Thursday, August 17, 2017

Serikali ya Zimbabwe Kumsaidia mke wa Mugabe

Serikali ya Zimbabwe imemuombea Mke wa Rais Mugabe, Grace Mugabe  kinga ya kidplomasia dhidi ya kesi ya ushambuliaji inayomkabili nchini Afrika kusini.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na maofisa wa polisi wa taifa hilo leo asubuhi zimedai kuwa hayo yamefanyika kwa mujibu wa sheria, huku wakisisitiza kwamba mwana mama huyo bado yupo Afrika ya Kusini huku wakipinga ripoti za awali zilizosambaa kwamba Grace Mugabe alikuwa amerudi nchini Zimbabwe.

Akizungumza mbele ya kamati ya bunge mapema, Kaimu Mkuu wa Polisi Lesetja Mothiba (Afrika Kusini) alisema kuwa Grace Mugabe anatakiwa aende mahakamani kulingana na sheria.

Taarifa za awali zinasema kuwa Bi Mugabe anadaiwa kutenda kosa la kumshambulia mwanamitindo mwenye umri wa miaka 20 katika hoteli jijini Johannesburg Afrika ya Kusini baada ya kumkuta na wanae alioko masomoni Afrika Kusini.
==


Advertisement
Punguzo la Bei 20% msimu huu wa Idd.Agiza saa hii ya Automatic, na lipa mzigo ukifika majiji yote TanzaniaAdvertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )