Thursday, September 7, 2017

Biteko Amkingia Kifua Spika Ndugai Sakata la Madini ya Tanzanite

Mwenyekiti wa kamati iliyotathmini mfumo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa madini ya tanzanite, Dotto Biteko amesema Spika wa Bunge, Job Ndugai hakuwaingilia walipokuwa wakitekeleza majukumu yao.

Biteko amesema leo Septemba 7 kuwa, Spika aliwapatia ushirikiano waliouhitaji ili kufanikisha jukumu lao.

Amesema hayo wakati wa kukabidhi ripoti kwa Rais John Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam.

“Katika mchakato mzima, Spika hakutuingilia hata kidogo na endapo ripoti zetu zitakuwa na udhaifu basi ni wa kwetu na si wa Spika,” amesema Biteko.

Amesema mfumo wa uchimbaji wa madini ya tanzanite ni dhaifu kiasi kwamba Serikali inanufaika na asilimia nne tu ya madini yote yanayochimbwa.

“Madini yaliyochimbwa tangu mwaka 1998 yana thamani ya zaidi ya Sh8.2 trilioni lakini katika fedha hizo, Serikali imenufaika na asilimia nne tu,” amesema.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )