Friday, September 8, 2017

Wanasheria Kenya walaani Tundu Lissu kupigwa risasi

Chama cha Wanasheria nchini Kenya (LSK) kimelaani vikali  tukio la kupigwa risasi Rais wa Chama cha Wanasheria  wa Tanganyika (TLS),  Tundu Lissu.

Rais wa LSK, Isaac Okero amesema tukio hilo limewashtua  wanasheria wote wa Kenya.

“Tumepata taarifa kwamba Lissu amepigwa risasi akiwa kwenye gari lake mjini Dodoma, kwa kweli imetushtua sana na inahuzunisha,” amesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

“Kwa pamoja tunalaani tukio hilo kwa kuwa hili limewagusa wanasheria wote wa Afrika na hata dunia kwa jumla.  Tunasikitika kwa uvunjifu wa sheria uliofanyika,’’ amesema.

Amesema Lissu anafahamika kwa kutetea haki za binadamu, hivyo wanasheria wote wapo pamoja naye katika kipindi hiki kigumu kwake na Mungu atamsaidia atarudi katika hali yake ya kawaida.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )