Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, December 4, 2017

Kauli ya Polepole Baada ya Mbunge wa CUF Kujiuzulu na Kutangaza Kuhamia CCM

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole  amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) hakitampokea yeyote anayetaka kurudi ndani ya chama hicho bila kufuata utaratibu. 

Kauli hiyo imekuja baada ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni(CUF), Maulid Said Abdallah Mtulia kutangaza kujiuzulu nafasi zake zote za uongozi alizokuwa akizishikilia kwenda CCM.

Polepole aliyasema hayo wakati akiwahutubia wananchi wa CCM mkoa wa Mara katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mkoa wa Chama.

“Ameamua kule aliko haoni itikadi,haoni siasa, haoni mwelekeo, Chama kina baba wawili huwezi kuwa na nyumba ina baba wawili alafu utasikiliza watoto watamsikiliza nani, basi amehama,” alisema Polepole.

“Sasa mimi niko hapa Musoma mimi nitumie fursa hii anayemuunga mkono ni Rais wetu ambaye ni mwana CCM kwelikweli na ndiye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ikimpendeza afuate utaratibu akiona mazuri ya Rais yule asione vinaelea kwa mazuri yale asione vimeshushwa vimeundwa na wanaounda mambo mazuri ya Magufuli ni Chama cha Mapinduzi.”
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )