Loading...

Tuesday, November 21, 2017

Taarifa ya Ofisi ya Makamu wa Rais kuhusu taasisi ya Samia Habari Suluhu

Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakanusha taarifa inayosambaa katika Mitandao ya Kijamii kuhusu Taasisi ya Kiraia ijulikanayo kama Samia Habari Suluhu. 

Taasisi hiyo inajitambulisha  kuwa inatoa mikopo ya fedha taslim, pikipiki na bajaji kwa wanawake wajasiriamali kwa masharti ya kuweka dhamana ya fedha taslimu shilingi laki mbili. 

Ofisi inapenda kuujulisha umma kuwa taarifa hizo ni za uongo na uzushi na zina lengo la kuupotosha umma wa Watanzania.

Makamu wa Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, hamiliki taasisi yoyote ya aina hiyo na hahusiki kwa namna yoyote na kazi za taasisi hiyo na wala haitambui taasisi hiyo.

Ofisi ya Makamu wa Rais inawataka Wananchi kuzipuuza taarifa hizo zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwani zinalenga kuleta taharuki na kupotosha Umma wa Watanzania.

Imetolewa na:
Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ikulu- Dar es Salaam
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )