Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, October 6, 2017

Kijana ameahidi kummaliza Tundu Lissu atakaporudi Tanzania

Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Mafunzo na Uratibu wa Kanda, Benson Kigaila amefunguka na kulilamikia jeshi la polisi kushindwa kumkamata kijana ambaye anaendelea kuandika vitisho kwenye mtandao wa jamii juu ya Tundu Lissu.

Kigaila amesema kuwa kabla ya Mbunge wa Singida Mashariki kupigwa risasi Septemba 7, 2017 mjini Dodoma huyo kijana kupitia mitandao ya kijamii aliomba apewe ruhusa ya kumuuwa Lissu kwa mikono yake mwenyewe. Kigaila amedai kuwa kijana huyo hivi sasa ameendelea kuandika ujumbe mbaya zaidi kupitia mitandao hiyo hiyo ya jamii bila ya polisi kumchukulia hatua zozote zile.

"Sasa huyo kijana anaandika vibaya zaidi.Anasema 'Anasikitika sana kwa mtu aliyefanya hilo tukio la kumpiga Lissu...anasema alitegemea asikie Lissu amekufa siyo kwamba Lissu amejeruhiwa na anasema wanamsubiri Lissu atakaporudi Tanzania mara hii hawatafanya kosa, wanasema walifanya kosa Dodoma sasa huyu mtu awe ni yeye kweli au si yeye aliyefanya tukio hilo, awe ni mwendawazimu au si mwendawazimu tulitegemea polisi wawe wameshamkamata wapo naye wanamuuliza haya anayosema ni kwa sababu gani lakini polisi halimuoni huyo kijana" alisema Kigaila

Aidha Kigaila amesema kuwa kitendo cha polisi kutomchukulia hatua kijana huyo kinazidi kuwapa mashaka kuwa huenda wanamtambua huyo kijana lakini hawataki kumkamata kwa sababu zao binafsi.
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )