Monday, September 11, 2017

Lowassa Amtembelea na Kumjulia Hali Tundu Lissu

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa yupo Nairobi nchini Kenya kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu aliyelazwa katika Hospitali ya Aga Khan, baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana.

Lissu ambaye pia ni mwanasheria wa Chadema alijeruhiwa kwa risasi tano Alhamisi Septemba 7 akiwa ndani ya gari nyumbani kwake Area D mjini Dodoma akitokea bungeni.

Katika akaunti yake ya Twitter, Lowassa ame-tweet akisema, “Earlier today i paid a visit at Nairobi Hospital to see our MP, President of TLS and dear friend @tundulissutz He is recovering well. It is Sad times for Tanzania. Let us all keep praying.”

Kwa tafsiri isiyo rasmi amesema “Mapema leo nilitembelea Hospitali ya Nairobi  kumwona mbunge, Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) na rafiki kipenzi Tundu Lissu. Anaendelea vizuri. Ni kipindi cha masikitiko kwa Tanzania. Kwa pamoja tuendelee kuomba.”

Katika tweet hiyo, Lowassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, ameweka picha akiwa pamoja na Alicia ambaye ni mke wa Lissu; Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na dereva wa Lissu Simon Mohamed Bakari.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )