Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, December 30, 2017

Waziri Jafo Avitaka Vituo Vyote Vya Afya Kutengeneza Bustani Za Kupumzikia!

Nteghenjwa Hosseah, TAMISEMI.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amevitaka vituo vyote vya Afya Nchini sambamba na hospital za Wilaya kutengeneza bustani ya kupumzikia kwa wagonjwa wanaosubiria matibabu katika maeneo hayo.

Waziri jafo ameyasema hayo wakati akikagua Ujenzi wa miundombinu ya Afya katika Kituo cha Afya Makole kilichopo Manispaa ya Dodoma na kuutaka uongozi wa Kituo hicho kutenegenza bustani ya kisasa pamoja na kupanda miti ya kutosha ili kutunza matunzingira lakini kupendezesha eneo la hospital.

“Hili Agizo liende kwa Vituo vyote Nchini pamoja na Hospital za Wilaya zilizoko chini ya TAMISEMI kuhakikisha wanaekeleza maelekezo haya katika ameneo yote nataka hospital iwe sehemu ya kupa faraja mgonjwa kwa kupata huduma nzuri lakini pia kusubiria huduma hiyo katika maeneo yanayovutia wakati wote” Alisema Waziri Jafo.

Akikagua majengo matano yanayojengwa katika Kituo hicho cha Afya na kusimamiwa na TAMISEMI Waziri Jafo amesema ameridhishwa na Ujenzi wa miundombinu hiyo ya Afya katika Hospital ya Makole  kwani umefuata ramani zilizotolewa na Wizara, unajengwa kwa ubora na uko ndani ya muda wa Utekelezaji.

“Hivi ndio ninavyotaka wataalamu wangu kujiongeza katika baadhi ya maeneo mfano hapa Mmejenga Mabara kubwa kulingana na wingi wa wagonjwa mnaowahudumia kwa siku sasa sio kwa sababu ramani imeonyesha maabara ndogo basi kila mtu anafuata hivyo hivyo ni lazima tujiongeze kulingana na mahitaji ya ameneo yetu ya huduma” Alisema Waziri Jafo.

Akizungumzia maendeleo ya mradi Mganga Mfawidhi wa  Kituo cha  Afya Makole  amesema Ujenzi huu umesema ujenzi wa Maabara, chumba cha Upasuaji, Wodi ya Kina Mama, Nyumba ya Mganga pamoja na Ukarabati wa Kichomea Taka utakamilika mapema mwezi February 2017 na Fedha zilizopokelewa kwa ajili ya ujenzi huo zitatosha na kukamilisha ujenzi wa miundombinu yote.

Kituo cha Afya Makole ni miongoni mwa vituo 211 Nchini vilivyopokea/vitakavyopokea  Fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya Afya lengo ikiwa ni kuboresha Miundombinu ya Afya ili kuweza kutoa huduma bora kwa watanzania.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )