Saturday, October 14, 2017

Hamisa Mobeto: Sioni Kipya kwa Diamond


Hamisa amewashangaa watu wanaodai kuwa anamtumia mtoto wake  ili kuwa karibu na Diamond  na kudai kuwa hana sababu ya kufanya hivyo.

Mrembo huyo amesema kuwa hakuna kipya anachokiona kwa Diamond kwa sasa kwani amekuwa naye kwa miaka tisa.

 "Sioni kipya wala cha ajabu mtu nimeshakuwa naye kwa miaka tisa, iweje leo niambiwe namtumia mtoto,"

 Kuhusu utata wa jina la mtoto wake Hamisa amesema akiwa na ujauzito yeye na Diamond walikubaliana wamuite mtoto huyo Abdul Latif.

 "Alitaka aitwe hivyo ili lifanane na mwane Latifa, lakini baadaye akasema aitwe Daylan ili liendane na Nillan.

 "Kuna wakati alikataa ujauzito hadharani nami nikaamua mwanangu aitwe Abdulnaseeb ila kwa sasa nimekubali anaitwa Dylan Abdul Naseeb," amesema

Advertisement
==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )