Tuesday, October 3, 2017

Aliyemuita Rais Magufuli ‘kilaza’ Jela Mwaka Mmoja

Mhasibu wa Shule ya Sekondari St Joseph, Elizabeth Asenga ametiwa hatiani kwa kosa la kumuita Rais John Magufuli kilaza.

Elizabeth ametiwa hatiani leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya upande wa jamhuri kuthibitisha kosa.

Mhasibu huyi anadaiwa kuandika “hakuna rais kilaza kama yeye duaniani” katika mtandao wa kijamii wa Whatsapp.

Hakimu Shaidi akitoa uamuzi wa mahakama, alimtaka mshtakiwa huyo kulipa faini ya Sh milioni tano au jela mwaka mmoja ambapo amelipa faini hiyo na kuachiwa huru.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )