Wednesday, October 18, 2017

Picha 3 za Tundu Lissu Baada ya Kutoka Nje Kwa Mara ya Kwanza

Familia ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu imesema kwamba kwa mara ya kwanza ndugu yao alipotolewa nje kupata hewa na kuota jua kauli yake aliyoitoa alisema kuwa ni sawa na ukiwa mfungwa huoni jua, mawingu wala hupigwi upepo wa kawaida.

Katika mahojiano aliyofanyiwa Kaka wa Lissu,  Wakili Alute Mughwai Lissu amesema kwamba mara baada ya ndugu yake kutolewa nje na kukaa kwa takribani dakika 30 siyo yeye Lissu peke yake aliyefurahi bali ndugu wote waliokuwepo hospitalini hapo walifurahia mno hilo tukio.

Bw. Alute amesema kwamba awali Manesi walipanga kumtoa nje Jumamosi (Oktoba 14) na kwa kuwa Lissu alijua tunakwenda, aliwaeleza wasimtoe bali wasubiri ndugu zake wafike.

"Nilikuwa mimi na ndugu wengine. Ilipofika saa 10 jioni tulimtoa na mimi ndiye nilimtoa ICU, alifurahi na sisi tulifurahi kwa hatua hiyo,” amesema Kaka huyo mkubwa wa Lissu.

Alute ameeleza kwamba baada ya Lissu kupata upepo wa nje kwa nusu saa nzima alirudishwa wodini ambako amefafanua siyo ICU tena ingawa pia kuna ulinzi na uangalizi wa karibu na si kila mtu anaweza kumwona na kuongeza kwamba hali ya ndugu yake inazidi kuimarika huku akili  zake zikiwa  timamu.

Pamoja na hayo Alute amesema kwamba suala la kumpeleka sehemu tofauti ya matibabu ndugu yao familia ndiyo itakayoshughulika zaidi kwa ukaribu na kuongeza kwamba,  ndugu wengine wapo sehemu mbalimbali kama Kenya, Australia, Marekani, Canada ambao watabidi wajadiliane kwanza ndipo watatoa taarifa juu ya nini kinaendelea.

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )