Tuesday, August 15, 2017

Q Chief: TID ana matatizo ya akili........ Naomba Aniache, Apambanane na Hali Yake!


Msanii Q Chief amemchana swahiba wake wa kipindi kirefu Khaleed Mohamed 'TID' kuwa ana matatizo ya akili na ndiyo maana anazungumza vitu visivyomuhusu kwa jamii.

Q Chillah amebainisha hayo baada ya kuwepo na ugomvi miongoni mwao hivi karibuni ambapo TID alihojiwa na EATV kuhusu suala hilo akadai yeye hamfahamu msanii anayeitwa Q chief na wala hana urafiki naye.

“Mimi naona kama watu wazima kila mtu angeangalia na kupambana  na hali yake na kuangalia jinsi gani anaweza kurudi kwenye nafasi yake ya muziki.

" Kwa nini kila siku anizungumzie mimi nahisi kuna kitu special amekiona kwangu na hataki kuniambia hivyo atakuwa ana matatizo. 

"TID ana matatizo ya kisaikolojia hivyo anatakiwa ajitathmini kiundani, kama mpaka waheshimiwa wameamua kumsaidia lazima aonyeshe muelekeo ili waendelee kuwa na imani na yeye", alisema Q Chillah.

Kwa upande mwingine, Q Chillah amesema hatopenda mambo ambayo ameimba kwenye tungo zake mbalimbali yaje kuwakuta watoto wake

Kwa sasa Q Chief anafanya vyema na wimbo wake mpya 'Naogopa' ambao ameuachia siku za karibuni.

Advertisement
==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )