Monday, October 16, 2017

Kaimu Katibu Mkuu Ammwagia Sifa Rais Magufuli


Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa vijana  wa UVCCM Taifa Shaka Hamidu, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kwa kurejesha mwamko ndani ya chama.

Shaka amesema kuwa katika uongozi wa Rais Magufuli kama Mwenyekiti wa Chama cha CCM, UVCCM imeweka rekodi ya kupokea maombi mengi zaidi ya watu wanaowania nafasi ya Uenyekiti Taifa kwenye uchaguzi wa mwaka huu. Jumla ya vijana 113 kutoka Tanzania bara na Zanzibar wamejitokeza kuwania nafasi hiyo.

“Katika uongozi wa Dkt, Magufuli akiwa Mwenyekiti wa chama limekuwa ni jambo la historia inaonyesha jinsi gani vijana wamekuwa na mwamko na hamu ya kukitumikia chama, kwakweli anastahili pongezi na hizi ni dalili nzuri kwa Chama”, amesema Shaka.

Kwa upande mwingine Shaka amesema hivi sasa zoezi linaloendelea ni usaili wa wagombea wote walioonesha nia ya kuwania uongozi ili kuwabaini na kuwapitisha wenye sifa sitahiki. Moja ya sifa kuu ya kugombea uongozi ndani ya UVCCM ni kuwa na miaka 30 au chini ya hapo ili katika uongozi wako usizidi miaka 35 kwani kila awamu ni miaka mitano.

Nafasi zinazowaniwa katika uchaguzi huo ambao mchakato wake umeanza tangu mwezi April kwa ngazi za Shina na Tawi ni Mwenyekiti, na Makamu wake, Wajumbe watano wa Halmashauri kuu ya Taifa (NEC), wajumbe watano wa baraza kuu la umoja huo Taifa na wawakilisha wa Jumuiya hiyo katika Jumuiya nyingine ndani ya chama.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )