
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )